Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Rustam Minnikhanov na “Uchaguzi” Nchini Tatarstan

Habari:

Kuanzia 11 hadi 13 Septemba 2020, uchaguzi wa rais wa jamhuri na manaibu wa manispaa ulifanyika nchini Tatarstan. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, gavana wa sasa wa kikoloni wa Moscow, Rustam Minnikhanov, "alishinda kwa kiwango kikubwa chenye kushawishi" katika idadi ya kura. Kulingana na data rasmi, alipokea asilimia 83.28 ya kura huku wapiga kura waliojitokeza ikiwa ni asilimia 79.

Maoni:

Wachambuzi wanaripoti kuwa kulingana na mahesabu halisi ya waangalizi huru kwenye vituo vya kupigia kura ambapo haikuwezekana kudanganya idadi ya waliojitokeza, ilikuwa kati ya asilimia 22 hadi asilimia 28.5.

Mamlaka ziliurefusha uchaguzi huo kwa siku tatu, zikitoa hoja ya afueni kwa idadi ya watu na kinga dhidi ya kuenea kwa virusi vya korona. Lakini, kulingana na waangalizi, hili lilifanywa ili kuwezesha uchakachuaji kamili kupitia ujazaji kura madebeni. Kulikuwa na visa, kama kilichotokea katika kituo cha kupigia kura nambari 118 huko Kazan, ambapo mwangalizi huru mmoja alifanikiwa kunasa video ya ujazaji kura madebeni. Kinyume na sheria ya sasa, mchakato wa kupiga kura na kazi ya kituo cha kupigia kura hazikukatizwa. Kinyume chake, mwenyekiti wa PEC aliwaita polisi. Wakati huo huo, walijaribu kuiba simu ya mwangalizi huo, na kwa kutumia hoja kwamba alikuwa ameshughulishwa na hili, walifuta kumbukumbu zote za simu nyingine. Polisi, hata hivyo, walimtaka afute rekodi ya video hiyo ya ulaghai katika kuhesabu kura, na ajiondoe kwenye kura hizi. Na kesi ya kiidara ikaletwa dhidi ya mwangalizi huyu kwa "uchukuaji filamu bila idhini".

Wakati huo huo, ni dhahiri kwa kila mtu kwamba uchaguzi wa kiongozi wa Tatarstan ulifanyika rasmi kabisa, bila kuwepo mbadala wa yule wa sasa. Kiini cha uchaguzi ni kujenga hisia tu ya uhalali wa Minnikhanov kama "chaguo la watu" na pia kuficha kuporomoka kwa hamu ya watu katika mchakato wa uchaguzi.

Ikumbukwe kwamba Putin aliongea kwa kumuunga mkono Minnikhanov, kwa uaminifu wake kwa Moscow, nia yake ya kuendelea kufuata sera ya uoanishaji, ugeuzaji wa idadi ya Waislamu wa Tatarstan kuwa na tabia za Urusi, na pia kuwa tayari kwake "kugawa" rasilimali za Tatarstan pamoja na Moscow. "Hakika nitaunga mkono uteuzi wako kama mgombea wa wadhifa wa kiongozi wa jamhuri kwa muhula ujao na, kwanza, nataka kukushukuru kwa kipindi cha kazi kilichopita na nikutakie mafanikio kwa kipindi kijacho," Putin alimwambia Minnikhanov wakati wa mkutano katika muundo wa video.

Kumbuka kwamba Minnikhanov anajulikana kwa kuonyesha mara kwa mara Moscow uaminifu wake na kuwa tayari kwake kushiriki katika upeo wa juu wa uoanishaji wa Waislamu wa jimbo la Volga wakati wa urais wake. Kwa hivyo, kwa mfano, Minnikhanov mnamo 2018, wakati wa mkutano wa baraza la raisi la maendeleo ya elimu ya mwili na michezo, alipendekeza kurudisha uuzaji wa bia viwanjani. "Kwa kweli, naona aibu kuongea kama Mwislamu kuhusu bia, lakini ninawajali ndugu zetu wa Orthodox," Minnikhanov alisema wakati huo, huku kukiwa na kicheko cha kuidhinisha cha washiriki wa Urusi katika mkutano huo. "Ikiwa Waislamu wanataka kuikaribia bia kwa uhuru, tutaona," Putin alisema kwa kejeli.

Watu wa Tatarstan walidanganywa katika miaka ya tisiini, wakikubali kuhifadhi hadhi ya raia wa Shirikisho la Urusi chini ya kisingizio cha uwepo wa ule unaoitwa. "Ubwana": Tatarstan ina katiba yake na rais wake, na vile vile nguvu kubwa za bajeti zilizo ndani ya makubaliano ya 1994 juu ya uainishaji wa mamlaka kati ya Kazan na Moscow. Leo, sambamba na ukuaji wa utambuzi wa kidini na kisiasa wa watu, pamoja na kurudi kwa watu kwenye asili yake ya Kiislamu, watu wanajua zaidi na zaidi hali halisi ya mambo, wameanza kuvutiwa na historia ya ukoloni wa jimbo hili. Lakini, Moscow pia haijalala, ikiweka utambuzi wa umma nchini Tatarstan chini ya udhibiti mkali, ikikandamiza jaribio lolote ya mwamko wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shaikhetdin Abdullah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 02 Oktoba 2020 11:03
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Kuna Tatizo Gani Sabah? Haja ya Mageuzi ya Kweli »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu