Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ushindani Mkali wa Madaraka na Pesa kati ya Tabaka Tawala Unaashiria Kuporomoka kwa Mfumo wa Kisekula wa Kirasilimali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kwa uchache watu wanane waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ghasia, haswa mapigano kati ya wafuasi wa wagombea, yalivuruga uchaguzi wa awamu ya tatu wa muungano wa parishad jana... Pamoja na wahasiriwa wanane, takriban watu 53 wameuawa katika ghasia za uchaguzi juu ya kura za UP zilizokwama, ambazo zilizoanza mnamo Juni.... Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Katibu wa Tume ya Uchaguzi Humayun Kabir Khandaker, hata hivyo, alidai kuwa mbali na baadhi ya matukio ya kukosa mwelekeo, uchaguzi wa jana kwa kiasi kikubwa ulikuwa wa kusherehekewa. "Nadhani huu unaweza kuwa mfano kwa chaguzi zote," alisema.

Maoni:

Kutokana na matukio ya mara kwa mara ya wizi mkubwa wa kura, watu wa Bangladesh tayari wamepoteza hamu yao katika uchaguzi katika ngazi zote. Vyama vya kisiasa vya upinzani aidha vimesusia au kulazimisha kuondoa ugombea wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini haya yametawaliwa na ghasia za umwagaji damu na mauaji. Huu si chochote ila ni ushindani wa wazi kati ya tabaka tawala kwa ajili ya madaraka na pesa. Swali linazuka ni nini kinawafanya kuwa wakaidi na wenye pupa. Jibu pekee linalokubalika kwa hili ni kushindwa kwa Urasilimali - fungamano lake la kimfumo halifafanui tena uhusiano kati ya watawala na watawaliwa, wala masharti ya ushirika kati ya tabaka tawala. Pazia limepomoka na sura ya ulafi wa Urasilimali inaonekana waziwazi sasa hivi kwamba kila mtu anataka kuhakikisha vipande vyake vya keki. Hii ni kwa sababu chini ya mfumo unaotawala wa kirasilimali wa kisekula siasa hutazamwa kama linda kapu lako la pesa mwenyewe, njia ya kujipatia utajiri. Sasa, tabaka tawala limeacha wajibu wao kwa watu na kujiingiza katika kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya madaraka na pesa. Hii ni dalili tosha kwamba mfumo huu utaporomoka hivi karibuni.

Watawala wamekuwa aina ya tabaka lililojitenga ambalo haliwezi kujiunganisha na mahitaji na hisia za watu. Vyenginevyo, kuna mantiki gani kufanya uchaguzi usio na maana katikati ya 'janga la Covid-19'? Watu wanataka ajira, huduma za afya, kumudu bei za vitu muhimu ndani yao nk. na sio mwenyekiti mpya wa Muungano wa Parishad kutoka kundi lile lile la wanasiasa wafisadi.

Kwa kushindwa kwa Urasilimali, watu wanaegemeza imani yao tena kwa Uislamu kwa sababu Uislamu unatoa mbadala wa kuaminika kwa mfumo mbovu wa utawala uliopo nao ni mfumo wa Khilafah. Katika Uislamu, siasa hutazamwa kuwa ni wajibu adhimu na kila mtu akiwemo Khalifa anawajibika kwa nafasi aliyonayo na kuwajibika duniani na Akhera. Mtume Muhammad (saw) amesema:

«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ الْإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya aliowachunga. Kiongozi ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.” (Sahih Al-Bukhari).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Karim Abu Zayed
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu