Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Utawala Mbovu wa Saudia

Habari:

Saudi Arabia, mojawapo ya nchi tajiri zaidi duniani, inawafungia kinyama mamia ikiwa sio maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika ikileta kumbukumbu ya kambi za utumwa za Libya kama sehemu ya msukumo wa kukomesha kuenea kwa Covid-19, uchunguzi uliofanywa na gazeti la 'The Sunday Telegraph' uligundua.

Picha za simu zilizotumwa kwa gazeti hilo na wahamiaji hao waliofungiwa ndani ya vituo vya vizuizi zinaonyesha mamia ya wanaume waliotaabani waliolemazwa na joto la Arabuni wakilala bila ya mashati katika safu zilizosongamana ndani ya vyumba vidogo vilivyofungwa madirisha. Picha moja inaonyesha kile kinachoonekana kuwa maiti iliyofinikwa kwa blanketi la rangi ya zambarau na nyeupe katikati yao. Wanasema ni mwili wa mhamiaji mmoja aliyekufa kutokana na joto jingi mwilini na kwamba wengine hawapati chakula na maji ya kutosha ili kuendelea kuishi.

Picha nyengine, ambayo inaogofya sana na kushindikana kuchapishwa, inaonyesha kijana wa Kiafrika amejinyonga katika dirisha kwenye ukuta wa ndani wenye mawe ya vigae. Kijana huyo alijiua baada ya kukata tamaa, marafiki zake wanasema, wengi wao wamekuwa kizuizini tangu Aprili.

Wahamiaji hao, wengi wakiwa na makovu migongoni mwao, wanadai kupigwa na walinzi waliowatupia matusi ya ubaguzi wa rangi. "Hapa ni kama jahanam. Tunachukuliwa kama wanyama na kupigwa kila siku," Abebe alisema, raia wa Ethiopia ambaye amezuiliwa katika moja ya vituo hivyo kwa zaidi ya miezi minne. "Endapo nitaona kuwa hakuna jinsi ya kukimbia, nitajiua. Wengine tayari wamefanya hivyo," aliongezea kupitia mtu wa kati na kati aliyeweza kuwasiliana kupitia simu ya magendo. "Uhalifu wangu pekee ni kuondoka nchini mwangu kutafuta maisha bora, lakini watatupiga kwa mijeledi na nyaya za umeme kana kwamba sisi ni wauwaji."

Saudi Arabia yenye utajiri wa mafuta kwa muda mrefu imekuwa ikiwanyanyasa wafanyikazi wahamiaji kutoka Afrika na Asia. Mnamo Juni 2019, ilikadiriwa idadi ya wafanyikazi wa kigeni 6.6 milioni ni asilimia 20 ya watu wa mataifa ya Ghuba, wengi wao wakilipwa ujira duni na aghlabu wakifanya kazi za sulubu. (Chanzo: Daily Telegraph 30/08/2020) 

Maoni:

Huku riwaya mbaya nyengine tena ya ukiukaji wa haki za kibinadamu wa Saudi Arabia ikiibuka, ni lazima tuulize maswali ni kwa nini taifa hili ambalo linadai kuwakilisha Dini tukufu ya Uislamu mara kwa mara linahusishwa na unyanyasaji wa kutisha kwa wafanyikazi wahamiaji na wakimbizi wake?

Badala ya kuwakirimu mafukara na makabwela, na kumlipa ujira adilifu yule anayetafuta ajira kama Uislamu unavyoagiza – kitendo kilichoko sasa cha kuwapa makao wafanyikazi wahamiaji kutoka Asia Kusini ndani ya mahandaki yaliyo na misongamano yasiyo na miundombuni ya usafi wala huduma za matibabu, kimeongezeka kwa ongezeko la hivi majuzi la wakimbizi kutoka pembe ya Afrika. 

Wengi wao ni waathiriwa wa mawakala wa kuajiri na walanguzi wa binadamu, waliosafiri kukimbia umasikini nyumbani kwao, lakini wakanaswa nchini Saudi Arabia upande mmoja ikiwa ni kutokana na janga la maambukizi lakini pia kutokana na mageuzi ya nguvu kazi yaliyoanzishwa mwaka jana na Muhammad bin Salman – ambaye anapaswa kuwajibika kwa hali za kinyama ambazo watu hawa wanapitia.

Viwango vya kujitoa uhai na maradhi ya kiakili kando na maradhi mangineyo yamekita mizizi miongoni mwa wafungwa hawa; ilhali licha ya hali hizi mbaya, mipango ya kuwarudisha makwao mara moja imetupiliwa mbali – ikiwaacha wanaume hawa kuteseka katika hali mbaya zaidi za kuishi watu mia ndani ya chumba kimoja. Zaidi ya hayo inaonekana kana kwamba ishara kubwa za serikali ya Saudia za kugawanya chakula na maji zinaweza kumudiwa kwa mahujaji wa Hajj na Umrah pekee, kwa sababu wanaume hawa wanadhalilishwa zaidi kupitia kupata maji kidogo mno, na wanapewa kipande kidogo tu cha mkate asubuhi na wali kidogo jiona ili kula.

Picha za satelaiti zinaonyesha kuwepo na majengo kadhaa yenye kutwapa makao wahamiaji wasio na nyaraka katika eneo la Shumaisi karibu na Makkah na mji ulio na bandari wa Jazan karibu na Yemen, kila moja likiwa na maelfu ya watu.

Wale waliowahi kutembela Ufalme huu kuna uwezekano kuwa washawahi kushuhudia ubaguzi wazi wa rangi nyuma ya mfumo wenye ngazi mbili ambao Waafrika na Waasia wanaupitia. Kuanza namna wanavyohudumiwa wakati wanapowasili, hadi katika maeneo, makaazi na mabweni wanayotengewa – kuna tofauti kubwa mno katika kuamiliwa kwao na fursa zao, ikilinganishwa na Waarabu na yeyote anayetoka Magharibi.

Chini ya Urasilimali wa Magharibi, ubaguzi wa rangi ni janga, lililoshonwa ndani ya nidhamu zake, lilipo katika kila ngazi ya jamii na mizizi yake imo ndani ya maadili na mienendo ya kijamii ya dola ya kitaifa. Lakini chuki za ubaguzi wa rangi zenyewe ziko dhahiri; zinajificha nyuma ya dhana ya tamaduni nyingi na miito ya fursa sawa – lakina mtu yeyote asiye mweupe anajua kwamba madai haya ya juu hufeli vibaya mno pindi uhalisia wake unapojaribiwa kwa idara ya mahakama, polisi na wafanyikazi. 

Vilevile Saudia kama dola ya kitaifa hutafuta fikra ya kujinufaisha kibinafsi juu ya dhana zote za akhlaqi na muamala wa kibinadamu kwa wahamiaji wake. Ajenda yake ya kitaifa ndio iliyoamua sera zake za ubaguzi wa rangi, ambapo chuki na kushuka hadhi kwa kipote cha watawala yanajitokeza kama tawi wazi la Urasilimali. Ambayo yanatoa maelezo ya unyanyasaji usio na idadi unaoelekezwa sio tu kwa wafanyikazi wa kiume pekee, bali pia mateso na mauaji ya mayaya na wafanyikazi wa nyumbani wa kike huwa hayaadhibiwi.

Kinyume na Urasilimali, nidhamu ya utawala ya Kiislamu huwathamini watu mbali na manufaa wanayoweza kutoa na haihitaji kufanya kazi kwa mujibu wa mfumo wa kidaraja au wa kitabaka. Bila ya kujali, kabila, taifa, asili, uwezo na jinsia, Uislamu humkirimu na kumheshimu pakubwa mfanyikazi, msafiri, na muhitaji, kama hukmu zake za sheria na hadith zake fafanuzi zinavyothibitisha.

Hadith za Kiislamu zimejaa mifano ya uadilifu, muamala mwema na njia za kumkirimu masikini kama alivyoonyesha mfano Mtume wetu mtukufu Muhammad (saw) yeye binafsi, maswahaba zake na vizazi vya Waislamu baada yao.

Ukweli ni kwamba mfumo wa Kiislamu unaendeshwa katika kushibisha mahitaji ya watu kwa kuondoa umasikiti kupitia ugavi adilifu, na wa usawa – na sio tu uzalishaji mwingi pekee.

Pia kama ilivyo dhihirishwa na Maanswari mjini Madina, katika kuwasaidia wahamiaji ili kuchangia katika ustawi wa taifa, na kutimiza kwa urahisi wajibu wao wa kibinafsi kama kufanya kazi ili pia kutoa.

Abdullah Ibn Umar amesema Muhammed (saw) amesema,

«أَعْطُوا اَلْأَجِيرَ أَجْرَهُ قَبْلَ أَنْ يَجِفَّ عَرَقُهُ»

Mlipeni mwajiriwa ujira wake kabla jasho lake halijakauka”; na inajulikana vyema kwamba Mtume wetu (saw) daima alihakikisha mtumishi wake anaishi, anakula na kuvaa kama yeye – bila ya kuwa chini. Vilevile Khalifah muongofu Umar bin Al-Khattab, hakutembea tu mabarabarani usiku ili kuhakikisha watu wako salama na amani; na kisha kuzisaidia familia yeye binafsi zinapokuwa zahitajia pekee – bali aligawanya chakula katika maeneo yote ya Kiislamu huku akisema anahofia kufanya dhulma kwa kiumbe chochote namna kitakavyo kuwa kidogo, kwani vyote vina haki ya kuishi kwa amani na usalama chini ya Uislamu.

Kanuni tukufu, vima na sheria za Uislamu zimeundwa na Muumba wa mbingu na ardhi Yeye Binafsi ili kuwainua wanadamu kama watu binafsi, na kama ummah. Haki yake inaweza kuleta kheri kwa kila mtu anayefikishiwa.

[وَقُلْ جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [Surah Al Isra: 81].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Maleeha Hasan

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 06 Septemba 2020 14:11

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu