Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Waislamu wa Asia ya Kati Wanataka Mabadiliko

Lakini ni Kipi Kinachohitajika Kubadilishwa!?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Julai 4, Shirika la Habari la Fergana, likinukuu Afisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu na Huduma ya Usalama ya Serikali, liliripoti: “Mnamo Julai 1-2, maandamano makubwa yalifanyika kupinga kuanzishwa kwa marekebisho ya Katiba ambayo yangeinyima jamhuri hadhi yake ya kisheria. Kulingana na wachunguzi, mnamo Julai 1 saa 14:50, mwanablogu na mhariri wa gazeti la "In the Service of the People" Dauletmurat Tazhimuratov alituma video ya ombi kupitia chaneli ya Telegraph ya Makan.uz akiitisha mkutano mbele ya jengo la bunge kwa ajili ya uhuru wa Jamhuri ya Karakalpakstan.

Kufikia saa 15:30, Tazhimuratov alipelekwa hadi idara ya polisi ya Nukus kwa kutoa wito kwa raia kuandaa mkutano haramu kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kujua juu ya kuzuiliwa kwa mwanablogu huyo, kikundi cha wafuasi wake kilikwenda kwa idara ya jiji ya mambo ya ndani wakitaka kuachiliwa huru kwa Tazhimuratov. Wakiwa njiani kuelekea soko kuu la wakulima, walifanya ghasia. Tazhimuratov aliachiliwa huru, lakini ghasia hazikusimama, sasa zikafanyika kwa ushiriki wa mwanablogi huyo".

Maoni:

2022 umekuwa mwaka wa misukosuko kwa Waislamu wa Asia ya Kati. Machafuko hayo maarufu yalitokea nchini Kazakhstan, Tajikistan, na Karakalpakstan, Uzbekistan. Kila mara wananchi wanapopinga dhulma ya tawala na kutaka kubadili maisha yao mabaya, watawala kwa kauli moja wanatuhumu “nguvu kutoka nje” kuandaa machafuko nchini, kutangaza hali ya hatari na kuwapiga risasi raia wao.

Mwanzoni mwa Januari, watu nchini Kazakhstan, huku wakitoridhika na sera ya mamlaka, walifanya maandamano makubwa. Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev aliwataka raia kutokubali wito wa "watu waharibifu". “Tulilazimika kukabiliana na majambazi wenye silaha, waliopata mafunzo, kutoka ndani pamoja na nje ya nchi. Ilikuwa ni majambazi na magaidi," Tokayev alisisitiza. Almaty pekee, kwa mujibu wa rais, ilishambuliwa na watu 20,000 wenye itikadi kali. KZh Tokayev aliongeza kuwa kinachojulikana kama vyombo vya habari huria na takwimu za kigeni zimecheza dori ya uchochezi nchini. Maandamano hayo yalizimwa kikatili na jeshi na polisi.

Katikati ya Mei, Waislamu wa eneo la milimani la Tajikistan hawakuwa na wakati wa kuandamana dhidi ya utawala dhalimu wa mamlaka, kwani walizingirwa na kuanza kupigwa risasi. Baada ya mamlaka kuripoti kwa mafanikio juu ya kushindwa kwa magenge ya kigaidi. Taarifa ya mamlaka inasomeka hivi: "Makundi ya wahalifu yaliyopangwa ya Jimbo lenye utawala uhuru la Gorno-Badakhshan, chini ya uongozi na ufadhili wa mashirika ya kimataifa yenye msimamo mkali na ya kigaidi, ili kukiuka usalama wa serikali, kudhoofisha misingi ya utaratibu wa kikatiba, kuzuia shughuli za vyombo vya kutekeleza sheria, kuwatisha watu, yalishambulia msafara wa magari ya kitengo maalum cha kupambana na ugaidi cha Jamhuri ya Tajikistan". Maandamano haya pia yalizimwa kikatili na jeshi na polisi.

Mwanzoni mwa Julai, vyombo vya habari vilitangaza habari za maandamano makubwa huko Karakalpakstan, Uzbekistan. Mrija wa mwisho ndani ya kikombe cha subira ya watu, utawala dhalimu wa madaraka, ulikuwa ni marekebisho mapya ya katiba, ambayo yanahusiana na hadhi ya jamhuri. Swali lilihusu sehemu inayosema kwamba katika katiba ya sasa ya nchi, watu wanaweza kupata ubwana na kujitenga na Uzbekistan kwa kupiga kura, na katika marekebisho hayo mapya, wanataka kuondoa uwezekano huu.

Mara tu watu walipoingia mabarabarani, mamlaka ziliwaacha wanajeshi kuwapiga risasi na kuwatawanya watu wasioridhika. Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev alisema: "Kwa kweli, matukio haya hayakupangwa kwa siku moja au siku 10. Vitendo hivi vimetayarishwa kwa miaka mingi na nguvu ovu za nje." Maandamano haya pia yalizimwa kikatili na jeshi na polisi.

Kama tunavyoona, katika visa vyote vya kutoridhika kwa watu na utawala dhalimu wa mamlaka, muundo kama huu unaweza kufuatiliwa - viongozi wanamlaumu adui dhaniwa wa nje, hawatambui na hawasemi kwamba watu wamechoka na uhalifu. mateso na kutojali sheria kwa wale walio madarakani. Wananchi wanataka kujiuzulu kwa mamlaka na kwamba maisha yabadilike kuwa bora.

Watu wanatojitolea muhanga, hata kwa gharama ya maisha yao, lakini hakuna kinachobadilika. Utawala wa kihalifu ungalipo, uhalisia mbaya haubadilika, na maisha yanakuwa hata magumu zaidi.

Ndiyo, watu wamechoshwa na uhalifu wa madhalimu na wanataka mabadiliko. Lakini haitoshi kutaka tu mabadiliko. Kwanza, munahitaji kuamua misingi ambayo kwayo mabadiliko yatafanywa!? Ikiwa mabadiliko hayo yanatokana na Katiba iliyobuniwa na mwanadamu, hali ikoje leo na kama Rais wa Uzbekistan Sh. Mirziyoyev anavyosema: "Watu ndio chanzo na mwandishi pekee wa Katiba." Yaani mwanadamu ndiye mtunzi wa sheria, basi huu ndio msingi wa kidemokrasia - kisekula. Kwa msingi huu, kulingana na kanuni ya kutenganisha dini na maisha, mtu ndiye mtunga sheria - karibu nchi zote za dunia zinaishi.

Msingi huu ni kutenganisha dini na maisha, ambapo Muumba wa vitu vyote Mwenyezi Mungu alifutwa kutoka kwa maisha, na mwanadamu mwenyewe ndiye hujitengenezea sheria kwa ajili yake mwenyewe. Msingi huu umekuwa ndio tatizo kuu la wanadamu. Mwanadamu, anaendelea kwa mujibu wa hawaa zake, kufuta sheria za zamani na kutoa sheria mpya.

Mfano wa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba ya Uzbekistan unaonyesha kuwa zaidi ya mabadiliko 200 yanatarajiwa kufanywa kwa vifungu 64 vya Sheria hii Msingi, pamoja na kujumuishwa kwa vifungu vipya. Mwanadamu, kwa akili yake finyo, anajaribu kujitengenezea mfumo wa maisha kwa ajili yake mwenyewe, akijitia katika mateso ya mara kwa mara na misukosuko, na kila wakati inazidi kuwa mbaya zaidi. Na hii hutumiwa na madhalimu na bwana wao, kubadilisha na kurekebisha sheria kwa ajili yao wenyewe.

Enyi watu wa Asia ya Kati! Sisi ni Waislamu na msingi wetu unatokana na Uislamu. Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu, na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mtungaji sheria wetu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Kitabu Chake Kitukufu:

(إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ)  “Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu” [12:40]

(وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu” [5:49].

Na aya nyingine nyingi za Qur’an Tukufu zinazobainisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kutunga Sheria, na Qur’an na Sunnah pekee ndizo chanzo cha katiba.

Waislamu! Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha tuteremshia rehema yake - Uislamu! Uislamu ni mfumo kamili wa maisha kwa jamii na serikali. Uislamu ndio msingi ambao kwao lazima tufanye mabadiliko. Hapo tu ndipo tutakapopata mafanikio na ustawi.

Hizb ut Tahrir, kwa msingi wa Quran na Sunnah, imetayarisha rasimu ya Katiba na mpango kwa ajili ya Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Harakisheni mujiunge na Hizb ut Tahrir juu ya kazi ya kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu ndani ya dola ongofu ya pili ya Khilafah kwa njia ya Utume. Tamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu