Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utawala wa Magharibi na Uhalalishaji wa Haki za LGBT nchini Japan: Funzo kwa Waislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Japan ilipitisha mswada wenye utata unaolenga kukuza ufahamu wa jumuiya ya LGBT, licha ya ukosoaji kwamba inakosa hakikisho la haki za binadamu na inaweza kuunga mkono ubaguzi kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Kama nchi pekee ya G7 bila ulinzi wa kisheria kwa miungano ya watu wa jinsia moja, Japan ilikabiliwa na shinikizo, haswa kutoka Marekani, kuzitambua ndoa za jinsia moja. Hata hivyo, sheria mpya iliyopitishwa haifikii matarajio hayo. Rasimu ya awali ya mswada huo, ambayo ilisisitiza haja ya "kutovumilia" ubaguzi kwa msingi wa mwelekeo wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia, ilirekebishwa ili kueleza kuwa kusiwe na "ubaguzi usio wa haki." Wakosoaji wanasema kuwa mabadiliko haya yanaruhusu upendeleo unaowezekana. Ingawa raia wengi wa Japan wanaunga mkono ndoa za watu wa jinsia moja, haki za ushirika zinazotolewa kwa sasa hazilingani na zile za ndoa. (CNN, 16/06/2023) 

Maoni:

Huku kukiwa na mgogoro wa idadi ya watu wa Japan, uamuzi wa nchi hiyo wa kuhalalisha haki za LGBT unaonyesha ukosefu wake wa uhuru katika siasa za ndani. Kwa mtazamo wa kimantiki, mtu anaweza kusema kwamba Japan inapaswa kutanguliza kulinda raia wake kwa kuendeleza ndoa za kitamaduni, kukuza ustawi, na kupiga marufuku shughuli kama vile ngono huru na ndoa za jinsia moja. Hata hivyo, kwa sababu ya kuonekana kuwa Japan inajifungamanisha na udhibiti wa kisiasa wa nchi za Magharibi au utawala wa kivita, nchi hiyo inatatizika kutunga sera zinazozingatia maslahi yake na hatima yake. Uhalisia huu unaonyesha hatari za asili za kutegemea dola za kikoloni za Kimagharibi. Zaidi ya hayo, uanachama wa Japan katika vikao vya Magharibi kama vile G7 unaweza kuwa mtego, unaohatarisha ubwana wa serikali yake na kuizuia kuchukua hatua kwa maslahi yake yenyewe. Ni muhimu kwa Japan kutambua kwamba vikao na mashirika ya kimataifa si lazima yaendeleze mahusiano kwa usawa kati ya wanachama; badala yake, wale walio na mamlaka makubwa zaidi huwa na udhibiti juu ya mwelekeo wa mambo ya kimataifa. Mienendo mithili ya hiyo inaweza kuzingatiwa katika mashirika mengine ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Biashara Duniani, na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambayo mara nyingi huonekana kama zana za dola za Kimagharibi kukuza fikra za kisekula na za kiliberali na kutangaza utawala kote ulimwenguni.

Jambo hili linapaswa kuwa funzo kwa Waislamu kote duniani, likiwasaidia kuelewa athari mbaya za kuanzisha mahusiano ya karibu na dola za Kimagharibi, ima kupitia ushirikiano wa pande mbili au wa pande nyingi. Kiasili si haramu kushirikiana na nchi zisizo za Kiislamu, lakini masharti fulani lazima yazingatiwe, kama vile kuhakikisha kwamba ushirikiano huo haugongani na maslahi na maadili ya ulimwengu wa Kiislamu au hauambatani na maadui wa Uislamu. Ushirikiano unapaswa kujikita katika kanuni za Kiislamu badala ya kuegemea mapatano ya kisekula, kiliberali na kibepari pekee. Muhimu zaidi, uhusiano na dola ya Kiislamu na nyinginezo unapaswa kuegemezwa kwenye lengo la da'wah, kutaka kusimamisha ulimwengu unaotawaliwa na Uislamu. Mtazamo huu unawakilisha njia pekee ya kueneza rehema (rahmah) kwa Umma na wanadamu huku ukijilinda dhidi ya athari za fikra na dola haribifu zinazoleta tishio kwa maisha ya mwanadamu na ulimwengu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu