Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Tubadilishe Dereva au Gari?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Erdogan, ambaye ameshinda tena uchaguzi wa urais, alitangaza Baraza jipya la Mawaziri la Rais lililokuwa likitarajiwa sana katika Jumba la Çankaya.

Maoni:

Katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa, mawaziri wengine wote wamebadilika isipokuwa wawili tu. Mehmet Şimşek, jina lililotarajiwa sana katika uchumi, aliletwa kwa Wizara ya Hazina na Fedha, huku Ali Yerlikaya, Gavana wa zamani wa Istanbul, akiletwa kwa Wizara ya Mambo ya Ndani. Ilhali Hakan Fidan akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, Yaşar Güler akiwa Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa. Ibrahim Kalın akaletwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi.

Inawezekana kulitathmini baraza jipya la mawaziri kwa njia kadhaa:

Rais Erdogan alipoanzisha mfumo wa urais wa mtindo wa Marekani, alibuni taasisi za serikali, ambazo hapo awali zilitawaliwa na Waingereza, ili kutumikia siasa za Marekani. Kwa kuchaguliwa tena kwa Erdogan kama Rais na mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri, ililengwa kwamba maafisa watiifu kwa Marekani wawekwe kuwa wasimamizi wa taasisi za kimkakati za serikali na serikali haipaswi kutoka nje ya udhibiti wa Marekani hata kama kuna mabadiliko madaraka katika mchakato ufuatao. Kwa hivyo, hata ikiwa Erdogan ataanguka kutoka mamlakani, Marekani imeimarisha zaidi uwezekano wa kudumisha utawala wake nchini Uturuki kupitia taasisi.

Kwa upande mwingine, uteuzi wa Mehmet Şimşek, mmoja wa mawaziri wapya, katika Wizara ya Hazina na Fedha ulisababisha msisimko na matarajio makubwa katika jamii. Kumekuwa na upungufu mkubwa wa uwekezaji wa mtaji wa moja kwa moja wa kigeni unaoingia Uturuki katika miaka ya hivi karibuni. Kwa kuregeshwa kwa Mehmet Şimşek kama mkuu wa uchumi, ililenga kuongeza kuegemea katika soko la kimataifa na kuingia tena katika nchi mtaji wa moja kwa moja wa kigeni.

Hata hivyo, leo kuna mgogoro mkubwa wa kiuchumi nchini Uturuki, ambapo uwezo wa ununuzi umepungua kutokana na mfumko wa bei wa juu, kuumiza watu, kuwaburuza watu katika umaskini na taabu kila siku. Kuna mchakato unaendelea ambapo lira ya Uturuki inapoteza thamani dhidi ya dolari siku baada ya siku. Ugumu wa kiuchumi umezunguka pande zote za maisha. Matarajio yametolewa kwamba Waziri wa Hazina na Fedha Mehmet Şimşek angesuluhisha matatizo ya kiuchumi. Mazingira yaliundwa katika mwelekeo huu; “Je, Mehmet Şimşek anaweza kutatua matatizo yote haya?’’ Haijulikani, lakini suluhu ya matatizo ya sasa si kumbadilisha waziri. Mawaziri kadhaa wamebadilishwa kabla ya hili, lakini matatizo yamebakia yale yale. Kwa kweli, yaliendelea kuongezeka. Serikali sitini na sita zimebadilika kutoka msingi wa jamhuri hadi leo. Na sasa serikali ya sitini na saba imeingia madarakani. Lau utatuzi wa matatizo ungesababishwa na mabadiliko ya madaraka au mtu, moja ya mamlaka hizo ambazo zimefika hadi sasa ingefanikiwa kutatua matatizo yaliyopo. Lakini hadi sasa, haijawahi kufanikiwa. Baada ya hapo, kamwe haitafanikiwa vilevile.

Tatizo kuu ni mfumo. Chanzo cha matatizo yote haya na migogoro ni mfumo wa kidemokrasia wa kirasilimali unaotabikishwa leo na mpangilio wake wa kiuchumi. Ni nidhamu ya pesa za karatasi ya mfumo huu. Ni mfumo wa benki uliojengwa juu ya riba na soko la hisa ambazo huwanyonya watu na kutengeneza pesa kutokana na pesa. Mfumo huu si wa kibinadamu, hauna maadili na sio wa Kiislamu. Unatokana na unyonyaji. Upo tu ili kuwafanya wachache kuwa na furaha na matajiri zaidi. Hauwasumbui hata mabepari kuona watu wanaishi maisha duni katika umasikini. Mfumo huu haujali kuhusu upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa watu na ugavi wao wa adilifu miongoni mwa watu.

Hivyo basi, maadamu utaratibu wa kiuchumi wa kibepari unatekelezwa, kamwe haitawezekana kutatua matatizo ya kiuchumi yanayoendelea. Hoja sio kubadilisha dereva, lakini kubadilisha gari yaani, mfumo wa kibepari. Hata hivyo, suluhisho pekee la matatizo ni kusimamisha tena Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo utatekeleza utaratibu wa kiuchumi wa Uislamu kwa ujumla wake.

[وَمَنْ اَعْرَضَ عَنْ ذِكْر۪ي فَاِنَّ لَهُ مَع۪يشَةً ضَنْكًا]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Ta-Ha 124]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz ÇELİK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu