Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 ‘Matumizi ya Ubaguzi wa Rangi kama Chambo cha Kisiasa’ Ni Ala Nyengine Tena ya Kuchukiza ya Siasa Chafu za Kisekula

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika wiki za hivi karibuni, vyombo vya habari vya Uingereza vimeangazia matumizi ya  ‘ubaguzi wa rangi kama chambo cha kisiasa’ na mawaziri mbalimbali katika serikali ya Uingereza ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura wa mrengo wa kulia na chuki dhidi ya wapiga kura wenye asili ya kigeni. Inafuatia msururu wa kauli za kashfa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Suella Braverman ambaye aliwataja wanaume wa Pakistan wa Kiingereza kuwa na uwezekano wa hali ya juu ya kuwa sehemu ya magenge ya wanaohusika na unyanyasaji wa kijinsia kwa wasichana wazungu wanaoishi katika mazingira magumu nchini humo, ambayo ni sifa ya tabia hiyo ya kinyama inayohusishwa kwa namna fulani na kabila au tamaduni zao. Alilega moja kwa moja katika msururu wa kesi kubwa zinazohusisha wanaume wenye asili ya Pakistan badala ya kukiri kwamba unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ni tatizo lililoenea nchini, linalohusisha sekta na makabila yote. Alisema kuwa wahalifu wa uhalifu wa kingono unaohusisha magenge ni "makundi ya wanaume, karibu Wapakistani wote wa Uingereza". Hii ni licha ya ukweli kwamba ripoti ya 2020 kutoka kwa Afisi yake ya Mambo ya Ndani ilisema kwamba ilipata shida sana kupata uhusiano kati ya ukabila, rangi na unyanyasaji wa kijinsia wa watoto, na kuhitimisha kuwa wanachama wengi wa magenge ya kuwaharibu watoto walikuwa wanaume weupe walio chini ya umri wa miaka 30. Hii haishangazi kwa kuwa idadi kubwa ya watu ni weupe. Braverman pia alisema katika mahojiano ya Sky News kwamba wanaume wa Pakistani wa Uingereza, "huwatazama wanawake kwa njia ya kudhalilisha na isiyo halali na ambao hufuata njia ya kizamani na ya kuchukiza kabisa kwa jinsi wanavyotenda". Waziri huyo wa Mambo ya Ndani pia ametoa matamshi kadhaa ya dharau dhidi ya wahamiaji, kuwataja wahamiaji na wanaotafuta hifadhi wanaovuka kwa boti ndogo kuingia nchini kama 'wavamizi' na kuhusisha uhamiaji na viwango vya juu vya uhalifu, uuzaji wa dawa za kulevya, ukahaba na unyonyaji. Robert Jenrick, Waziri wa Uhamiaji, pia alisema, "uhamiaji kupita kiasi, usio na udhibiti unatishia kumonyonyoa huruma inayoashiria jamii ya Uingereza" na kwamba wale wanaovuka kuingia nchini wanajumuisha "mitindo na maadili tofauti kwa wale walio nchini Uingereza ... kudhoofisha mshikamano wa kitamaduni unaounganisha jamii mbalimbali pamoja."

Maoni:

‘ubaguzi wa rangi kama chambo cha kisiasa’ ni matumizi ya kauli za uchochezi au uwongo kuhusu rangi au uchochezi wa chuki ya rangi au hasira dhidi ya makabila fulani, mara nyingi ili kupata manufaa ya kisiasa. Chombo hiki kimekuwa ni sehemu kubwa ya siasa za kisekula na mbinu ya kuandaa uchaguzi katika dola za kisekula kote ulimwenguni. Haishangazi kwamba kauli za Braverman na Jenrick zilikuja dhidi ya mazingira ya chaguzi za mitaa mwezi huu na uchaguzi mkuu unaokaribia mwaka ujao nchini. Kauli za kupinga uhamiaji na chuki dhidi ya Waislamu pamoja na siasa za utambulisho zinazolenga makabila fulani kwa muda mrefu zimekuwa kelele za usuli wa uchaguzi wa rais wa Ufaransa huku wagombea wakishindana wao kwa wao ili kuwaonyesha wapiga kura wao ni nani aliye na sifa kubwa zaidi za chuki dhidi ya wageni. Wanasiasa wa mirengo yote nchini Ufaransa - kushoto, kulia na katikati - wamesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya raia wa kigeni nchini humo kumeshusha maadili ya jadi ya Kifaransa. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema wakati wa uchaguzi wa mwaka jana wakati wa mkutano wa kisiasa kwa wafuasi wake, "Tunapoogopa matukio ya uhamaji, nadhani lazima pia tutetee DNA yetu." Katika siasa za Marekani, mikakati iliyobuniwa kuwatia shaka na kuwaogopa Wamarekani Weusi na wahamiaji imetumika kwa muda mrefu kushinda uchaguzi. Donald Trump alitumia maneno ya chuki dhidi ya wahamiaji na chuki dhidi ya wageni ili kuyashawishi maeneo fulani nchini katika chaguzi za urais za 2016 na 2020.

Haya yote kwa mara nyingine tena yanadhihirisha hatari na migawanyiko ya asili ya mfumo wa kisekula wa kibepari ambapo wanasiasa hawana mashaka juu ya kueneza uwongo, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya makabila ili kushinda chaguzi. Ni mfumo unaowaruhusu wanasiasa kuzichezea jamii dhidi ya wenzao, kuchochea chuki za rangi na kuwatia moyo watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia kwa manufaa ya kisiasa bila kujali matokeo mabaya kwa maisha ya watu binafsi na jamii. Mwaka jana, uhalifu dhidi ya Waislamu uliongezeka kwa 28% nchini Uingereza. Hili lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na kukua kwa makundi ya chuki ya mrengo wa kulia ambayo yalitumia dhana potofu kuhusu Waislamu, ikiwa ni pamoja na zile zinazouzwa na wanasiasa. Mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya kituo cha wahamiaji huko Dover na wakimbizi wanaoishi katika hoteli huko Knowsley nchini Uingereza pia yalihusishwa na lugha ya uchochezi dhidi ya wahamiaji iliyotumiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza. Mnamo mwaka wa 2019, gaidi wa mrengo wa kulia, Brenton Tarrant, ambaye aliwaua Waislamu 51 kwenye misikiti 2 huko Christchurch, New Zealand, aliandika "kwa Rotherham" kwenye risasi yake kabla ya kuifyatua. Rotherham ni mji nchini Uingereza ambao wanasiasa wa mrengo wa kulia mara nyingi hutumia kama mfano kutangaza uwongo wao wa ushiriki usio wa usawa wa wanaume wa Kipakistani katika magenge kutokana na kesi ya kiwango cha juu ambapo wanaume kadhaa wa Kipakistani walipatikana na hatia ya unyanyasaji wa wasichana wadogo wa kizungu.

Je, mfumo kama huu ambao unaoendekeza lugha hii kwa malengo ya uungwaji mkono kisiasa, mtindo wa siasa wa Machiavelli ambapo malengo huhalalisha njia na ambapo hakuna kitu hafifu ilimradi tu kunaleta kura chache duni, kitaonekane kama njia bora ya kutawala serikali? Je, mfumo kama huu unaotumia maoni ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni na unaochochea chuki na mivutano ya kikabila badala yake unaotaka kuwaondoa, unatawezaje kuunda jamii zenye mshikamano na salama? Je, mfumo kama huu unaowaruhusu wanasiasa kujaribu kukuza umaarufu wao kwa kutumia wachache kama mifuko ya kushinda uchaguzi, unawezaje kuonekana kuwa wa maendeleo na wa kistaarabu? Na mfumo kama huu unaoleta mgawanyiko kati ya watu na kuzitenga jamii unawezaje kuonekana kuwa muundo salama wa kisiasa?

Sisi kama Waislamu, kwa hakika umefika wakati wa kuukataa mfumo huu wa kisekula uliotungwa na mwanadamu kutoka katika ardhi zetu ambao vile vile umezua mgawanyiko baina ya Waislamu na kuruhusu wanasiasa kuuchochea moto wa ubaguzi wa rangi katika jamii zetu kwa manufaa ya kisiasa! Hakika umefika wakati wa kuregea kwenye Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo ina njia iliyojaribiwa kwa muda mrefu ya kung’oa ubaguzi wa rangi kutoka kwa watu na kuwayeyusha wale wa makabila na mataifa mbalimbali ndani ya dola moja ambapo wote wanahisi kuheshimiwa na kulindwa kwa usawa kupitia sheria za adilifu za Uislamu. Hakika umefika wakati wa kuanzisha tena mfumo huu wa kimaendeleo na wa kistaarabu ambao chini yake siasa inahusu kuchunga mahitaji ya watu kwa dhati badala ya kuleta pambano la kurushiana matope kati ya wanasiasa wanabinafsi na wenye uchu wa madaraka ambao wako zaidi ya tayari kuwasha moto wa ubaguzi wa rangi ndani ya jamii zao kwa manufaa yao ya kisiasa!

[ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَى شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاء الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

“Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu.” [Al-Jathiya: 18]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu