Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 “Uislamu ni Dini ya Nguvu ya Elimu na Tabia Njema”

(Imetafsiriwa)

Habari:

Tumekuwa tukichapisha msururu kwenye TechTank unaoitwa, “Washindi na washindwa katika kutimiza matarajio ya kitaifa ya ujasusi bandia.” Utafiti umetathmini nchi 44 kuhusu jinsi kila nchi ilivyojiweka nafasi nzuri kufikia malengo yake ya kitaifa ya AI. Katika machapisho yaliyofuata, kila nchi iliorodheshwa katika sehemu ndogo mbili za mipango yao ya utekelezaji: watu na teknolojia Katika chapisho hili la mwisho katika msururu huu, tunaimarisha umakini wetu kwa Marekani na kile inachohitaji kufanya ili kupata utawala katika soko la dunia katika mkakati wake wa kitaifa wa AI. (Brookings.edu)

Maoni:

Kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia (WWI), Ulaya ilikuwa ndio kiongozi katika sayansi na teknolojia. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia (WWII), ilikuwa ni Marekani hadi China ilipoingia kwenye uwanja wa maendeleo ya sayansi na teknolojia na siku hizi, aghlabu tunaona uhasimu na ushindani kati ya Marekani na China katika maendeleo ya kijeshi, kiuchumi na teknolojia. Kwa takriban karne moja, ni vigumu kupata maandishi yoyote ya maandishi yanayosema ulikuwa ni Uislamu kupitia kuutabikisha ambapo Waislamu ndio walioweka msingi wa sayansi na teknolojia.

Hali yetu ilikuwaje tulipotawaliwa na Uislamu, jeshi na uchumi wenye nguvu, kwa karne nyingi tukawa hadhara kubwa katika historia ya wanadamu iliyopanuka kwa karne nyingi. Mipaka yetu ilifika China upande wa mashariki na Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi na kusini mwa Ufaransa Kaskazini na misitu ya Afrika upande wa Kusini.

Katika uwanja wa elimu, Abu al Baraka al Baghdadi aligundua sheria za mwendo karne 5 kabla ya Newton. Vitabu vyake vilipatikana katika maktaba za Ulaya na vilitafsiriwa kwa Kiingereza na Kifaransa wakati wa Newton. Ibn Sina aligundua mdudu minyoo anyesababisha kichocho na homa ya uti wa mgongo. Al Biruni ndiye aliyegundua nguvu ya mvuto wa ardhi (gravity) kabla ya Newton! Kwani alikuwa ndiye mwanachuoni wa karne ya 3 aliyesema “Kitu huanguka chini kwa sababu ya nguvu ya uvutano iliyokusanyika ndani yake”. Lakini nchi za Magharibi ni wezi kwani wanaiba elimu kutoka kwa mataifa mengine na kujihusisha nayo wao.

Al-Biruni ndiye aliyefafanua kupatwa kwa jua na mwezi, yeye ndiye aliyeweka msingi wa kupima ardhi katika hemispheres. Alieleza kwamba dunia ni duara kimaumbile na kuamua latitudo na longitudo ya dunia. Pia alisema kuwa kasi ya mwangaza ni kasi zaidi kuliko kasi ya sauti na alielezea kasi ya mzunguko wa dunia. Watu hawa wote walikuweko karne nyingi kabla ya Newton lakini kama ilivyotajwa hapo awali Magharibi ni wezi, dunia iliona mchana peupe jinsi nchi za Magharibi zinavyoiba rasilimali kutoka Iraq, Afghanistan na Somalia pindi zilipozivamiwa; wamekuwa wakiiba mafuta yetu kutoka kwa maeneo ya mafuta ya Waislamu tangu zamani.

Nani aliyekuwa wa kwanza kugundua pendulum ya saa? Al Yonus Al Masri lakini Magharibi inahusisha ugunduzi huo na Galileo katika karne ya 17. Abu Bakar Al Razi ndiye aliyevumbua nyuzi za upasuaji zinazoyeyuka na kufanya utumizi wa nyuzi hizi katika upasuaji wa ndani kuwezekana. Al Khwarizmi aligundua algoriti zilizofungua njia ya kuvumbuliwa tarakilishi/vipakatalishi, maarifa ya programu na simu za iPhone, nk. Katika mchakato huo, usimsahau Ibn e Haytham, ambaye aliweka nadharia ya kuakisi na kujibu swali muhimu zaidi kuhusu optics yaani "vipi tunaona?" Al Jazari alivumbua bomba la maji kuvuta maji kimakaniki ambayo huongeza kilimo ndani ya ardhi nyingi za Khilafah na pia aligundua nadharia kwamba mwendo wa duara unaweza kuzalisha kawi.

Hebu tusikilize wanachosema wanahistoria wa mataifa mengine, bila shaka ni wachache kiasili, mwanahistoria wa kifaransa Debar alisema “Sisi Wazungu tuna deni kwa Waarabu katika kupata starehe katika maisha yetu ya kila siku, Waislamu ndio waliotufunza usafi wa miili yetu,” alisema zaidi Waislamu walikuwa kinyume na Wazungu ambao hawakubadilisha nguo zao isipokuwa pale wanapoanza kutoa harufu, pia alisema maktaba ya Qurtaba (Qordoba) ilikuwa na vitabu 400,000. Qurtaba ilikuwa na hospitali 50 miaka 700 kabla ya Paris hata kujua hospitali moja. Waislamu ndio waligundua mipako ya sukari kwa ajili ya dawa chungu ili mgonjwa aifurahie, Waislamu ndio waliokuwa wakitwahirisha vifaa vya upasuaji kabla ya upasuaji.

Ndio tulikuwa ni watu ambao hata hatujui kusoma wala kuandika, basi ni nini kilitufanya kuwa Ummah wa madhubuti katika kila nyanja ya maisha ambayo dunia imewahi kushuhudia kwa muda mfupi kutokana na hamu ya elimu ya tiba kuanzia usanifu hadi kilimo kuanzia kwa uchumi hadi kwa jeshi, ni jambo gani jipya lililotubadilisha, kutung’arisha, kutuangaza, hakuna chochote isipokuwa ni Uislamu! Uislamu ni Dini ya elimu, Dini ya nguvu, Dini ya tabia njema, Dini ya hadhara kamili. Yote yameondolewa kutoka kwetu tulipopoteza ngao yetu; yaani Khilafah kwani Uislamu haukujulikana tena baada ya Khilafah kuvunjwa na sasa tuko katika hali mateso, maangamivu usiyo na huruma, kuporwa, kudhalilishwa mikononi mwa Makafiri kote duniani, na njia pekee ya Uislamu kujulikana tena ni kwa kuutabikisha kupitia Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammad Adel

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu