- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Macron na Ruwaza Yake ya Ufaransa Yenye Kuuchukia Uislamu
Habari:
Macron asema Uislamu 'uko katika mgogoro', ukisababisha kuzorota kwa Waislamu
'Uislamu ni dini iliyo kwenye mgogoro kote ulimwenguni leo', anasema Macron, huku akizindua mpango wa kuuhami usekula. (Chanzo: Al Jazeera Na Mashirika ya Habari)
Maoni:
Kwa nini nchi ya kisekula ya Ulaya 'yenye nguvu ya kimfumo' inadharau na kushambulia imani, utamaduni, kushajiisha matusi kwa Mtume mtukufu (saw) wa Waislamu bilioni 1.8 kote ulimwenguni, na kuwanyanyasa na kuwatenga raia wake wachache na kuwatesa wanawake wao?
Ufaransa ilikuwa ndio kitovu cha 'tamaduni tofauti tofauti' na 'wenye kujitenga' kutoka Vaudois katika karne ya 12, Huguenot katika karne ya 17, hadi katika Mapinduzi yake karne ya 18. Kwa nini basi chuki hii isiyo na mantiki, inayowaka moto wa kiitikadi, imani na sheria za mfumo ambao ulikuwa ndio cheche ya Mwangaza wa Ulaya?
Kwa nini usekula wa Kifaransa unahitaji nyundo ya dola kuwanyanyasa madhaifu wake, wengi wao wakiwa ni wachache kiidadi. Kwa nini dola huru ya kisekula inaamua kutumia njia ambazo Ujerumani ya zama za Nazi ilitumia dhidi ya Mayahudi? Au kuufinyanga Uislamu, katika mshipa wa 'Maimamu walioidhinishwa na CPC' ya serikali ya kiimla ya China?
Kwa nini wanabeba chuki dhidi ya Uislamu?
Je! Ni kwa sababu usekula haujatimiza maisha ya watu? Je! Ni kwa sababu huria haikuweza kustaarabisha kikweli na kuunganisha na hivyo basi unahitaji 'adui wa kindani' kupurukusha na kupotosha?
Labda ni kwa sababu 'muundo wa kijamhuri' wa Ufaransa umeshindwa kuleta haki halisi ya kijamii katika maisha ya raia wake, na badala yake "usawa kamili" wa Ufaransa umekitisha ubaguzi wa kimfumo. Liberté, égalité, fraternité kwa muda mrefu yamekoma kuwa na maana yoyote katika maisha ya raia wa kawaida.
Labda ni kwa sababu Covid-19 anazidi kufichua udanganyifu, dosari na mapungufu wa usekula kama mfumo uliodhoofika, usiofaa kimakusudi, usiofaa kwa jamii zilizostaarabika na za kibinadamu.
Labda ni kwa sababu 'mfumo badali' wa Uislamu ni kizingiti cha tamaa ya wazi ya Macron ya Ukoloni 3.0 huko Sahel, Sahara na Mashariki ya Kati. Labda ni kwa sababu Uislamu unatoa wito wa 'hadhara badali' ya udugu wa kweli katika jinsi, rangi, tabaka na mipaka (bandia) ya kitaifa yote. Uislamu ni mfumo wa kibinadamu na wa uadilifu, unaofaa kwa wanadamu ambao hukomboa na kufanya kazi kwa usalama na ustawi wa raia wake wote na kutajirisha bila ya haja ya kuwadhalilisha watu wachache, kutukana imani zao, wala unyonyaji wa wanyonge au masikini.
Kwa Macron na marafiki zake wa kibepari, Uislamu ndio tatizo na usekula (urasilimali wa kiliberali) ndio jibu. Kwa watu wengine wote, usekula ndio tatizo, na Uislamu ndio jibu. Mwenyezi Mungu (swt) anawaarifu walio wakweli,
]وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]
"Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!" [Al-Isrā’: 81]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Hamzah