Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uchaguzi Mkuu wa 15 - Je, Kutakuwa na Mabadiliko Yoyote?

Habari:

Mnamo tarehe 10 Oktoba 2022, Waziri Mkuu wa Malaysia alitangaza kulivunja Bunge la 14 ili kutoa nafasi kwa Uchaguzi Mkuu wa 15. Tangazo hili linahitimisha uvumi na makisio ambayo yalikuwa yamekua makali zaidi tangu Septemba. Mfalme, Sultan Abdullah Ri’yatuddin Al-Mustafa Billh Shah alitoa ridhaa ya kuvunjwa kwa Bunge wakati wa hadhara kwenye Kasri la Kitaifa mnamo tarehe 9 Oktoba. Kuvunjwa huku kunaonyesha kwamba uchaguzi mkuu lazima ufanyike ndani ya siku 60. Siku ya uchaguzi hatimaye ilitangazwa kuwa tarehe 19 Novemba 2022.

Maoni:

Hatimaye, tarehe iliyosubiriwa kwa muda mrefu imetangazwa. Wananchi wa Malaysia watajitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 15 (GE15) mnamo tarehe 19 Novemba 2022. Tangu kutangazwa kwa tarehe ya GE15, vyombo vya habari vya kawaida vimekuwa na shughuli nyingi katika kutekeleza majukumu yao ya kusherehekea GE15 kwa kupeperusha maonyesho mbalimbali na kutoa majukwaa kwa kuchambua na kujadili maoni kuhusu uchaguzi na mwelekeo wa kisiasa wa nchi. Shughuli hizi zote zinafanywa kama juhudi za kujenga na kupasha joto anga huku kuwashawishi watu wapige kura ili kuhakikisha mafanikio ya GE15 ijayo.

Wapo wale wanaotarajia kuwa GE ya 15 ni fursa kwa watu wa Malaysia kuregesha utulivu wa kisiasa na uchumi wa kitaifa pamoja na kuwaunganisha Waislamu. Hata hivyo, hata kabla ya GE15, tayari tunashuhudia mgawanyiko mkubwa zaidi katika historia miongoni mwa Waislamu nchini Malaysia. Mgawanyiko huu unadhihirishwa na ukweli kwamba vyama kadhaa vipya vya kisiasa vya Waislamu wa Malaysia vilianzishwa kabla ya uchaguzi. Zaidi ya hayo, vyama hivi vitashindana wenyewe kwa wenyewe au kuungana kwa pamoja kwa msingi wa baadhi ya manufaa. Wengine wanaweza kuhoji kwamba mgawanyiko huo unatokana na baadhi ya kanuni za kimsingi na kwa ajili ya kutafuta haki, hata hivyo bado inadhihirisha mfarakano wa wazi baina ya Waislamu. Kwa hivyo, Waislamu wataendelea kuzozana wao kwa wao, jamii itabaki imegawanyika na matarajio ya kupata utulivu wa kisiasa yatabaki kuwa ndoto tu.

Hivi ndivyo makafiri wa Magharibi wanavyotamani - kwamba Waislamu waendelee kugawanyika na kubaki wametengana, wawe wanyonge na wadanganyike kwa urahisi. Hii inafanyika mbele ya macho yetu. Waislamu sio tu kwamba tumegawanyika kiulimwengu, hata ndani ya nchi moja, hatuna umoja. Uislamu unawajibisha watu wake kuungana sio tu katika masuala ya kiimani, kiroho na kiakhlaqi, bali pia katika siasa. Hili linaweza kufikiwa tu pale Waislamu wote watakaporudi kuufanya Uislamu kuwa ndio msingi pekee katika maisha yao. Hata hivyo, Uislamu unapokuwa sio msingi tena wa maisha, matamanio ya mwanadamu yatachukua mahali pa Uislamu. Matamanio ya mwanadamu yanapochukua nafasi ya Uislamu katika maisha na siasa, pindi vyombo vya kidemokrasia vinapochukua nafasi ya Khilafah ya Kiislamu na Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, kama Dini, endapo haitabikishwi tena kwa ukamilifu wake, tunaweza tu kutarajia uvunjaji sheria, makosa na uharibifu ndani ya jamii. Katika uchaguzi mkuu uliopita, wanasiasa walikutana kwa ajili ya manufaa ili kuendeleza ajenda zao za kisiasa. Leo katika kuelekea GE15, tunashuhudia matukio yale yale. Huenda kukawa na wachache ambao ni wanyofu na waaminifu katika kuwatumikia watu, lakini watu hawa ni nadra. Na katika mfumo wa kidemokrasia, unyoofu na uaminifu wao humezwa kwa urahisi na mafuriko ya ufisadi na ubaguzi. Kwa hivyo, je GE15 itaweza kweli kuleta mabadiliko ambayo umma wa Malaysia unatarajia? Kuna shaka kubwa sana.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu