Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika Yaonekana Kuhifadhi Mizani Mpya barani Ulaya

(Imetafsiriwa)

Habari:

Hivi majuzi, Marekani imependekeza kuwa subira ya nchi zinazoiunga mkono Ukraine itapungua ikiwa mazungumzo ya amani na Urusi hayataanza.  [Washington Post]  Mabadiliko ya sauti kutoka kwa utawala wa Biden yanaonyesha kuwa labda Amerika haitaki kuona Urusi ikidhoofika zaidi.

Maoni:

Kwa mara ya kwanza, inaonekana ni jambo la ajabu kwa utawala wa Biden kumhimiza Rais Zelensky kushiriki katika mazungumzo ya amani, hasa wakati Ukraine imepata mafanikio makubwa na kuharakisha kurudi nyuma kwa Urusi kutoka maeneo kadhaa muhimu. Zaidi ya hayo, kushindwa kwa Urusi kuanzisha ubwana wa anga na rasimu ya uhamasishaji ya Putin-kubwa zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia-inaonyesha waziwazi jinsi gani vita hivyo vinavyoendelea kwa Urusi. Kwa kuzingatia hali mbaya ya Urusi, mtu angetarajia Biden kuishinikiza Ukraine kufikia mafanikio zaidi kwenye uwanja wa vita kabla ya mazungumzo yoyote ya amani.

Uchunguzi wa karibu wa dhurufu nyuma ya juhudi za Amerika kuifanya Ukraine izungumze na Urusi unaonyesha mtandao mgumu wa mambo yanayofanya kazi. Bei ya juu ya kawi-iliyosababishwa na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine na vikwazo vya Magharibi-inafanya kuwa vigumu kwa watu wa Marekani kumudu kupanda kwa gharama za maisha. Zaidi ya hayo, majaribio mtawalia ya Hazina ya Marekani ya kukabiliana na mfumko wa bei kwa kuongeza viwango vya riba hadi viwango vipya hayajafeli tu bali pia yamezidisha mateso kwa watu. Mgogoro mithili ya huo wa gharama ya maisha unaleta uharibifu kote Ulaya na kuipima azma ya washirika wa karibu wa Amerika hadi kikomo. Halafu kuna tishio la kudumu kutoka kwa chama cha Republican kuzuia mswada wa msaada wa Ukraine. Hili linaweza kutokea mara baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula—ambapo Wanarepublican wanatarajiwa kupata mafanikio makubwa katika Bunge la Marekani la Congress.

Haya yote ni mambo muhimu ambayo husaidia kuipa maisha marefu sera ya Amerika ya Ukraine. Lakini sababu muhimu zaidi nyuma ya msimamo wa hivi karibuni wa Amerika ni kwamba mizani imepatikana na ukuu wa Amerika kuregeshwa. Sera ya mambo ya nje ya Marekani inatazamiwa kudumisha mizani ya mamlaka katika sehemu mbalimbali za dunia chini ya uangalizi wa utawala wa Marekani. Uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine ulitegemea kuidhoofisha Urusi na sio kuiangusha nchi hiyo. Mnamo Aprili Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin alisema, "tunataka kuona Urusi inadhoofika kiasi kwamba haiwezi kufanya aina ya mambo iliyoyafanya katika kuivamia Ukraine." [CNN] Hii ina mantiki ya kimkakati kwa sababu ikiwa Urusi ingeporomoka, ingeleta ombwe la usalama katika Asia ya kati, kuiwezesha China kupanua ushawishi wake katika Eurasia na kuathiri mkakati uliopo wa Amerika wa kuidhibiti China.

Kwa jinsi mambo yanavyoendelea, watunga sera wa Marekani wamekadiria kwamba Urusi imedhoofika sana, majeshi yake yamedhalilishwa, na Ulaya—hasa Ujerumani—inategemea zaidi usalama wa Marekani kuliko wakati mwingine wowote. Kwa hivyo, kwa kuzingatia sababu zilizotajwa hapo juu zilizothibitishwa na mizani mpya barani Uropa, Biden anatazamia kuimarisha amani kati ya Ukraine na Urusi. Wakati wa mazungumzo yoyote ya amani, Amerika itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa Ukraine isiyokaliwa kimabavu inakiuka mipaka kwa Urusi, na hivyo kuifanya kuwa nchi ya Asia isiyoweza kuleta changamoto za kiusalama kwa Ulaya.

Ni wajibu kwa Waislamu wenye ufahamu kuwa na utambuzi wa siasa za mamlaka kati ya dola kubwa na kupatiliza fursa za kuukomboa Ummah kutokana na minyororo ya dola za kigeni.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu