Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Unyumbuaji Misuli wa Kijeuri wa IMF ili kunyakua Utawala wa Uchumi wa Bangladesh Unafichua Uhusiano Halisi wa Bwana na Mtumwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa umeelezea hatua pana za mageuzi, ikiwemo kuleta nidhamu katika sekta ya fedha na kuongeza ukusanyaji wa mapato, kwa Bangladesh kupata mkopo wa dolari bilioni 4.5. Hatua hizo zilijadiliwa wakati wa msururu wa mikutano kati ya ujumbe uliozuru wa IMF na mashirika mbalimbali ya serikali na idara za Bangladesh. (The Daily Star)

Maoni:          

Jinsi IMF inavyorandaranda ndani ya afisi mbalimbali za serikali nchini Bangladesh, kama vile Bodi ya Kitaifa ya Mapato (NBR), Wizara ya Fedha na Benki ya Bangladesh (benki kuu ya Bangladesh), ni ukiukaji wa wazi wa itifaki na kanuni zote za kidiplomasia. Sio hivyo tu, wawakilishi wa IMF wanafanya mikutano ya moja kwa moja na maafisa kutoka tarafa za vituo hivi vya neva vya nchi, wakiwahesabu, kuwashinikiza na kuwapa maagizo juu ya hatua za baadaye. Inafichua uhusiano wa bwana na mtumwa kati ya IMF na Bangladesh. IMF, chombo cha ukoloni mamboleo wa Magharibi, haikuonyesha hata uungwana wa chini kwa vibaraka wao wa ndani kwa sura ya wanasiasa na maafisa wa serikali na kama ilivyotarajiwa, serikali ya Bangladesh haikuona aibu katika uvunjifu wa sheria huu wa kimatusi uliofanywa na IMF na ikaliita hili 'mambo ya kawaida'. Baadhi ya wanaojiita wasomi wanauwasilisha udhibiti huu wa wazi na uvamizi wa taasisi hii ya Kikoloni kama baraka kwa watu wa Bangladesh! Wanakuuza wazo kwamba matakwa ya uundaji sera ya marekebisho yaliyotolewa na IMF kwa hakika ndio sharti la utulivu wa uchumi wetu. Timu ya IMF ilidai kuongezwa kwa ukusanyaji wa mapato, kupunguza mfumko wa bei, kupunguza mikopo ya asili katika sekta ya benki, kuondoa kiwango cha riba kinacho chukiza na kuweka kiwango cha ubadilishanaji fedha za kigeni kinachoegemea soko na mengine mengi. Zahid Hussain, mfanyikazi wa zamani wa Benki ya Dunia alisema, ‘haya ni matatizo yanayojulikana sana, ya zamani na kizingiti cha muda mrefu cha uchumi wa Bangladesh. Sasa, kutokana na shinikizo la IMF, serikali inapaswa kuzingatia masuala haya kwa uzito’. Kwa uhalisia, IMF inafahamu vyema kwamba bila matatizo haya kutengenezwa na kuendelea kuwepo katika uchumi, hakuna nchi itakayoomba mikopo ya IMF. Sasa, ni ukweli unaojulikana na uliothibitishwa kwamba IMF na washirika wake moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja wanazua shida kama hizo katika mataifa dhaifu ili kuzifunga nchi hizo kwa ofa zao za mkopo. (An Economic Hit Man Confesses and Calls to Action, John Perkins: TEDx Talks).

Baada ya kushindwa katika vita vya msalaba, Ulaya ya Kikristo iliunda ‘Ligi Takatifu’ mbalimbali ili kuwashinda Waislamu na kuanzisha mashambulizi mbalimbali ya kijeshi na uvamizi wa kimishenari. Baada ya 1683 M, Waislamu walipolazimishwa kuondoka kwenye ‘Mkamato wa Vienna’, uvamizi huu wa kimishenari uliongezeka na baadaye kufanikiwa kuivunja Khilafah mwaka wa 1924. Hata hivyo, uvamizi wa wamishonari haukuishia hapo. Sasa, baada ya miaka mingi sana, uvamizi wa kimishenari bado unaendelea mithili kwa sura ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi za maendeleo ambayo yalifikia maelfu na Kanisa la Uingereza, Kanisa la Sweden, Kanisa la Denmark, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri na Mamlaka nyingine za Kanisa mbali na mipango ya kikoloni kama USAID, UKAID, DANINA n.k wanamwaga mabilioni ya dolari kila mwaka kwenye NGOs hizo ili zifanye kazi katika nchi za Waislamu. Kwa hivyo haiaminiki kwamba IMF inaweka masharti hayo ili kupata tu awamu za mikopo yake ya dolari bilioni chache wakati wamiliki wa IMF wamekuwa wakitoa kwa ukarimu katika miradi mbalimbali ya wazi na ya siri nchini Bangladesh. Ukweli ni kwamba, mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yanafanya kazi mashinani nchini Bangladesh kueneza imani ya Kikafiri, fahamu na tamaduni za Dola hizo za Kikoloni ili kuzifanya fikra hizi zikubalike kwa Waislamu na IMF/Benki ya Dunia zimekuwa zikifanya kazi ya kurasimisha na taasisisha udhibiti wao juu ya Dola yetu kwa muda mrefu. Katika Quran Tukufu Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya kuhusu nia zao halisi:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِنْ دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَاعَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Aali-Imran: 118].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Risat Ahmed
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu