Alhamisi, 17 Safar 1446 | 2024/08/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuna Tatizo Gani Sabah?

Habari:

Jana (26 Septemba 2020) jimbo la Borneo la Sabah lilionekana likienda katika upigaji kura. Matokeo rasmi ya uchaguzi wa 16 wa jimbo la Sabah yanashuhudia muungano wa Gabungan Rakyat Sabah (GRS) ukishinda kwa idadi kubwa ya viti 38 dhidi ya viti vya Warisan Plus' 32 huku wagombeaji huru wakibeba viti vitatu vilivyobaki. Kama kawaida, kampeni kabla ya uchaguzi zilikuwa moto na wagombea wakitoa ahadi huku wakikashifiana wao kwa wao. Na inafurahisha kuzingatia taarifa ya Waziri Mkuu wa zamani wa Sabah, Datuk Seri Mohd Shafie Apdal alipoulizwa kutoa maoni juu ya maswala yanayohusiana na shida za Sabah. Kama zinagatio la pembeni, Shafie alihamia upinzani wakati wa machafuko ya hivi karibuni ya kisiasa. Shafie alisema, "Watu wengine wanasema ikiwa hatutajiunga na serikali ya majimbo, basi hali itakuwa ngumu kwetu. Katika katiba, (akimaanisha shida maalum huko Sabah) ni jukumu la serikali ya majimbo ", na akaongeza:" Ima tutajiunga au la, ni jukumu lenu (serikali ya majimbo). Ikiwa watashindwa kutekeleza jukumu hilo, nitawapeleka mahakama! ”

Maoni:

Ni wazi, Shafie alimaanisha kuilaumu serikali ya majimbo ikiwa muungano wake utashinda uchaguzi ambao unaweza kusababisha serikali ya majimbo kulipiza kisasi na kukataa kuisaidia Sabah kutatua shida zake. Lakini, hii haitafanyika kwani Warisan Plus, muungano unaoongozwa na Shafie, ulishindwa uchaguzi na idadi kubwa kiasi. Pamoja na hayo, inapaswa kuwa dhahiri kwa wengi kwamba Shafie alikuwa akipiga tu mguu wake mwenyewe kukosoa shida zinazoendelea ambazo serikali ya majimbo ilishindwa kutatua huko Sabah. Kama waziri mkuu wa zamani wa Sabah, je Shafie hajitambui kuwa shida zozote zilizoikumba Sabah, zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu, kwani Sabah imekuwa chini ya utawala wa Barisan Nasional (BN) na yeye alikuwa sehemu ya BN! Jambo moja la hakika ni kuwa, hali katika Sabah inafichua sura mbaya ya demokrasia ya Malaysia. Sabah kiuhalisia ni jimbo tajiri sana lakini watu wake wamebaki maskini kwa miaka mingi. Sabah inazalisha asilimia 42 ya pato la mafuta ya Malaysia lakini sheria ya majimbo inasema kwamba haki katika maendeleo ya mafuta ya petroli iko mikononi mwa kampuni za serikali zinazodhibitiwa na serikali ya majimbo. Jimbo hili la Borneo pia linajivunia pwani ndefu zaidi na inachangia pakubwa katika sekta ya uvuvi. Kwa kuongezea, Sabah inachangia asilimia 25 ya uzalishaji wa mafuta ya nazi nchini. Pamoja na utajiri huu wote, Sabah inabaki kuwa jimbo masikini kabisa nchini. Sabah ilirekodi kiwango cha juu zaidi cha umaskini kwa asilimia 19.5, ikijumuisha familia 99,869 kulingana na Mapato ya Msitari wa Umasikini ya 2019. Kwa kweli, asilimia 50 ya watu masikini zaidi nchini wanaweza kupatikana katika jimbo hili tajiri. Sabah pia inavuta mkia nyuma ya wenzao huko Malaysia Magharibi katika takwimu za umaskini na upunguzaji usawa. Huku mgawo wa Gini kwa Malaysia ukipungua hadi 0.399 mnamo 2016, ulipanda katika jimbo Sabah hadi 0.402, na kuifanya kuwa maskini zaidi na isiyo sawa na mikoa yote nchini!

Ni wazi kwamba kuna tatizo baya mno katika jimbo la Sabah! Maoni ya Shafie yalikuwa yamefunua ubaya wa siasa za demokrasia na usaliti uliofanywa na chama chake cha awali dhidi ya watu wa Sabah. Ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi za hivi karibuni na kampeni zilizopita za jambo hilo, sio chochote zaidi ya utapeli na uongo ambao utaendelea kuibuliwa na wanasiasa wanaogombea. Watu wa Sabah na Malaysia kwa ujumla (na kwa hakika yake ulimwengu wa Kiislamu) wanahitaji kutambua kuwa katika demokrasia, wanasiasa wana uwezo wa kutumia maneno matamu na udanganyifu ili kupata mamlaka, lakini mara tu wanapopata wanasaliti uaminifu ambao wapiga kura waliwapa na watu wa kawaida wanaendelea kuishi maisha duni. Lakini, ili kuwa mwadilifu, ni dhulma kujumlisha fikra hii kwa wagombea wote. Kumekuwa na juhudi za kushughulikia usawa katika ugavi wa utajiri na maendeleo, lakini juhudi hizi bado ni ndogo kwa sababu ya ujanja wa kisiasa na ubinafsi ndani ya vyama tawala. Shida zinazotokea katika jimbo la Sabah ni chache tu ya shida nyingi zinazoikumba nchi hii kama rushwa, ufisadi, ulafi wa mamlaka, magenge, ukiritimba na zingine. Bila ya Uislamu kuwa kiini cha siasa nchini Malaysia na nchi zingine za Kiislamu, shida zile zile za zamani zitaendelea na watu wa nchi hiyo watafanya makosa mara kwa mara katika kuamini na kuunga mkono demokrasia. Waislamu hawapaswi kung'atwa mara mbili na nyoka kutoka kwenye shimo moja. Lakini tumeng'atwa mara nyingi, isipokuwa tufanye kazi na kuhakikisha kuwa Uislamu unasisiwa kama nidhamu ya utawala.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu