Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Lengo la Erdoğan ni Demokrasia, Sio Uislamu!

Habari:

Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Uturuki na Mwenyekiti wa Chama cha AK, alihutubia washiriki katika Mkutano wa 140 wa Wakuu wa Mikoa wa Chama cha AK uliofanyika kwa njia ya video.

Katika hotuba yake, Erdoğan alieleza yafuatayo:

"Hata kama Ulaya na Amerika zitaanguka kabisa katika demokrasia na uchumi, tutaendelea kukuza taifa letu katika kila uwanja. Tumeazimia kupigana vita vivyo hivyo kwa ajili ya marafiki na ndugu zetu. Jina lake ni muundo wa Uturuki. Huwezi kupata demokrasia ya kikweli kama hii ambayo imejengwa juu ya maadili ya kibinadamu, lengo la maendeleo ya haki, mfano wa msingi wa haki na uadilifu mahali pengine popote. Insha'Allah, tutaunda muundo wetu wa 2053 sambamba na ruwaza hii. " (Shirika la Anadolu, 17.09.2020)

Maoni:

"Mlima umezaa panya" ni methali maarufu nchini Uturuki ambayo inajulikana na kila mtu. Maana yake ni: "mtu ambaye mambo makubwa yanatarajiwa kutoka kwake anajitokeza na kitu kidogo au matokeo kidogo."

Hakika, methali hii inalingana na wasifu wa kisiasa wa Rais Erdoğan. Kwa sababu Erdoğan, ambaye yuko madarakani kwa karibu miongo miwili, anaona demokrasia inafaa kwa Waislamu, ambao wanamuunga mkono kwa matarajio ya maisha ya Kiislamu, kwa lengo la kufikia 2053. Na zaidi, anafanya hivi katika kipindi ambacho anasimamia peke yake asasi za nchi na vyombo vya habari na zaidi ya hayo, anafanya hivi baada ya wakati alipofikia mamlaka kufungua Hagia Sophia kwa ibada. Kwa kweli, rai jumla miongoni mwa Waislamu nchini Uturuki ni kwamba Chama cha AK kitafanya mabadiliko kwa kile kinachoitwa mfumo wa Kiislamu mnamo 2023 ambalo ndilo lengo la Chama cha AK kabla ya 2053.

Lakini, mlima huo umezalisha panya na demokrasia iliyooza ikachezeshwa na Erdoğan na kuletea Waislamu na muundo mpya ambao ni ule unaoitwa "Muundo wa Uturuki".

Kwa kweli, suala hili ndio fungamano la mwisho la siasa za Erdoğan zilizofuatiliwa hadi leo, na haishangazi kwa wale wanaomfuata kwa uoni wa mbele na umakini. Wakati wa utawala wake, Erdogan na chama chake hawakuchukua hatua yoyote ambayo inapingana na kanuni za demokrasia. Shughuli zote katika sera za ndani na nje zilifanywa kwa kusisitiza demokrasia mwanzoni na mwisho. Mafanikio yote yaliyopatikana kupitia msaada na kujitolea kwa Waislamu, haswa Jaribio la Mapinduzi la Julai 15, ambalo lilikandamizwa na Takbirat na Sela (1) liliwekwa kwa ukali katika ukanda wa demokrasia. Fauka ya hayo, sura mbaya ya demokrasia ilijaribiwa kuonyeshwa kama kitu halali kwa kutumia hoja za kupendeza kama vile haki ya watu ya kuchagua watawala wao na kuishi kwa uhuru, ambayo yanachukuliwa kama matusi katika Uislamu.

Leo, Erdoğan, kwa kusema kuwa makafiri barani Ulaya na Amerika wanatabikisha demokrasia vibaya, anajaribu kuleta demokrasia ya kirasilimali, ambayo iko ukingoni mwa mauti, katika uhai kupitia kuwadanganya Waislamu.

Kana kwamba chanzo halisi cha shida haikuwa demokrasia yenyewe, ambayo ilichukua haki ya ubwana kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuwapa watu wanyonge, wenye mapungufu na kasoro. Kana kwamba sio demokrasia ambayo ilichipuza sheria zenye sumu kama vile "Mkataba wa Istanbul" ambao uliharibu familia na kizazi. Kana kwamba sio demokrasia iliyowasukuma watu katika umasikini na msongo wa mawazo kwa sera za uchumi zilizojengwa juu ya riba na mapato yasiyochumwa. Kana kwamba ardhi za Kiislamu hazikuvamiwa na kunyonywa kwa jina la demokrasia. Kana kwamba demokrasia sio nidhamu wa usimamizi iliyowekwa kwa nguvu na hila, ambayo ni kinyume na imani na thaqafa ya Waislamu. Kana kwamba sio fikra ya demokrasia ambayo ilivunja dola tukufu ya Uislamu, iliyodumu kwa karne 13, na kuuacha Umma wa Kiislamu bila ya kiongozi na Khilafah na kuufanya uwe rahisi kudhibitiwa mikononi mwa makafiri wa kikoloni. Kana kwamba mapinduzi ya Umma wa Kiislamu, ambayo yalisimama dhidi ya madhalimu wa Magharibi nchini Libya, Tunisia, Misri, Yemen na Syria hayakuibiwa na uongo wa kidemokrasia.

Licha ya ukweli huu wote, kuleta neno demokrasia na maadili ya kibinadamu bega kwa bega, kuzungumza juu ya haki na maendeleo kwa misingi ya demokrasia, na kujaribu kueneza demokrasia kati ya Waislamu sio chochote isipokuwa ulemavu wa kiakili. Kuweka wazi zaidi, ni kupoteza Akhera kwa ulimwengu wa mtu mwengine. Sasa, kama Ummah, tunapaswa kuona ukweli na kuwauliza maswali watawala kwa msingi wa Quran na Sunnah, na kuwaitikia wale wanaolingania Khilafah Rashidah, sio demokrasia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yıldırım

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu