Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nchi Kubwa Zaidi ya Kidemokrasia Duniani Yawakandamiza Wanawake wa Kiislamu ili "Kuwakomboa"!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Marufuku ya Hijab katika mji wa India wa New Delhi ilitolewa na serikali ya Karnataka mnamo tarehe 22 Februari 2022. Ilipitishwa na baadaye kupasishwa na Mahakama Kuu nchini India na wachambuzi wamekuja kuelewa matokeo yake mapana ya kijamii katika jumuiya za wanafunzi. Utafiti uliochapishwa na chama cha People's Union for Civil Liberties (PUCL) ulisema: "Hili linaweza kusababisha elimu ya vichochoroni kwa kuwa marufuku hiyo imewalazimu baadhi ya wanafunzi wanaovaa hijab kutafuta uhamisho kwenda kwenye taasisi zinazosimamiwa na Waislamu, na hivyo kupunguza maingiliano yao na wanafunzi wa jamii zengine”.

Maoni:

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha athari kubwa zaidi za kisaikolojia ambazo sheria hizi zimekuwa nazo kwa wanawake wachanga wa Kiislamu. Imesababisha hisia kubwa ya kutengwa na huzuni kati ya wanafunzi hawa, ambao wamewekwa katika hali mbaya na sheria hizi za kibaguzi.

Uhalisia wa kusikitisha wa kina dada hao ni kwamba mustakabali na maisha yao yako mikononi mwa mamlaka isiyowaheshimu na hutumia fikra ghushi za ukombozi wa wanawake kutetea ukiukaji wao wa haki za binadamu.

Mahakama Kuu ya Karnataka ilikuwa imetangaza kwamba “kuvaa hijab kwa wanawake wa Kiislamu sio sehemu ya amali msingi za kidini katika imani ya Kiislamu na hakulindwi chini ya haki ya uhuru wa dini unaodhaminiwa chini ya Kifungu cha 25 cha Katiba ya India.

Wakati wa kusikilizwa kwa rufaa za kupinga marufuku ya hijab katika Mahakama ya Upeo mapema mwezi huu madai ya kipuuzi yalitolewa kwamba; "Haki ya kuvaa pia itajumuisha "haki ya kuvua."

Ripoti ya PUCL ilisema kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa umewanyima wanawake haki yao ya kuvaa hijab kama jambo la hijab hiari na kitendo chao wenyewe.

Hukmu za kidhalimu zinazoelekeza kwa wanawake kile wanachoweza kuvaa zinaonyesha unafiki mkubwa katika simulizi ya kiliberali ya kidemokrasia ambayo inataka kuwakomboa wanawake wa Iran kutokana na maamuzi kama hayo ya mavazi, lakini inatumia adhabu zilezile kwa wanawake wa Kiislamu wanaochagua Hijab.

Mitazamo ya kidemokrasia ya kiliberali ingeshutumu marufuku ya serikali kibaraka ya kikoloni ya Afghanistan dhidi ya wanawake katika elimu ili kuchafua sura ya Sharia, lakini kufanya vivyo hivyo kusherehekea maadili ya Magharibi.

Nchini India ni muhimu kutambua kwamba umuhimu kwa wanawake wengi, bila kujali dini zao, wanapenda kufinika vichwa vyao kwa sababu inawafanya wajisikie salama au wana uhusiano wa kitamaduni na kitendo hicho. Hawaguswi na utekelezwaji wa marufuku hiyo, ambayo inaonyesha wazi kwamba Uislamu ndilo jambo linaloshambuliwa haswa. Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir pia imetoa habari na maoni ya hapo awali kuhusu ubaguzi wa mahali pa kazi kwa wanawake wa Kiislamu nchini India, huo ndio ukombozi wa kirongo wa wanawake chini ya sheria za kisekula. Njia pekee ambayo wanawake wa Kiislamu wanaweza kutimiza uwezo wao kamili ni chini ya utawala wa Khilafah ambao utasimamia mahitaji yote ya wanawake kama raia wa Dola hii, bila ya ubaguzi.

Elimu ya wanawake inathaminiwa katika Uislamu na mgongano wa kuwanyimwa elimu wanawake wa Kiislamu hautakuwa ni suala tena kwa kuwepo Sharia ya dhati.

(يُؤتِى الْحِكْمَةَ مَنْ يَشاءُ وَمَنْ يُؤتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ اُوتِىَ خَيْراً كَثِيراً وَمَا يَذَّكَّرُ اِلَّا اُولُوا الاَلْبَابِ)

“Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili.” [Al-Baqara: 269]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu