- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Je, Marekani Inazingatia Mtindo wa Uturuki kwa Pakistan?!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Zalmay Khalilzad alinukuu tweet, "Pengine maafa yanaweza kuepukwa, lakini ikiwa tu mambo 2 yatatokea. Mkuu wa Jeshi Munir anahitaji kujiuzulu, na uchaguzi lazima kutangazwa kwa tarehe maalum. Bila ya la kwanza, la pili haliwezekani. Bila hatua hizi mzozo wa kiuchumi, kisiasa na usalama wa Pakistan utazidi kuwa mbaya.” (The Tweet)
Maoni:
Tweet hiyo imeibua wasiwasi kwamba kwa namna fulani Marekani inahusika katika kuvunjika kwa jeshi la Pakistan. Wengine hata walidhani kwamba Marekani inapendelea mtindo wa Uturuki wa utawala, yaani, ambapo jeshi liko chini ya udhibiti wa raia ambaye, badili yake, anafanya kazi kikamilifu kulinda maslahi ya Marekani.
Yamkini, chini ya mtindo huu, Khan atasimamia jeshi la Pakistan kupitia Mkuu mpya wa Majeshi (CoAS), na mamlaka yake yatapunguzwa ili kuzuia ushiriki wa jeshi katika siasa za Pakistan. Sababu nyingine iliyotajwa kuunga mkono madai kama hayo ni kwamba Marekani lazima iidhoofishe Pakistan ili India iingie kikamilifu kukabiliana na China. Sehemu ya mpango huu ni pamoja na kuipokonya Pakistan silaha zake za nyuklia, kupunguza ukubwa wa vikosi vya kijeshi vya Pakistan hadi 200,000, kuisalimisha Kashmir kwa India kupitia kuifanya Laini ya Udhibiti (LoC) kuwa ya kudumu, na hatimaye kuunganishwa kwa Pakistan katika shirikisho pamoja na India.
Uchunguzi wa karibu wa utawala wa Marekani nchini Pakistan unakanusha uvumi kama huo. Hii ni kwa sababu Marekani, kwa miongo kadhaa, imetumia utashi wake kupitia jeshi la junta kusimamia masuala ya ndani ya Pakistan, maendeleo ya kitaasisi ya jeshi la Pakistan, pamoja na sera pana za kigeni za nchi hiyo.
Ukakamavu wa jeshi umetekeleza matakwa ya Marekani kwa uaminifu kila ilipohitajika. Kwa mfano, Jihad ya Afghanistan ilikuwa biashara ya Marekani iliyobuniwa kuharibu Umoja wa Kisovieti. Ili kutoa maisha marefu kwa juhudi hii ilimaanisha kuwa jeshi la Pakistan lililazimika kuifanya jamii ya Wapakistani kuwa ya Kiislamu ili kuunga mkono juhudi hii kikamilifu. Hili lilihitaji mabadiliko ya mtaala wa elimu katika kuunga mkono Uislamu, kuenea kwa madrasa, kuanzishwa kwa kambi za mafunzo kwa Wanajihad, na kushajiishwa kuwavuta wasomi na wapiganaji wa Kiarabu kuishi na kupata mafunzo katika kambi hizi.
Baada ya 911, Marekani iliamua kubadili sera yake ya Uislamu ya Pakistan. Musharraf alilazimika na sio tu kubomoa miundombinu ya wanajihad bali alianzisha operesheni za kijeshi ili kuwakamata na kuwaweka jela makumi ya maelfu ya raia wa Pakistan. Chini ya enzi ya Musharraf, kuondolewa kwa Uislamu Pakistan kuliongezewa na kuongeza kasi ya kuitia Umagharibi Pakistan.
Musharraf alienda mbali hata zaidi kuliko ilivyotakiwa na akaweka ulinzi kwa baadhi ya silaha za nyuklia ambapo iliiwezesha Marekani kufuatilia zilipo na pia kupanga mipango ya kuisalimisha Kashmir ili kuiimarisha India. Warithi wa Musharraf kama vile Kayani, Sharif, na Bajwa wametenda kwa ukaidi sawa na wametekeleza majukumu yao kwa uaminifu kwa Marekani.
Wakati wa utawala wa Marekani nchini Pakistan, kipaumbele chake kikuu daima kimekuwa kuhakikisha uadilifu wa ukakamavu wa jeshi. Kuuvunja vunja uongozi wa jeshi huku Marekani ikitafuta kuiorodhesha India katika vita vinavyotarajiwa dhidi ya China ni ujinga. Uongozi wa jeshi uliovunjika unaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe au utekaji nyara wa wanamgambo wa Kiislamu. Baya zaidi, inaweza kuharakisha uasi wa Pakistan, ambao utakuwa ni jinamizi kwa usalama kwa India na kuzuia majaribio ya Marekani kuitumia India dhidi ya China.
Mbali na hilo, kuliweka jeshi chini ya utawala wa kiraia kuna uwezekano wa kulitia nguvu jeshi hilo kupinga majaribio yoyote ya kulidhoofisha. Katika siku za nyuma, Marekani ilifanikiwa kudhoofisha jeshi la Pakistan kwa kusukuma mabadiliko kupitia CoAS na kuhakikisha uadilifu wa jeshi la junta kutekeleza utashi wa Washington. Muundo huu wa utendakazi hauwezekani kubadilika hivi karibuni.
Kwa ujumla, Magharibi imetumia kwa mafanikio mfumo dhaifu wa kiraia au pazia ya demokrasia inayofanya kazi chini ya kivuli cha jeshi lenye nguvu ili kudhibiti sehemu nyingi za ulimwengu wa Kiislamu na kuzuia muungano wake wa kimaumbile. Hivyo basi, mtindo huu wa utawala utabadilika pale tu uongozi wa jeshi utakapoacha utiifu wake kutokana na kulinda maslahi ya Magharibi na kuupeleka katika kutawala kwa Uislamu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti