Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ongezeko la Ukimbizi wa Watoto nchini UAE Lahitaji Majibu ya Haraka

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la Khaleej Times nchini UAE liliripoti kwamba kuna ongezeko la kutia wasiwasi la watoto wanaokimbia nyumbani. Umri haswa wa vijana hao ni watoto wa kuanzia miaka 7 hadi mabarobaro wachanga. Watoto wengi hupatikana baada ya kuripotiwa kwa polisi na kabla ya hatari yoyote kubwa kuwajia. Ongezeko la mfadhaiko kutokana na michezo ya kubahatisha mtandaoni, utamaduni wa sinema za watu wazima, mivutano ya wazazi na hofu ya utendaji duni masomoni yote yametajwa kuwa sababu ya matatizo ya watoto na wataalamu.

Habari:

Thaqafa maarufu ya Kiliberali ya Kimagharibi kwa bahati mbaya imeyapiku maadili mema ya ya Kiislamu ambayo yanapaswa kuwa nuru ya uongofu katika nyumba za Waislamu. Dola nyingi za Ghuba zinahalalisha utafutaji wa huduma kwa watoto kutoka kwa wafanyikazi wahamiaji wasiopendezwa kabisa na thaqafa ya maadili ya Uislamu. Ikiwa dori ya mama hatafahamika na kuchukuliwa kuwa kazi ya juu kabisa anayoweza kufanya mwanamke, basi ni jambo lisilokuwa na budi kuwa watoto watapuuzwa kihisia. Wakiachwa kupotoshwa na mawakala wa tabia mbaya na kunyimwa kijamii, watoto wametengwa kisaikolojia kutoka kwa fungamano la malezi ya familia. Kisha wanatolewa nje ya nyumba na kuweza kuhisi kwamba chochote, hata aina nyingine ya mateso, ni bora kuliko maumivu yanayohisiwa mahali ambapo tunapaswa kuwa hifadhi ya usalama. Mwenyezi Mungu (swt) aliweka malipo makubwa na wajibu katika kuchunga kizazi cha mbeleni cha Waislamu kama ilivyojadiliwa katika aya ya Quran;

 [يَا أَيُّھَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَھْلِیكُمْ نَارًا وَقُودُھَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَیْھَا َمَلائِكَةٌ َغِلاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَھُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [At-Tahrim 66:6]

Kutokana na dalili hii na nyingine nyingi, kina mama wa Kiislamu kamwe wasijihisi kuwa wanaweza kuwepo nyumbani kimwili lakini kutokuwepo kisaikolojia katika malezi ya watoto. Ndani ya Khilafah, shule na nyumba lazima zote zikubalike kwa ajili ya kulea watoto pamoja na msaada wa kijamii. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aurudishe mfumo huu mtukufu kwa mara nyingine tena ili watoto kamwe wasihisi haja ya kukimbia kutoka nyumbani kwao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu