Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuhalalisha Mahusiano na Umbile la Kiyahudi ni Wenyewe ni Usaliti Ewe Çavuşoğlu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akizungumza katika kikao cha Mazungumzo Maalum cha Jukwaa la 8 la Mazungumzo ya Mediterania, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu alisema, “Itakuwa ni makosa kufikiria kuwa kuhalalisha mahusiano na Israel ni usaliti kwa kadhia ya Palestina.” (Nationality 03.12.2022)

Maoni:

Akiwahutubia viongozi wa Waarabu mnamo Oktoba 03, 2020, Erdogan alisema, “Jaribio lolote linaloidhinisha mipango ya Israel ya kuitwaa Jerusalem na ardhi ya Palestina na ambalo linapuuza haki halali za ndugu zetu wa Palestina ni usaliti kwa imani ya Salahuddin Ayyubi.” Naam, tunauliza: kwa nini ule uliokuwa usaliti jana umeacha kuwa usaliti leo? Na kwa nini kuashiria tukio hili kama usaliti kunaonekana kama fikra ya makosa? Ali al-Qaradaghi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu, Ali al-Qaradaghi, alisema katika taarifa yake mnamo Septemba 12, 2020, “Kuhalalisha mahusiano na Israel ni usaliti mkubwa wa kanuni zote za kibinadamu, kitaifa na Kisharia.” Na maafisa wengi zaidi wa AKP wamesema kuwa kuhalalisha mahusiano na "Israel" ulikuwa usaliti. Ni kitu gani kimebadilika? Je, ni dhana ya kisiasa au maslahi, au ni kwamba Uturuki inatenda kwa mujibu wa sera za bwana wake, Marekani, kama sehemu ya sera ya Marekani ya kulioanisha umbile la Kiyahudi ndani ya ulimwengu wa Kiislamu?

Kando na kukaliwa kwa mabavu Palestina na Jerusalem, kuhalalisha mahusiano na umbile nyakuzi la Wazayuni, ambao waliwaua raia 10 wa Uturuki huko Mavi Marmara mnamo 2010, wakiwakaribisha katika Jumba la Rais, na kuteua balozi, achilia mbali kuuhesabu kama usaliti wa Uislamu na Waislamu, ni usaliti kabisa kwa watu wa Uturuki. Kinyume na madai ya Çavuşoğlu ni usaliti kwa kadhia ya Palestina kwamba, serikali ya Erdoğan, ambayo inafanya kazi kwa fikra mbovu na iliyopitwa na wakati kulinda serikali yake fisadi na kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi, na kwa kudai “hakuna kinyongo katika siasa”, ilipanda treni ya uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, adui mkubwa wa Uislamu na Waislamu, na utawala wa Assad, mchinjaji na muuaji wa Waislamu.

Kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi bila shaka ni usaliti mkubwa kwa mujibu wa Uislamu. Kwa kuwa inachukuliwa kuwa usaliti mkubwa kulingana na Uislamu, Waislamu tangu 1948, tarehe ya kuanzishwa, walikubali na kuamini kuwa kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi ni usaliti. Kwa sababu ya imani hii iliyokita mizizi na kuzama ndani ya Waislamu, watawala wasaliti na majasusi hawakuweza kuhalalisha mahusiano yao na umbile la Kiyahudi kwa miongo kadhaa ili wasiweze kukabiliwa na hasira na uwezekano wa uasi usioweza kudhibitiwa wa watu, na ilibidi wafanye mahusiano nyuma ya milango iliyofungwa. Kama inavyojulikana, uhalalisha mahusiano ni neno la kisiasa ambalo linaonyesha kuhalalisha mahusiano kati ya vyombo vya kisiasa baada ya mvutano, migogoro na vita. Kuhalalisha mahusiano maana yake ni kutambua haki ya umbile nyakuzi na vamizi la Kiyahudi ya kuishi katika ardhi tukufu ya Palestina.

Ikiwa misamiati ya usaliti na uhalalishaji mahusiano itaachiwa akili ya mwanadamu, itatofautiana kulingana na wakati na mahali. Kwa mfano, kulingana na Erdogan, kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi ilikuwa usaliti jana, na sio leo. Kwa hiyo, haiwezi kuachiwa akili ya mwanadamu kuamua nini ni usaliti na nini sio. Kwa sababu wakati hapo itatofautiana kulingana na watu na hali, kama ilivyo leo. Lakini, kulingana na Uislamu, uhalalishaji mahusiano na umbile nyakuzi la Kiyahudi ni dhambi kubwa na uadui. Kwa sababu inamaanisha kuridhia na kukubali unyakuzi, uadui na uchokozi wa mnyakuzi dhidi ya ardhi ya Kiislamu na Waislamu. Kwa sababu hii, Uislamu unalichukulia umbile lolote ambalo limenyakua ardhi yoyote ya Kiislamu kama adui na kuwachukulia wale wanaotenda kinyume na mtazamo huu kama wasaliti, na kukichukulia kitendo hiki kuwa ni usalit. Uhalisia huu hautofautiani wala haubadiliki kulingana na zama, mahali, watawala na wanasiasa. Haijalishi tuko katika zama gani, na haijalishi ni nani anayeingia madarakani, hii haitabadilika, na hata wale wanaojaribu kubadilisha hawa watachukuliwa kuwa wasaliti.

[لَتَجِدَنَ أَشَدّ النَاسِ عَدَاوَةً لِلَذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma’idah 82]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu