Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Turkestan Mashariki ni Jeraha la Umma Linalovuja Damu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo siku ya Ijumaa Septemba 16, baada ya Swala ya Ijumaa katika Misikiti ya Hajibayram jijini Ankara na Fatih jijini Istanbul, mauaji ya kinyama yaliofanywa na Makafiri wa Kichina kwa Waislamu wa Uighur huko Turkestan Mashariki ulipingwa vikali kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Koklu Degisim pamoja na ushiriki mkubwa wa Waislamu. (Jarida la Koklu Degisim, Haksöz Haber, Gazeti la Akit)

Maoni:

Virusi vya Korona, vilivyoanzia China na kutishia dunia nzima na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, vinadaiwa kushika kasi katika Turkestan Mashariki hivi karibuni, na watu wa Uighur wamefungwa majumbani mwao chini ya kauli mbiu "Zero Covid".

Waislamu wa Uighur ambao hawaruhusiwi kutoka nje ya nyumba zao, milango ya nyumba imechomelewa ili wasitoke nje ya nyumba zao, na watu wa Uighur ambao hawawezi kupata bidhaa za chakula kwa sababu hawawezi kutoka nje ya nyumba wanahukumiwa kifungo cha njaa nyuma ya milango waliofungiwa na kuachwa kufa.

Turkestan Mashariki, ambayo imekuwa chini ya kukaliwa kimabavu na Wachina tangu 1949, imekaribia kugeuka kuwa kuzimu kwa miaka 6 hadi 7 iliyopita. Chini ya jina la mageuzi ya kifikra na utakaso wa kiitikadi, mamilioni ya Waislamu wa Uighur wametupwa katika kambi za mateso na magereza. Chini ya jina la 'mradi wa familia ya ndugu', wanaume wa Kichina waliwekwa kama wapangaji ndani ya nyumba waliomo wake, kina mama na mabinti wa Waislamu wa Uighur waliofungwa jela, na heshima na usafi wao kukiukwa. Serikali ya Kikafiri ya China inajaribu kuwaangamiza Waislamu wa Uighur kwa kuwaua na kuwahusisha na mauaji ya halaiki, mateso na ukatili ambayo imetekeleza.

Vilio vya Waislamu wa Uighur wa vinapaa hadi mbinguni, lakini watawala na wafalme wa Umma wa Kiislamu wanaokaa kwenye kasri wamekuwa viziwi kwa vilio hivi, ingawa wanavisikia, wamependelea kuvipuuza.

Wamewapuuza kwa urahisi Waislamu wa Uighur ili mahusiano yao na biashara na China ya kikafiri isiweze kuzorota. Biashara yao imekuja kabla ya dhamiri zao, ubinadamu na imani yao, na uhai, damu na heshima ya Waislamu wa Uighur vimetolewa mhanga kwa sera ya halisi iliyoegemezwa juu ya maslahi. Majeshi ambayo yanaweza kuhamasishwa kwa ajili ya maslahi ya kafiri mkoloni Amerika, Ulaya na NATO yamekwama kwenye kambi zao inapokuja kuhusu kuwasaidia Waislamu.

Cha kusikitisha ni kwamba, huku Turkestan Mashariki ikiomboleza, watawala wa nchi za Kiislamu walikuwa wakishughulika kusalimiana na mikono michafu ya viongozi wa Kikafiri wa China, Urusi na India katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai nchini Uzbekistan mnamo tarehe 16 Septemba.

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie.

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللَّهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» ‏

“Muislamu ni ndugu yake Muislamu. Hamdhulumu, wala hamsalimishi. Mwenye kumtimizia ndugu yake haja zake, Mwenyezi Mungu humtimizia haja zake. Mwenye kumuepusha Muislamu na dhiki, Mwenyezi Mungu Atamuondolea dhiki Siku ya Kiyama. Atakayemsitiri Muislamu aibu zake, Mwenyezi Mungu naye atamsitiri aibu zake Siku ya Kiyama.”

 Kinachoumiza na kusikitisha zaidi kuliko ukweli kwamba watawala wa nchi za Kiislamu wanawatelekeza Waislamu wa Uighur kwa mateso ya kafiri China ni kwamba wanachuoni wengi wa Kiislamu, wanatheolojia, walimu au viongozi wa maoni wanafanya kazi pamoja na watawala wao na serikali juu ya kadhia hii, hawabebi uongozi sahihi, hawawanasihi watawala wao.

(إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ)

 “Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni...” [Surah Al-Fatır 28]. Aya hii inawausia wanachuoni wasimwogope yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu na wamtii Mwenyezi Mungu, waichukulie haki kuwa juu katika dhurufu na hali zote. Pia kuna mwamko unaoonyesha kwamba yule aliyeuawa kwa sababu ya kusema ukweli dhidi ya sultan jeuri ni jirani ya Hamza (ra).

Maandamano yaliyofanywa na Koklu Degisim na neema iliyodhihirishwa na Waislamu kwa hamasa nyingi, yalionyesha kwamba Ummah unahitaji umoja na nguvu.

Hizb ut Tahrir, sauti ya Waislamu wa Uighur, ambayo hainyamazi kimya kuhusu mateso yoyote yanayoupata Umma wa Kiislamu, inawalinda Waislamu wa Uighur mbele ya ukatili unaofanywa na Kafiri China huko Turkestan Mashariki na haiwaachi peke yao ilhali bila shaka ndiyo yenye sifa na inastahili uongozi huu.

Suluhisho moja na la pekee ambalo Hizb ut Tahrir inazingatia ni kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itazitisha, itazizuia au, ikibidi, kupigana na dola za Kikoloni za Kikafiri za Amerika, Ulaya, China, Urusi, India, Israel na dola nyenginezo zote zinazowatesa Waislamu kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu.

Mtume (saw) amesema:

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma na hujilinda kwayo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi ÖZER

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu