Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vuta ni Kuvute ya Dola za Magharibi nchini Kosovo na Dori ya Uturuki

(Imetafsiriwa)

Habari:

Eneo la Balkan linasalia kuwa mazingira mwanana kwa mivutano ya kikabila. Machafuko ya hivi karibuni nchini Kosovo kwa mara nyengine tena yalizua wasiwasi kwa nchi za Ulaya kwa utulivu wa bara Ulaya.

Maoni:

Mvutano uliongezeka wakati serikali ya Kosova ilipopitisha sheria mnamo 2022 zinazohitaji watu wa Serbia kaskazini mwa Kosovo kubeba hati za vitambulisho vya Kosovo na nambari za usajili wa magari. Hii ilisababisha kujiuzulu kwa mameya wenye asili ya Kiserbia na maafisa wa polisi na maandamano makubwa kaskazini. Waserbia walikataa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo ilisababisha wagombea Waislamu kushinda jambo lililochochea ghasia zaidi.

Urusi imeonyesha uungaji mkono mkubwa kwa Waserbia na kulaani vitendo vya Kosovo, ikionya juu ya uwezekano wa "mlipuko mkubwa" katika Balkan. Serikali ya Urusi imeelezea wasiwasi wake na kudokeza uwezekano wa kuingilia kijeshi.

Nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani, zimetaka hatua za haraka zichukuliwe ili kupunguza hali ya wasiwasi na kuwataka viongozi wa Serbia na Kosovo kupunguza mvutano huo. Juhudi zimefanywa kutuliza hali, huku Waziri Mkuu wa Kosovo akionyesha nia ya kushiriki katika mazungumzo na majadiliano yanayofanyika kati ya viongozi wa Kosovo na Serbia.

Kuhusika kwa Urusi katika kuchochea mvutano nchini Kosovo ni kusababisha matatizo ya ndani barani Ulaya kutokana na msimamo wao katika mzozo wa Urusi na Ukraine. Nchi za Magharibi zinajitahidi kudhibiti hali hiyo na kuzuia kuongezeka zaidi, kwani zinatambua uwezekano wa mzozo huo kuvuruga eneo hilo na kugeuza rasilimali kutoka kushughulikia mgogoro wa Ukraine.

Kwa jumla, nchi za Magharibi zinafanya juhudi za kutuliza hali na kuzuia mvutano wa Kosovo usizidi kuwa mzozo mkubwa, huku Urusi ikilenga kutumia hali hiyo kwa manufaa yake.

Utulivu wa Kosovo ni muhimu, na ni muhimu kwa EU na Marekani kufuatilia kwa karibu hali hiyo. Ndiyo maana, NATO kwa uratibu na EU, imetuma kikosi cha makomando wa Uturuki kama sehemu ya "misheni ya kulinda amani" nchini Kosovo.

Kinaya ni kwamba EU imepiga hatua chanya kuelekea Serbia kuhusiana na uanachama wake wa EU huku ombi la fedheha la Uturuki la uwanachama wa EU limewekwa kwa muda usiojulikana ndani ya  friza.

Inatia uchungu kuona kwamba jeshi la Uturuki limepandikizwa nchini Kosovo na EU na NATO, wakati Kosovo hadi 1918 ilikuwa sehemu ya Khilafah ya Uthmani. Ni dola hizo hizo za Magharibi ambazo hapo awali zilichochea mivutano ya kikabila na harakati za kujitenga dhidi ya Khilafah. Ilhali, leo, wajukuu wa Mauthmani wanajituma "kulinda amani" kati ya mivutano hii ya kikabila na kusaidia malengo na ajenda za ukoloni mamboleo wa Magharibi.

Fahamu ya madhumuni ya jeshi katika Uislamu ni kulinda Dini, damu na heshima ya Waislamu na kuwaleta wasiokuwa Waislamu kwenye Nuru ya Uislamu. Uislamu umekuja kuwaokoa watu kutoka katika minyororo ya dhulma na ukandamizaji wa mifumo iliyotungwa na mwanadamu hadi kwenye uadilifu wa Uislamu. Haukuja kutumikia mifumo dhalimu na ya udanganyifu iliyotungwa na wanadamu au kutumiwa nayo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu