Jumanne, 07 Rajab 1446 | 2025/01/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhuru Hauwezekana Chini ya Mfumo wa Kidemokrasia wa Kirasilimali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Jitayarisheni na msubiri wito wangu kwa Islamabad, Imran Khan asema huko Lahore Jalsa “LAHORE: Mwenyekiti wa PTI Imran Khan Alhamisi aliwataka Wapakistani kujitayarisha kuanzisha kampeni ya "uhuru halisi" na kusubiri wito wake kwa Islamabad, huku Waziri Mkuu huyo aliyeng’atuliwa mamlakani akisisitiza hatakubali "serikali iliyoingizwa kutoka nje" kwa gharama yoyote.” (Chanzo: geo.tv)

Maoni:

Ni mfumo huu wa kidemokrasia wa Kirasilimali ndio uliotuweka chini ya pingu za Marekani. Ni demokrasia ndiyo inayotoa njia za kutabikisha sera za dola za kikoloni kupitia sheria za bunge na ni kupitia sheria kama hizo tu sasa uchumi wetu unadhibitiwa na IMF na FATF na sera yetu ya kigeni au kwa maneno taasisi yetu ya utawala iko chini ya CENTCOM na UNO. Elimu yetu inadhibitiwa na USAID na UNESCO, shukrani kwa mfumo huu wa kidemokrasia wa Kirasilimali uliotungwa na mwanadamu ambao unatoa njia kwa dola za kikoloni kupenya.

Na sasa ni dhahiri mchana peupe kuwa sera za IMF zinatufanya tuwe madhalili kila uchao. Na huu ndio mfumo wa kidemokrasia unaohakikisha kwamba tunaendelea kurudisha zaidi ya nusu ya mapato yetu kwa riba na kupanga upya kodi na kuhakikisha tunarudisha mkopo na riba kwa wakati unaofaa kupitia kuwatoza ushuru mbaya watu maskini na kuwaepusha matajiri waovu.

Ni demokrasia ndio iliyomleta rais wa SBP kutoka nje; mfumo huu mbovu ndio uliotufanya tuwasaliti ndugu na dada zetu wa Waislamu huko Kashmir na kumsaidia Modi sio tu kubaki madarakani bali pia kuachilia jeshi lake la wahalifu kufanya maonevu ya kikatili, na huu ndio mfumo wa kidemokrasia unaoruhusu ndege za CENTCOM kuruka kupitia Anga yetu na kutekeleza machafuko ya kihalifu nchini Afghanistan.

Kila serikali chini ya mfumo huu wa kidemokrasia ya kirasilimali itachukua mwelekeo kutoka kwa mabwana zao bila kujali wanasiasa wanasemaje ndani au nje ya korido za madaraka kwa sababu kiuhalisia mfumo huu wa kidemokrasia wa Kirasilimali unaochukuliwa kutoka nje ya nchi hivyo kila kitakachokuja na kuendeshwa chini ya mfumo huu hatimaye kitaagizwa kutoka nje ya nchi. Wakati umewadia sasa tuelewe na tusiwe sehemu ya kauli mbiu zozote kutoka kwa watu ambao ni watetezi wa mfumo huu wa kidemokrasia.

Ni kupitia kuiondoa demokrasia ya Kirasilimali na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume pekee ndio tutakomesha uingiliaji huu wa kikoloni katika mambo yetu. Khilafah pekee ndiyo itamaliza maagizo ya IMF na kukataa riba vyovyote itakavyokuwa. Khilafah ndio itakayokusanya majeshi ili kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Waislamu na kuziunganisha Ardhi za Waislamu chini ya vivuli vya Khilafah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammad Adel

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu