Ijumaa, 18 Safar 1446 | 2024/08/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katiba Hii Mpya Nchini Tunisia ni Ipi?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kura ya maoni ya katiba nchini Tunisia

Maoni:

Kura ya maoni ya katiba imepangwa kufanyika nchini Tunisia mnamo tarehe 25 Julai. Ikipita itakuwa ni katiba ya pili baada ya mapinduzi ya 2011. Ingawa katiba zote mbili ni katiba za kisekula kikamilifu kuna tofauti kati ya hizo mbili. Katiba ya kwanza ambayo ilitumika mwaka 2014 ilitoa mamlaka zaidi kwa bunge, tofauti na katiba mpya inayo rundika madaraka pambizoni mwa Rais. Hii itampa Rais wa Tunisia Kais Saied mamlaka na udhibiti zaidi juu ya Tunisia kuliko hapo awali. Katika kuelekea rasimu ya katiba, Rais tayari ametoa wazo la nini anachokiandama katika katiba mpya. Alinyakua udhibiti kupitia kutumia mamlaka ya dharura, aliwaondoa waziri mkuu, waziri wa ulinzi, kaimu waziri wa sheria, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kituo kikuu cha televisheni cha taifa cha Tunisia, Wataniya, wajumbe wa serikali, kusimamisha bunge kwa siku 30, kinga ya bunge, kuifutilia mbali tume ya katiba na sehemu kubwa ya katiba yenyewe.

Ninapoandika makala haya, niko nchini Tunisia. Kinachoonekana dhahiri katika nchi hii ni kwamba ushawishi wa Ufaransa unaonekana waziwazi na pasi shaka haukuishia na kuondolewa kwa ukoloni Tunisia. Ndio maana Vuguvugu la Waarabu lililoanzia hapa lilikuwa jinamizi kwa Ufaransa kwani iliogopa kupoteza mshiko wake wa muda mrefu nchini Tunisia na fursa kwa nchi zingine za Magharibi kuingia na kutekeleza utawala wao. Hasa tangu mapinduzi, Tunisia imekuwa uwanja wa michezo wa kutawala kwa dola za Kimagharibi, kama vile Ufaransa, Uingereza na Marekani. Ndiyo maana mchochezi halisi kiu ya kutaka kutawala zaidi Tunisia ni zaidi ya Rais Kais Saied na wasaidizi wake. Ni Ufaransa ambayo anashirikiana nayo, ambayo inasukuma katiba hii mpya ili kukaza hatamu zake kama ilivyofanya kwa karne moja na nusu iliyopita.

Msimamo wa vyama vingi vya kisiasa na sehemu kubwa ya wananchi ni kwamba wanapinga dhidi ya hatua hii ya kidikteta kutokana na hofu ya kurudi katika hali ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Kwa hiyo, ili kufanikiwa na kupata kibali cha Waislamu nchini Tunisia walitumia baadhi ya maneno ya “Kiislamu” katika katiba hiyo mpya, kana kwamba Tunisia ni sehemu ya Ummah na kwamba Uislamu utalindwa, lakini ndani ya muundo wa usekula. Kwa hiyo, wanajaribu kuwadanganya na kuwapoteza Waislamu kwa maneno matupu.

Msukumo mkubwa wa kupatikana kwa katiba ya pili pia umekusudiwa kama risala kwa wananchi kwamba mapinduzi yamefikia kikomo na yamehitimishwa kwa katiba hii ya mwisho. Hivyo basi kuwapotoa watu njia ya mabadiliko halisi na kuzielekeza hisia za watu katika kuukubali mfumo wa zamani.

Lakini upande wa nyuma ni kwamba Waislamu wamebakia kuwa na hamu kubwa ya Uislamu. Vyovyote vile mipango ya dola Kimagharibi na vibaraka wao itakavyo kuwa, hawakuweza kubadilisha mapenzi na kujitolea kwa Waislamu kwa ajili ya Uislamu, hata baada ya karne nyingi za ukoloni wa kithaqafa wa Kimagharibi. Ni suala la muda tu kwamba Nuru ya Uislamu itatawala kwa mara nyingine tena, hata kama mabepari kama vile Ufaransa, Uingereza na Marekani wapende au wasipende.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu