Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wanaume wetu Waislamu Wanafedheheka bila ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 17 Oktoba 2022, BBC iliripoti juu ya kugunduliwa kwa wahamiaji 92 waliokuwa hawana nguo wengi wao kutoka Syria na Afghanistan, ambao wengi wao walikuwa na majeraha. Walipatikana kwenye mpaka kati ya Uturuki na Ugiriki na polisi wa Ugiriki. Zilisajiliwa na Shirika la Walinzi wa Mipakani na Pwani la Muungano wa Ulaya, Frontex, ambao wanachunguza jambo hilo. Wanaume hao wanadhaniwa kuvuka mto Evros wakiwa na boti za mpira.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi lilitoa wito uchunguzi ufanyike na kusema kuwa "limesikitishwa sana na ripoti na picha hizo za kushtua".

Maoni:

Heshima na hadhi ya waumini ni jambo tukufu. Kitambulisho cha wanaume kama viongozi na walinzi wa Ummah wa Muhammad (saw) kiko wazo ndani ya Qur’an.

(الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء بِمَا فَضَّلَ اللّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُواْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللّهُ وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا)

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.” [4:34].

Unyanyasaji huu wa nafasi ya uanaume ni ukiukaji kamili wa vifungu vya Sharia na hatuwezi hata kukubali mtu mmoja (Muislamu au la) kutendewa namna hii. Hata wafungwa wa kivita wana haki za binadamu za chakula, mavazi na malazi. Vitendo hivi vya kinyama katika ule unaoitwa ulimwengu wa "kisasa" vinaakisi thaqafa duni na mbovu ya urasilimali na maadili ya kiliberali ambapo mataifa yananyanyasa mataifa mengine kwa faida ya kibinafsi.

Maafisa wa Uturuki wanailaumu Ugiriki kwa ukiukaji wa haki za binadamu na Ugiriki ilirusha lawama mlangoni mwa Uturuki. Waziri wa ulinzi wa raia wa Ugiriki, Takis Theodorikakos, aliituhumu Uturuki kwa "kutumia uhamiaji haramu" na amenukuliwa akisema "tabia" yake ni "aibu kwa hadhara".

Msaidizi mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan, Fahrettin Altun aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, "Mashini ya Ugiriki ya habari za uwongo imerudi kazini." "Mechi hii ya tenisi" ya maneno inageuza tu aibu na mateso ya mwanadamu kuwa mchezo unaoongeza chumvi kwenye jeraha kwa waliokandamizwa.

Erdogan alitumia hotuba ya Umoja wa Mataifa kuituhumu Ugiriki kwa kubadilisha Bahari ya Aegean kuwa "makaburi" na kusema ina "sera za ukandamizaji" kwa uhamiaji. Hata hivyo ukweli kwamba Uturuki ilitia saini makubaliano yake na Umoja wa Ulaya mwaka 2016 na kuchukua mabilioni ya dolari kama malipo kwa polisi kwenye mpaka wa Syria ni kitendo cha unafiki mkubwa.

Ugiriki imeitaka Uturuki kuheshimu mkataba wa 2016 na Umoja wa Ulaya hivyo ni wazi jinsi watawala wetu wanavyodhibitiwa na wachezaji wa nje. Hivi karibuni Athens itapanua uzio wa maili 25 (kilomita 40) kwenye mpaka wake wa kaskazini na Uturuki ili kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo, kwa hivyo tunaweza tu kutarajia idadi kubwa zaidi ya Waislamu wanaotapa tapa kuwa chini ya muamala huu wa kishetani wa kinyama.

Mamia kwa maelfu wanaokimbia vita, wakiwemo watoto wamezuiwa kuingia Uturuki huku wakipokea maagizo kutoka kwa mamlaka za kikafiri. Maafisa wa udhibiti wa Mipaka wa Uturuki kwa hakika waliwafyatulia risasi wahamiaji wanaojaribu kufikia usalama, kwa hivyo unyama na ukatili wa utaifa ni jambo ambalo viongozi wetu wa Waislamu wanajitwika ingawa ni haramu katika Sharia.

Ni wazi kuwa fedheha na udhalilishaji wa Waislamu umepangwa kwa ushirikiano wa watawala wa Waislamu duniani na hili ni jambo ambalo ni lazima lihesabiwe iwapo Ummah wetu utaweza kujiepusha na hofu ya ukandamizaji yaani maisha bila ya Khalifah wa Uislamu anaotekeleza sheria za haki za Quran na Sunnah ndani ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu