Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Rishi Sunak – Waziri Mkuu Mwanabenki

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kazi ya kwanza ya Rishi Sunak ilikuwa katika benki ya uwekezaji ya Marekani Goldman Sachs. Aliendelea kwa miaka 14 katika sekta hiyo kabla ya kuwa mbunge. Kwa njia nyingi, uteuzi wake ambao si wa kuchaguliwa unaashiria hatua kuu ya utawala mkubwa wa fedha wa mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa Uingereza - upenyezaji wa kimya kimya wa Westminster na Whitehall umekuwa ukifanyika kwa miongo kadhaa na bila kutambuliwa.

Hii ilikuwa kwa sababu wengi wa wahusika wakuu katika mabaraza ya mawaziri ya chama cha Conservative wa miaka ya 1980 walitoka katika sekta ya fedha. Norman Lamont alitumia miaka mingi katika benki ya uwekezaji ya NM Rothschild and Sons. Cecil Parkinson, ambaye alianzisha "Big Bang" ambayo ilifungua njia ya upanuzi mkubwa wa Soko la Hisa la London katika miaka ya 1980, alikuwa mhasibu aliyeajiriwa katika Square Mile. Na Nigel Lawson alianza ujuzi wake kama mwandishi wa habari za kifedha katika magazeti ya Sunday Telegraph na Financial Times. Kila mmoja amezungumza juu ya taaluma zao za Jiji kama ushawishi mkubwa zaidi kwenye fikra zao kuliko wanauchumi wowote wa kitaaluma. Mawaziri wengine wengi wa chama cha Conservative pia walitoka katika taaluma ya fedha hadi ima kwa Hazina au Wizara ya Biashara na Viwanda.

Hii ilikuwa ndio sababu kuu kwa nini viwanda vingi vilivyotaifishwa havikuuzwa kwa sekta binafsi tu bali vilinadiwa kwenye Soko la Hisa la London na kuhamishiwa mikononi mwa wawekezaji wa Jiji. Pia inaelezea ni kwa nini msururu wa mabadiliko ya kodi na kanuni za fedha zilipendelea fedha kubwa kuliko utengenezaji, na mabadiliko ya usimamizi wa mashirika yalipendelea "thamani ya mwenyehisa" kuliko yote mengine. Mapumziko ya kodi na usaidizi viliondolewa kwenye sekta na kutumika kupunguza ushuru kwa gawio, mauzo ya hisa na bondi.

Wakati New Labour ilipowasili ... kanuni ya "light-touch" ilizinduliwa ili kuweka sekta hiyo ipanuke. Mjadala thabiti wa wafadhili walitongozwa kuingia serikalini ili kuwezesha yote haya.

Na sekta ya fedha iliyozidiwa kwa hakika haijasaidia kwa utawala bora vilevile. Hakuna demokrasia yoyote kuhusiana na upunguzaji mkubwa wa utumishi wa umma unaotumika kulipia kuiokoa sekta ya benki ya kibinafsi, kama katika matokeo ya mporomoko wa 2008, au masoko ya bondi yanayoamua uaminifu wa serikali, au ukweli kwamba mabenki na fedha za kulinda hasara ndizo chanzo kikubwa zaidi cha kipekee cha michango ya chama cha Conservative. Wala imani katika demokrasia ya Uingereza haiwezi kuimarishwa na Waziri Mkuu tajiri kupitiliza ambaye amedaiwa kukwepa kodi na kujipatia utajiri kama mfadhili kwa gharama ya taifa. (Chanzo: The Guardian)

Maoni:

Rush Sunak ndiye Waziri Mkuu wa kwanza wa Uingereza asiye na asili ya kizungu, lakini ulimwengu haupaswi kutarajia chochote kubadilika, kwani kimsingi hakuna kilichobadilika. Kama mwanachama wa conservative, utiifu wake daima utakuwa kwa kipote cha matajiri, ambapo kwa upande wa Uingereza kimsingi ni wanabenki wa jiji.

Je, inashangaza kwamba kuna mlango unaozunguka kati ya wanabenki wakuu, washauri wao, wasimamizi na wanasiasa wakuu? Ni klabu ya kipote cha mabwenyenye, ambapo wanafichiana migongo yao.

Uislamu kwa upande mwingine kwa mfano wa Khilafah umeonyesha muundo thabiti na wenye kuwajibika wa utawala, ambapo maslahi ya raia kwa jumla hayatolewi kafara kwa ajili ya maslahi ya kipote cha matajiri.

Aisha alisimulia kuhusu Mtume (saw): Maquraishi waliingiwa na wasiwasi sana juu ya yule bibi wa Kimakhzumi aliyeiba. Wakasema: “Hakuna awezaye kusema na Mtume wa Mwenyezi Mungu (kumuombea mwanamke huyo) na hakuna wa kusubutu kufanya hivyo isipokuwa Usama ambaye ni kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Wakati Usama alipozungumza na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu jambo hilo, (mtume) alisema, «أَتَشْفَعُ فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللَّهِ؟» “Je, unaniombea nivunje moja ya adhabu (had) ya Mwenyezi Mungu?” Kisha akasimama na kuwahutubia watu, akisema, «يَا أَيُّهَا ​​النَّاسُ إِنَّمَا ضَلَّ مَنْ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ، وَإِذَا سَرَقَ الضَّعِيفُ فِيهِمْ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ، وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعَ مُحَمَّدٌ يَدَهَا» “Enyi watu! Kwa hakika Mataifa ya kabla yenu yalipotoka, kwa sababu walikuwa mtu mtukufu akiiba, walikuwa wakimuacha, lakini mtu dhaifu miongoni mwao akiiba walikuwa wakimuadhibu. Wallahi, lau kama Fatima, binti ya Muhammad angeiba, ningeukata mkono wake!”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu