Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Erdogan “Muislamu” Alishindwa katika Uchaguzi wa Rais na Erdogan Mwanademokrasia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Raia wa Uturuki katika uchaguzi wa Mei 28 walionyesha utashi na azma ya kuunga mkono njia ya maendeleo zaidi ya nchi. Hayo yamesemwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, akiwahutubia wananchi waliokusanyika mnamo Jumatatu usiku kwenye Ikulu ya Rais jijini Ankara, tovuti ya shirika la habari la Anadolu inasema.

Kiongozi huyo wa Uturuki amewashukuru wapiga kura wote kwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa upigaji kura, bila kujali chaguo la kisiasa. “Sio sisi pekee ambao tumeshinda. Uturuki imeshinda, demokrasia imeshinda!” Erdogan alisema.

Mwanasiasa huyo alikumbuka hayo tangu enzi ya Waziri Mkuu wa zamani Adnan Menderes katika miaka ya 1950. Katika njia ya maendeleo ya Uturuki, matatizo yaliundwa mara kwa mara ili kudhoofisha nchi.

“Leo, tunatangaza kuanza kwa mchakato ambao utaturuhusu kufikia malengo yaliyotangazwa na Rais wa zamani Turgut Ozal na Waziri Mkuu wa zamani Necmettin Erbakan.”

Mkuu huyo wa nchi alihakikisha kwamba kwa kuzingatia kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi nchini Uturuki, mamlaka inakusudia kuzingatia muda na nguvu zao zote katika kuchangia maendeleo ya nchi. “Nina hakika kwamba tutatekeleza pia fahamu ya Miaka 100 ya Uturuki kwa msaada na pamoja na wananchi,” Erdogan alisema.

Rais huyo alielekeza umakinifu zaidi katika hali ya nchi jirani ya Syria. Mkuu wa nchi alisema kuwa hadi wakimbizi 600,000 wameregea kwa hiari kutoka Uturuki hadi maeneo ya usalama katika ardhi ya Syria hadi sasa. “Shukran kwa mradi wa pamoja wa Uturuki na Qatar wa ujenzi wa nyumba katika ardhi ya Syria, tunapanga kurudisha wakimbizi wengine milioni 1 nchini Syria,” shirika hilo lilimnukuu Erdogan akisema.

Maoni:

Licha ya uongozi finyo dhidi ya mgombea wa upinzani na raundi ya pili ya uchaguzi, kushindwa kwa Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan hakukuwa na uwezekano. Ujanja pekee ilikuwa jinsi Erdogan angefanikiwa kushinda uchaguzi kwa mara nyingine na kubakia na mamlaka yake, akitwaa urais kwa mara ya tatu. Baada ya yote, alifika katika hatua ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi na kushuka kwa kiasi kikubwa katika kuorodheshwa kwake dhidi ya mazingira ya mgogoro mkubwa wa kiuchumi na matokeo ya mkasa wa tetemeko la ardhi la Februari nchini Uturuki.

Ni upendeleo tu ya Marekani ndio unaomsaidia Erdogan, aliyepewa jina la utani na vyombo vya habari vya Ulapa "asiyeweza kuzama" na "asiyeweza kuangamia", kusalia anaelea. Tangu katikati ya karne iliyopita, Amerika imejitahidi kuelimisha na kuimarisha vibaraka wake nchini Uturuki. Tangu ushindi wa chama cha Kidemokrasia katika uchaguzi wa miaka ya hamsini, Amerika imejaribu mara kadhaa kuwaleta watu wake mamlakani nchini Uturuki. Walakini, kutokana na mapinduzi kadhaa ya kijeshi, walichanganyika, na wengine waliuawa, na ilibidi kujenga upya kila kitu. Hiki ndicho anachomaanisha Erdogan anaposema kwamba “tangu utawala wa Waziri Mkuu wa zamani Adnan Menderes katika miaka ya hamsini. Matatizo hujitokeza mara kwa mara kwenye njia ya maendeleo ya Uturuki.”

Marekani ilitambua kwamba ingeweza kuimarisha ushawishi wake kwa kutumia katika kuwaunga mkono vibaraka wake wapiga kura kutoka miongoni mwa Waislamu, ndani ya nyoyo zao ambao wengi wao mapenzi ya Uislamu yangali hai. Tangu miaka ya sabiini, Amerika imechangamsha wanasiasa, vuguvugu na vyama vilivyotumia matamshi na kauli mbiu za Kiislamu kwa madhumuni ya umaarufu. Wanasiasa wanaoiunga mkono Marekani walianza kujificha nyuma ya Uislamu, tofauti na wale wanaoiunga mkono Uingereza, ambao walitetea waziwazi usekula na walikuwa na uadui na Uislamu.

Nchini Uturuki, tofauti na nchi zingine za Kiislamu, ambazo zingine zilitangazwa kuwa jamhuri za Kiislamu, Amerika ilitumia kinachojulikana. "Uislamu wa kisiasa", mwanzilishi wake ni Necmettin Erbakan, aliyetajwa na Erdogan. Kuudandia Uislamu na kuutumia kama kichocheo, hadi mwisho wa miaka ya tisiini ya karne iliyopita, vibaraka wa Marekani hatimaye waliweza kukazanisha mshiko wao wa mamlaka. Kwa kuingia madarakani kwa Chama cha Haki na Maendeleo, kinachoongozwa na Erdogan, Uturuki hatimaye ilihamia kwenye mzunguko wa ushawishi wa Amerika, na kuwa moja ya vyombo vikuu vya utekelezaji na ulinzi wa maslahi yake, katika kanda za Mashariki ya Kati na Afrika, na katika Transcaucasus na Asia ya Kati.

Akitaka hatimaye kukomesha upinzani wowote wa ndani, Erdogan anatoa wito wa kukusanyika pambizoni mwa fahamu ya "Miaka 100 ya Uturuki" aliyoivumbua, bila kusahau kusifu kwa mara nyengine tena demokrasia. "Ningependa kutoa shukran za taifa langu kwa kutupa likizo ya demokrasia," Erdogan alisema, akizungumza na wafuasi wake jijini Istanbul. "Ningependa kuwashukuru wawakilishi wote wa taifa letu, bila ubaguzi, ambao kwa mara nyingine walitukabidhi jukumu la kuongoza nchi kwa miaka mitano ijayo, kwa chaguo walilolifanya," Erdogan alinukuliwa akisema na Deutsche Welle katik hotuba kwa wafuasi wake jijini Istanbul.

Anazungumza kwa namna hii wakati wote, kama vile baada ya ushindi wake wa kwanza katika uchaguzi wa urais mwaka wa 2014, aliposema: “Ninashukuru taifa kwa kuniteua kuwa Rais wa 12 wa Jamhuri ya Uturuki. Sitakuwa rais wa walionipigia kura pekee, nitakuwa rais wa milioni 77. Leo mapenzi ya watu yameshinda tena, leo demokrasia imeshinda tena. Wale ambao hawakunipigia kura walipata sawa na wafuasi wangu. Wale ambao hawanipendi walipata ushindi sawa na wale wanaonipenda."

Maneno ya Erdogan: “Uturuki imeshinda, demokrasia imeshinda!” hakuna jipya. Amesisitiza mara kwa mara kujitolea kwake kwa demokrasia. Kwa mfano, alipokuwa akipinga shutma kutoka kwa wanasiasa wa Ulaya na upinzani wa ndani wa ubabe na udikteta, baada ya kukandamizwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililofeli mwaka 2016, alijisifu kama “mwanademokrasia wa kihafidhina.”

Ili kuyabakisha madaraka mikononi mwake, Erdogan analazimika kuthibitisha kuwa yeye sio mzalendo kuliko wapinzani wake wa kisiasa. Na sasa tunaona jinsi mgombea kutoka kwa Umoja wa Wazee wa Kitaifa (ATA), Sinan Ogan, ambaye alipata 5% ya kura katika raundi ya kwanza, aliwataka wafuasi wake kumpigia kura Erdogan, ambaye alipata jina la utani “mjengaji mtawala” kwenye vyombo vya habari. Kwa kuwa, kutokana na kura za wapiga kura wake, Erdogan hakuweza kunyakua ushindi kutoka kwa mpinzani wake Kemal Kılıçdaroglu, ambaye aliahidi kuwafukuza wakimbizi wa Syria ikiwa atashinda, kusamehe mikopo na kufanya matangazo ya bure ya mechi za ligi ya kitaifa ya soka.

Kulingana na David Hearst, mhariri mkuu wa tovuti ya habari ya Kiingereza ya Middle East Eye: “Wala kampeni ya Kilicdaroglu ya hofu si maneno matupu tu. Kuwalaumu waathiriwa kwa maafa waliyowatengeneza inaonekana kuwa kipengele cha mantiki ya utaifa.” Lakini Erdogan hata hakumtia aibu mpinzani wake, lakini, kama wanavyosema, "alicheza kwenye uwanja wake", akitumia "kampeni ya hofu" iliyochochewa na wana Kemal. Kwa maneno ya upole, pia anaahidi kutatua "tatizo la wakimbizi" kutoka Syria, licha ya ukweli kwamba, katika kutekeleza agizo la Amerika la kukandamiza mapinduzi dhidi ya kibaraka wake mwengine - Bashar al-Assad, serikali ya Erdogan ni mmoja wa wahusika wakuu wa mateso ya Waislamu nchini Syria.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mustafa Amin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu