Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kisu Kiitwacho IMF

(Imetafsiriwa)

Habari:

Baraza la mawaziri la federali lilikuwa limeidhinisha agizo mnamo Alhamisi la kuuza hisa za makampuni ya mafuta na gesi na mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na serikali kwa Imarati ili kukusanya dolari bilioni 2 hadi bilioni 2.5 ili kuepusha kushindwa kulipwa madeni. Imarati mwezi Mei ilikataa kutoa amana za fedha kutokana na Islamabad kutokuwa na uwezo wa kuregesha mikopo ya awali na badala yake iliomba kufungua makampuni yake kwa uwekezaji. (Tribune Pakistan)

Maoni:

Ukoloni haukwisha; ulibadilisha tu sura yake. Mojawapo ya zana zenye thamani zaidi inayotumiwa kuzuia nchi zinazoendelea kutokana na kupata uhuru wa halisi imekuwa ni madeni. Pakistan ilibuniwa huku ikibeba uchumi dhaifu, ikitarajia kutawaliwa na watawala wacha Mungu na kuendelea jinsi ulimwengu wa Kiislamu ulivyoendelea chini ya utawala wa Kiislamu. Kabla ya kipindi cha ukoloni, Uingereza ilinunua bidhaa kama vile nguo na mchele kutoka kwa wazalishaji wa Kihindi na kuzilipia kwa njia ya kawaida - aghlabu kwa fedha - kama walivyofanya kwa nchi nyingine yoyote. Lakini baada ya Kampuni ya East India kuanzisha ukiritimba juu ya biashara ya Wahindi, uporaji na ufujaji ulianza. Utawala wa miaka 200 wa Waingereza haukusababisha tu upoteaji mkubwa wa nyenzo lakini pia uligeuza kipote cha watawala kuwa viumbe chotara, na wenyeji kuwa vibarua dhaifu.

Makubaliano kati ya wakoloni na watawala vibaraka yalijengwa juu ya msingi wa kulinda maslahi ya kila mmoja.

Imepokewa kutoka kwa Abu Khidash: Amesema Mtume Rehma na amani zimshukie,

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ فِي الْكَلَإِ وَالْمَاءِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika juu ya vitu vitatu: katika malisho, maji na moto.”

Tangu baada ya kuundwa kwake, watawala wa Pakistan wamekuwa wakiuza mali zake za thamani (Mali ya Umma) bila aibu. Hadithi kila mara huanza na deni, hasara, uzembe wa Serikali iliyopita na kuishia kwa kudai muhanga zaidi kutoka kwa watu wake. Mikopo baada ya mikopo na mikopo zaidi ya kujikwamua na mikopo hiyo haijalemaza tu uchumi pekee bali imetia kovu kujithamini kwa watu wake. Sasa watawala hawa wamejiamini sana hata hawataki taratibu rasmi kuwa kikwazo. Tumeona uharibifu wa mali muhimu kama vile PTCL Shirika la Mawasiliano ya Simu la Pakistan. Mnamo mwaka wa 2005 Baada ya kulipakazia shirika lenye faida kubwa kuwa kampuni isiyofaa, isiyo na uwezo, na iliyopitwa na wakati, serikali iliuza hisa 26% (pamoja na udhibiti kamili wa usimamizi) kwa Etisalat yenye makao yake Dubai kwa $2.6 bilioni. Hata hivyo, wakati wa ubinafsishaji wake, PTCL ilikuwa kiteknolojia mojawapo ya wachezaji hodari wa mawasiliano ya simu katika Asia Kusini ikiwa na idadi kadhaa ya teknolojia mpya katika kanda. Kifedha, kampuni hiyo ilikuwa imechapisha mapato ya kila mwaka ya $1.4bilioni na faida halisi ya $452 milioni.

Ndani ya miaka minne thamani ya soko ya kampuni hiyo ilikuwa imeshuka kwa 75%, na kusababisha hasara ya karibu $3bilioni kwa serikali ya Pakistan (mmiliki hisa nyingi). Juu ya hayo, Etisalat leo bado ina deni la serikali zaidi ya $ 800 milioni (kutoka kwa bei ya ununuzi), ambayo inaweza kuwa mara mbili ya thamani ya sasa. Kinaya ni, badala ya kuregesha kiasi hiki, serikali sasa inaomba mikopo kutoka Imarati.

Ubinafsishaji wa sekta ya kawi ya Pakistan umelemaza uchumi mzima. Ubinafsishaji huo uliiingiza Pakistan katika mzunguko mbaya wa madeni. Bei ya nishati imepanda tu, ambapo haishangazi kutokana na wazalishaji wa umeme wa kujitegemea hawana ushindani. Na tukiangalia Benki za Pakistan, zinaonekana kuwa na faida zaidi baada ya kubinafsishwa miaka ya 2000 na hiyo ni kwa sababu faida hii ilitokana na kuikopesha Serikali.

Ikiwa tutaweka mkakati wetu sawa na tu kuacha kuwa kibaraka muhimu wa mtu, tunaweza kuwa mfano kwa ulimwengu wote. Hilo halitaleta tu utulivu wa kiuchumi bali tutaweza kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt). Sera ya kiuchumi ya Kiislamu inatokana na Aqida ya Kiislamu. Sera nyingine yoyote ya kiuchumi ni mbovu, na haiwezi kuleta utulivu kwani itaegemezwa juu ya ‘aql (akili) ya mwanadamu. Hivyo sera ya kiuchumi ya dola ya Kiislamu haitokani na kuongeza pato la taifa, bali inadhamini ugavi wa mali ya dola ya nje na ya ndani kwa kila mtu binafsi katika Ummah ili kila mtu apate kukidhi mahitaji yake ya kimsingi. Raisi wa Dola Khalifah ndiye mlinzi wa mali zake na analazimika kuzigawanya na kutoa kulingana na mahitaji ya maeneo ya Waislamu.

Khawlah al-Ansariyah (ra) amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ فِي مَالِ اللَّهِ بِغَيْرِ حَقٍّ فَلَهُمْ النَّارُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

“Watu wanaomiliki mali ya Mwenyezi Mungu (kama vile mali ya hazina ya dola ya Waislamu, Zaka nk.) pasi na haki watakuwa Motoni Siku ya Kiyama.” [Imepokewa na Al-Bukhari].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu