- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Umma Mmoja... Khilafah Moja
Katika kumbukumbu ya mwaka wa 104 H wa kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wageni wa tovuti za Afisi Kuu ya Habari, silsila mpya inayoitwa: “Ummah Mmoja... Khilafah Moja” iliyotolewa na Afisi ya Habari wa Hizb ut Tahrir ya Wilayah Pakistan.
#أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
KIPINDI cha 1
Khilafah ya Kiislamu ina bendera za kipekee, “Liwaa” na “Raya.” Dalili inatokana na dola ya kwanza ya Kiislamu, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliisimamisha. Bendera ya Liwaa ni nyeupe. “La Ilaha illa Allah, Muhammadur RasulAllah ﷺ,” imeandikwa juu yake kwa maandishi meusi. Inafungamanisha na mkuu (Amiri) wa jeshi. Inatumika kama bendera ya kawaida (a’lam) kwa ajili yake peke yake. Dalili ya hayo ni yale yaliyopokewa na Ibn Majah, أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ مَكَّةَ يَوْمَ الْفَتْحَ وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضُ “Mtume ﷺ aliingia Makka siku ya kutekwa kwake. Bendera yake ya Liwaa ilikuwa nyeupe.”
Jumatano, 01 Rajab 1446 H sawia na 01 Januari 2024 M
KIPINDI cha 2
Bendera ya Rayah ni nyeusi. “La Ilaha illa Allah, Muhammad Rasul Allah ﷺ” imeandikwa juu yake kwa maandishi meupe. Inabebwa na makamanda wa kijeshi wa vitengo, bataliani, vikosi, na vitengo vyengine, vya jeshi la Khilafah. Dalili ya hili ni kwamba Mtume ﷺ alipokuwa mkuu wa jeshi huko Khaybar alisema:
«لأُعْطِيَنَّ الرَّايَةَ رَجُلا يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ﷺ ، وَيُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ ﷺ, فَأَعْطَاهَا عَلِيًّا»
“Nitampa bendera ya Raya kesho mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Na akampa Ali (ra).” (Bukhari na Muslim)
Alhamisi, 2 Rajab 1446 H - 2 Januari 2025 M
KIPINDI cha 3
Mtume ﷺ amesema,
« وَإِنَّهُ لاَ نَبِيٌ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فَتَكْثُرُ» قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ، «فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ» “Hakuna Mtume baada yangu. Kutakuwa na Makhalifa wengi.” Maswahaba zake wakasema: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema, “Mpeni bay’ah mmoja tu, kwa wakati mmoja.” [Muslim]. Imam An-Nawawi amesema katika Sharh yake kwamba, “Iwapo Khalifa amepewa bay’ah baada ya Khalifa mwengine kuteuliwa, basi uteuzi wa kwanza ndio sahihi. Ni lazima utimizwe. Wa pili ni batili. Ni haramu kuutimiza. Ni haramu kwake kudai utimizaji huo. Hii ni bila kujali kama Waislamu walijua kuhusu Khalifa wa kwanza au la. Haijalishi kama walikuwa katika nchi moja au tofauti, au mmoja wao alikuwa katika nchi iliyotengwa kabisa na nyingine.”
Ijumaa, 3 Rajab 1446 H - 3 Januari 2025 M