Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Demokrasia Kamwe Haitaruhusu Utabikishwaji wa Kina wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mapigano yalizuka kati ya wafuasi wa JI na PPP nje ya Baraza la Sanaa la Pakistan (ACP) jijini Karachi mnamo tarehe 15 Juni, baada ya upigaji kura wa uchaguzi wa meya wa jiji kukamilika. Naibu Inspekta Jenerali wa Kusini (DGP), Irfan Ali Baloch, alisimulia kwamba makabiliano yalizuka baada ya ripoti za Mwanasheria wa PPP Murtaza Wahab kushinda katika kura kuibuka.

Maoni:

Uchaguzi wa serikali za mitaa wa jiji la Karachi ulipingwa vikali na vyama vikuu vya kisiasa. Chama tawala cha Sindh, Chama cha Watu wa Pakistan (PPP), kilituhumiwa na vyama vya upinzani kwa wizi wa kura. Hakuna chama ambacho kingeweza kufanikiwa kupata kura nyingi. Chama cha PPP kiliibuka kuwa chama kikubwa zaidi, kikifuatiwa na Jamat-i-Islami (JI) na Tehrik-e-Insaf (PTI). PPP na JI zote zilihitaji kuungwa mkono na PTI, ili kumchagua mgombea wao, kama Meya wa Karachi. Hatimaye PTI ilitangaza kumuunga mkono mgombeaji wa JI. Ilikuwa wazi kwamba muungano huu sasa ulikuwa na wingi wa wazi. Hata hivyo, siku ya uchaguzi wa meya, zaidi ya nusu ya wanachama wa PTI walikosa kupiga kura. Kwa hivyo mgombea wa PPP alishinda kinyang'anyiro hicho.

Drama hii haijafanyika nchini Pakistan kwa mara ya kwanza. Yeyote anayefurahia uungwaji mkono wa watawala halisi, taasisi ya jeshi, anaweza kupata matokeo yanayohitajika. Hapo awali, JI alishinda wadhifa wa meya wa Karachi wakati wa enzi ya Jenerali Musharraf. Ilifanyika kwa sababu Musharraf alihitaji kuungwa mkono na vyama vya Kiislamu. Alihitaji kupunguza shinikizo dhidi yake kwa sababu ya kuunga mkono "vita dhidi ya ugaidi" vya Marekani. Aliamuru MQM, chama kikuu cha kisekula cha Karachi wakati huo, kususia uchaguzi. Kwa hivyo, JI ilifanikiwa. Funzo linalopaswa kusomwa ni kwamba hakuna chama kinachoweza kufanikiwa bila msaada wa watu wenye mamlaka. Hii haijalishi ni watu wengi kiasi gani wanaounga mkono mitaani au kwenye kura.

Funzo jengine ni kwamba kushiriki katika mfumo wa kidemokrasia hakuimarishi njia ya Kiislamu. Inanufaisha tu mwendelezo wa mfumo wa kidemokrasia wenyewe. Kuimarishwa kwa mfumo wa kidemokrasia kunahujumu mapambano ya kusimamisha tena utawala wenye msingi wa Uislamu, Khilafah. Maridhiano na Uislamu yanachukuliwa kama mkakati chini ya mapambano ya kidemokrasia. Yeyote anayekataa maridhiano juu ya Uislamu anachukuliwa kuwa asiyefaa. Hata hivyo, uzoefu wa Erdogan na vyama vya Kiislamu vya kidemokrasia vya Pakistan, umeweka wazi kwamba utawala kamili wa Kiislamu hauwezi kutawala katika Demokrasia. Barabara na mitaro ya kupitisha maji taka zinaweza kujengwa, lakini utukufu wa Shariah hautapatikana kamwe chini ya Demokrasia.

Mabadiliko ya kweli yanawezekana tu kwa kufuata Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hakushiriki katika mfumo wa kikafiri, licha ya kupewa vyeo ndani yake. Yeye (saw) alifuata njia aliyoamuru Mwenyezi Mungu (swt). Aliweka Dawah yenye nguvu kwa Uislamu. Pia alitafuta Nusrah kutoka kwa watu wenye nguvu kwa ajili ya kusimamisha Uislamu. Pindi watu wenye nguvu mjini Madina, Answari, walipotoa Nusrah yao, dola ya kwanza ya Kiislamu ilipatikana, bila ya kuasi amri hata moja ya Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo, ni juu ya Waislamu wote kushikamana na njia hii, kwa ikhlasi na subira., bila ya kupotoka, mpaka Mwenyezi Mungu (swt) alete Nusra yake.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

{إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُمْ بِغَيْرِ حِسَابٍ} “Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.” [Surah Az-Zumar 39:10].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Sheikh – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu