Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Unyanyasaji wa Watoto Umefikia Kiwango cha Juu sana nchini Ufilipino, huku nchi za Magharibi zikiwa ndio Wahalifu Wanaoongoza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ufilipino ndiyo nchi yenye uzalishaji mkubwa zaidi wa nyenzo za unyanyasaji wa watoto. Mashirika ya kutoa misaada yamekadiria kwamba mtoto 1 kati ya 5 hudhulumiwa, na kwa kawaida wazazi na watu wa ukoo hufaidika kutokana na unyanyasaji huo. Kufungwa kwa miji wakati wa Janga la maambukizi kuliwaacha watoto walio hatarini wakiwa wamenaswa na watu wazima walio na tamaa ya kifedha. Wengi huenda wamewahi kuwa na historia za unyanyasaji na wamelifanya hii kuwa jambo la kawaida katika tamaduni zao. Mtandao wa kasi wa intaneti unaolipiwa na mamilioni ya wateja barani Ulaya, Marekani na Uingereza umeufanya unyanyasaji wa watoto unaofanywa na vyombo vya habari vilivyo athirika kipesa kuwa rahisi sana. Sekta ya kuwaharibu watoto kwa sasa ni biashara ya kiulimwengu ya mabilioni ya dolari.

Maoni:

Tabia  mbovu na potovu za fikra huria za Kimagharibi zinachafua ulimwengu mzima. Mamilioni ya watoto ambao wamepoteza maisha yao kwa fikra za kuhudumia uhuru wa watu wengine ni hadithi ya kusikitisha isiyoelezeka.

Njaa ya kibepari ya kupata faida kwa gharama yoyote ile ndiyo nia ya kinyama inayowasukuma wazazi kuwauza watoto wao utumwani. Watalii na wavamizi wa mtandaoni hujihisi huru kulipa ili watoto wadhulumiwe. Utamaduni huu potovu kamwe hautakoma, wakati ufadhilishaji pesa juu ya maadili unatawala ulimwengu. Mizunguko ya umaskini inayosababisha kutapatapa pia haitakwisha kamwe kwa mifumo mibovu ya kiuchumi iliyopo ambayo inaruhusu matajiri kutajirika zaidi na maskini kutegemea madeni ili kuishi.

Nidhamu ya hudud ya Sharia kwa hakika ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwani daima umetumika kama kizuizi madhubuti cha kuhakikisha haki za binadamu za watu. Hatua madhubuti za kuhakikisha kwamba hatia imethibitishwa pasi na shaka na adhabu kubwa kwa jinai mbaya zaidi iliifanya Khilafah kuwa mahali penye usalama wa hali ya juu kwa raia na watoto wote. Sio tu kwamba haki za kimwili za watoto zinalindwa kwa ukaribu katika Khilafah, Quran inakataza kwa uwazi unyanyasaji wa kihisia, kwani kuwalaani watoto wako na kutumia maneno ya kudhalilisha kuumiza hisia za mtu ni ni yenye kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu (swt).

«لَا تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ وَلَا تَدْعُوا عَلَى أَوْلَادِكُمْ وَلَا تَدْعُوا عَلَى خَدَمِكُمْ وَلَا تَدْعُوا عَلَى أَمْوَالِكُمْ لَا تُوَافِقُوا مِنْ اللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى سَاعَةَ نَيْلٍ فِيهَا عَطَاءٌ فَيَسْتَجِيبَ لَكُمْ»

“Musiziapize nafsi zenu, na musiwaapize watoto wenu, na watumishi wenu, na musiziapize mali zenu, musije mukamwomba Mwenyezi Mungu wakati wa kujibiwa du’a.”

Watoto katika Khilafah watafundishwa katika mfumo wa elimu unaofunza haya kuhusiana na vitendo vya kimwili visivyo halali na ulinzi wa faragha ya mwili. Leo kinyume chake inafunzwa katika mifumo ya elimu ya Kimagharibi huku uthabiti wa kijinsia na uasherati ukirejelewa kama njia ya furaha. BBC iliripoti mnamo Novemba 2022, mwanamume aliyebadili jinsia alimlea na kumshambulia msichana wa miaka 14 ambaye alipata ujauzito. Urahisi wa mahusiano kati ya wageni ndio sababu ya unyonyaji mkubwa wa vijana walio katika mazingira magumu duniani. Tunatoa wito wa kuregeshwa kwa mfumo wa haki na safi kwa namna ya Quran na Sunnah ili watoto wa dunia waweze kuokolewa na laana ya Urasilimali na maadili ya kiliberali.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu