- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Madhalimu Hutumia Maadili ya Kiislamu Kuwahadaa tu Waislamu pekee
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Juni 8, shirika la habari la Radio Liberty nchini Tajikistan liliripoti: “Sherehe ya ufunguzi wa msikiti mkubwa zaidi nchini Tajikistan ilifanyika Dushanbe. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Rais wa Tajikistan Emomali Rahmon na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim ibn Hamad Al Thani, ambaye aliwasili Dushanbe mnamo Juni 8 kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili.
Mamlaka za Tajik zinauita ujenzi wa msikiti mkubwa zaidi nchini humo kuwa ni mfano wa kuheshimu uhuru wa kidini, lakini mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na nchi za Magharibi mara kwa mara yanakosoa serikali ya Tajik kwa kuzuia uhuru wa kidini wa waumini.
Jiwe la msingi la msikiti huo liliwekwa na Rais Rahmon mwezi Oktoba 2009, wakati wa maadhimisho ya miaka 1310 ya mwanzilishi wa madh’hab ya Hanafi, Imam Abu Hanifa.
Msikiti Mkuu huo mpya wa Dushanbe, ambao ujenzi wake serikali ya Qatar imewekeza dolari milioni 70, unaweza kuchukua kwa wakati mmoja waumini 133,000, ambapo waumini 43,000 watakuwa ndani ya msikiti, na wengine pambizoni wake".
Maoni:
Ujenzi wa misikiti mikubwa umekuwa ndio mila ya madikteta wa Asia ya Kati. Msikiti kama huo, mkubwa zaidi ulifunguliwa na rais wa kwanza, Nursultan Nazarbayev, huko Nur-Sultan, mji mkuu wa Kazakhstan, mnamo Agosti mwaka jana. I. Karimov, kabla ya kifo chake, pia aliweza kufungua Msikiti mdogo katika mji mkuu wa Uzbekistan, Tashkent.
Hivyo, madikteta hutumia maadili na kauli mbiu za Kiislamu ili kuwahadaa Waislamu, wakionyesha madai yao ya kujitolea kwa Uislamu na Waislamu. Kwa bahati mbaya, Waislamu wanadanganywa na kujifariji kwa maneno "hapa wanajenga misikiti na kuturuhusu kuswali".
Lakini Uislamu haujumuishi tu msikiti, swala na saumu. Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, jamii na dola. Mtawala wa Waislamu, Khalifa au Imamu, anatawala kwa msingi wa Quran na Sunnah, anatabikisha Shariah katika mfumo wa kijamii, kiuchumi na kisiasa. Huduma za afya, elimu, ujenzi na ibada ndani ya dola hiyo vyote vimejengwa juu ya Uislamu. Haitoshi tu kujenga msikiti. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitukufu:
[أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ ٱلْحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ كَمَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْءَاخِرِ وَجَٰهَدَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ لَا يَسْتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ]
“Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuamirisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” [9:19].
Watawala wetu hawatawali kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na wameufunga utawala wao ndani ya mipaka iliyochorwa na wakoloni wabaya kwa msingi wa utaifa. Madhalimu hawa hawaenezi Uislamu, hawafanyi jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hawatabikishi Uislamu ndani ya dola yao wenyewe. Zaidi ya hayo, wanatumika tu kuwafurahisha mabwana zao. Siku chache kabla ya ufunguzi wa msikiti huo, Juni 5, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Sergei Lavrov aliwasili Tajikistan na kuanza ziara yake katika kambi ya 201 ya kijeshi ya Urusi huko Dushanbe, ambapo walizungumza juu ya vita na Ukraine. Ni wazi, vita dhidi ya Ukraine vinahitaji rasilimali kwa Kremlin, na Rahmon kwa uwajibikaji hutoa rasilimali za nyenzo na Waislamu wa Tajikistan ili kuwahudumia wakoloni makafiri.
Waislamu! Hapana shaka kwamba Uislamu ni dini kamili (Dini), ambapo kuna ufumbuzi wa matatizo yote katika maisha. Na kwa hiyo, fanyeni haraka kufidia kile kilichopotea na kukosekana katika maisha yetu, yaani utawala kwa msingi wa Quran na Sunnah. Fanyeni haraka kuhuisha Dola ya Pili Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume! Na twamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir