Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sura Halisi ya Demokrasia Kubwa Zaidi Ulimwenguni (India) Yafichuka

Habari:

Msamaha wa kusimamisha kazi nchini India kwa sababu ya 'uwindaji wa serikali'. Mamlaka zafunga akaunti za benki baada ya kukashifiwa kwa rekodi ya haki za binadamu ya serikali. (Gazeti la The Guardina 29 Septemba 2020)

Maoni:

Kufungiwa kabisa kwa Akaunti za Benki za shirika la Amnesty International India, na Serikali ya India, ambapo ilikuja kujulikana mnamo 10 Septemba 2020, imesimamisha kazi zote za shirika hili. Shirika hili limelazimika kuachisha kazi wafanyikazi wake nchini India na kusitisha kampeni yake yote inayoendelea na kazi ya utafiti.

Serikali inayoongozwa na Chama cha Bharatiya Janata (BJP) imeituhumu Amnesty India kwa kukiuka sheria juu ya ufadhili wa kigeni, chini ya Sheria ya Udhibiti wa Michango ya Nje (FCRA), sheria iliyoshutumiwa sana kwa kukiuka sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, ili kulenga vikundi venye ufasaha. Unyanyasaji wa mara kwa mara na vyombo vya serikali ya India, ikiwemo Kurugenzi ya Utekelezaji Sheria ni matokeo ya wito usio na shaka wa uwazi katika serikali, hivi karibuni kwa uwajibikaji wa polisi wa Delhi na Serikali ya India kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika ghasia za Delhi na Jammu na Kashmir.

Unafiki wa nidhamu za kisekula za kidemokrasia katika kukuza maadili ya haki za binadamu uko wazi kwani nidhamu hizi ni nadra kuwavumilia wakati sheria zao wenyewe zinatiliwa shaka kwa ukiukaji wa haki za binadamu. India, demokrasia kubwa zaidi ulimwenguni ni mfano mwengine wa hili. Serikali ya BJP imezidi kukandamiza asasi za kiraia, inanyanyasa na kuleta kesi zenye ushawishi wa kisiasa dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, wasomi, wanaharakati wa wanafunzi, waandishi wa habari, na wengine wanaokosoa serikali chini ya uasi, ugaidi, na sheria zingine za ukandamizaji.

Hii inafichua umbile halisi na sababu ya msingi ya tatizo ambayo iko katika nidhamu ya Kidemokrasia yenyewe. Kasoro hii ya muundo wa Kidemokrasia inahitaji kueleweka ili kutambua sababu halisi bila kudanganywa na kutafuta suluhisho ambapo shida halisi iko, yaani Demokrasia. Katika demokrasia, mamlaka yako mikononi mwa watu. Kwa hivyo, dhana ya wengi wacheze dori muhimu katika chaguzi za kidemokrasia yaani kila uungaji mkono unapokuwa zaidi kutoka kwa watu, ndipo chama kinapokuwa na nguvu zaidi. Baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu na kuwa na uhakika wa kuwapata wengi katika chaguzi za mustakbali, huwafanya wazidi kuiga zile tawala za kimabavu, ambazo hazivumilii ukosoaji wowote na zinawalenga bila aibu wale wanaodiriki kusema. Kwa kukosolewa kwa sera za serikali za kibaguzi na mashambulizi kwa sheria, viongozi wanaonekana kupenda zaidi kupiga marufuku na kuyapigia kelele maoni yanayopingana kuliko kushughulikia malalamiko.

Lakini, kuhusiana na Uislamu, Khilafah iko huru kutokana na kasoro hizi ambazo asili ya demokrasia inazimiliki. Mada kuu katika Uislamu ni kuamrisha mema na kukataza maovu na kutoa ushauri wa dhati kwa watu, bila kujali ni watu wa kawaida au mtawala. Katika Qur'an, Mwenyezi Mungu (swt) anatujulisha,

]كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Surah Aal-e Imran 3:110]

Mtume (saw) asema,

«إِنَّ الدِّينَ النَّصِيحَةُ»

“Hakina Dini ni nasaha (ya dhati).” Tukasema, “Kwa nani?” Mtume (saw) akasema:

«للَّهِ وَكِتَابِهِ وَرَسُولِهِ وَأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ»

Kwa Mwenyezi Mungu, Kitabu Chake, Mtume Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wao wa kawaida.” (Muslim).

Yeye (saw) pia amesema,

«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»

“Jihad bora ni neno la uadilifu mbele ya mtawala (Sultan) jeuri.” (Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Maja).

Na Yeye (saw) amesema:

«سيد الشهداء حمزة بن عبد المطلب ورجل قام إلى إمام جائر فأمره ونهاه فقتله»

“Bwana wa Mashahidi wote ni Hamza ibn Abdul Mattalib, na mtu aliyesimama mbele ya kiongozi jeuri akamwamrisha mema na kumkataza maovu kisha akauwawa kwa hilo.” (Hakim)

Kuna njia nyingi za kumhesabu Khalifah ndani ya Dola ya Kiislamu. Inatofautiana kuanzia kwa raia wa Dola hadi vyama vya siasa [Hizb as-siyaasi], hadi Baraza la Ummah [Majlis ash-Shurah] pamoja na Mahakama ya Matendo yasiyo ya haki [Mah’kamat al-Madhalim]. Mwishowe kuhesabiwa kuliko bora itakuwa ni kumcha Mwenyezi Mungu (swt) na kujua kwamba sisi sote tutajibu kwake (swt). Wale walio na jukumu zaidi wanapaswa kumcha Yeye (swt) zaidi, kwani wana mengi zaidi ya kujibu, kuliko wale walio na jukumu dogo.

Imam al-Shafi'i alisema, "Kuna aya katika Quran ambayo kila mkosaji anapaswa kuiogopa." Aliulizwa, "Aya hiyo ni ipi?" Akajibu,

]وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيّاً]

“Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.” [Surah Maryam 19:64]”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Hameed Bin Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu