- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Na Madhara Yanaendelea...
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika nia ya kuuridhisha Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), serikali ya Pakistan imetangaza kuondoa mara moja vikwazo vya kuagiza bidhaa kutoka nje. Hata hivyo, jumuiya ya wafanyibiashara na wachambuzi wote wanaamini kuwa hatua hii pekee haitaleta mabadiliko makubwa katika shughuli za kibiashara za kiutendaji isipokuwa akiba ya fedha za kigeni itaimarishwa kwa kiasi kikubwa. (Tribune)
Maoni:
Pakistan tangu kuundwa kwake imekuwa katika hali ya mgogoro wa kiuchumi na inazidi kuzama katika mtego wa umaskini. Kwa hakika, umaskini huu unachangiwa na viongozi wasiofaa na wadanganyifu wanaotawala Pakistan na nchi nyingine za ulimwengu wa tatu. Nchi hizi ziliachwa kwenye uchafu na kupewa hadhi ya kuwa taifa baada ya kutawaliwa na wabunifu wa sasa kwa mikopo na mitego ya umaskini wa kukopesha. Mfumo wa kiuchumi ambao unatumika nchini Pakistan unaunda mzunguko wa umaskini wa kujiimarisha wenyewe. Pakistan ilijiunga na IMF mwaka 1950 katikati ya matatizo ya kifedha. Mnamo 1958, Pakistan ilikuwa nchi ya kwanza kutafuta msaada kutoka kwa IMF. Uwe utawala wa kidemokrasia au kijeshi, wa kisekula au wa kihafidhina, kila mtu aliinamia IMF na Benki ya Dunia. Baada ya Ayyub, ilikuwa ni njia isiyozuilika iliyopitishwa na kila mtawala, na hii ilileta tu madhara kwa watu. Waziri wa Fedha Ishaq Dar ametangaza kuongeza zaidi ya bilioni 215 katika kodi mpya. Mzigo wa kodi hizi huwakumba watu wasio na uwezo zaidi huku matajiri na wenye ushawishi wakikwepa au kulipa kiasi kidogo tu. Mfumko wa bei nchini umevuka mipaka na kuna kupanda kwa bei za vyakula.
Amesema Mtume (saw). «لا ضرر ولا ضرار» “Hakuna kudhuru (darar) wala kudhuriwa (dhirar).”
Waziri Mkuu anayehudumu wa Pakistan, Shehbaz Sharif tayari alisema mwanzoni mwa mwaka wa 2023 kwamba masharti ambayo tutalazimika kukubaliana na IMF ni hayaingii akilini. Lakini itabidi tukubaliane na masharti hayo.” 2023 itaadhimisha kumbukumbu ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Pakistan lakini tunaona kuzorota kwa mara kwa mara kijamii, kimaadili, kifikra na kiuchumi. Sababu ya kuporomoka huku kwa mara kwa mara ni kutofuata wazo la kuundwa kwa nchi hii, ambalo lilikuwa ni kuwa na Dola iliyojemgwa juu ya msingi wa mfumo wa Kiislamu ambao hatimaye utakuwa ndio mwavuli wa sehemu zote zilizotawanyika za Umma wa Kiislamu. Waislamu wa Bara hili dogo wanaweza kuwa wamepata uhuru wa kimwili na kuhamia pamoja katika eneo lenye Waislamu wengi lakini mambo hayakwenda mbali zaidi ya hilo. Kwa hivyo, dola hii ya kitaifa iligeuka kuwa gereza la Waislamu ambapo bei za bidhaa kwa usambazaji wa vifaa hupangwa na wale waliotupa hadhi ya uhuru. Kwa hivyo, Pakistan hivi sasa inaweza kuwa inaziwepesisha dola za Kibepari lakini haina mfumo inaoufuata. Mfumo wa uchumi wa kibepari una lengo moja tu nalo ni kuongeza utajiri jumla wa nchi, na kufikia kiwango cha juu zaidi cha uzalishaji na anasa za kiwango cha juu kwa watu binafsi. Chini ya mfumo wa sasa wa kibepari wa kimataifa, taasisi kama IMF hutengeneza pesa kwa kuzifanya nchi za Ulimwengu wa Tatu kuwa watumwa kupitia mikopo ambayo kamwe hazitaweza kuilipa. IMF yenyewe ni taasisi ya kisiasa, inasimamiwa na watu walioteuliwa kisiasa kutoka mataifa wanachama, na maslahi ya kisiasa ya wanachama wake huathiri maamuzi yake. Hii ndiyo sababu tunaona IMF ikifanya kazi kama chombo cha sera za kigeni cha Marekani.
Sera ya Uislamu ya kiuchumi inatokana na Shari’ah (Qur’an na Sunnah) na kufaulu au kufeli kwake hakupimwi kwa faida na hasara. Badala yake, hupimwa kwa vipimo vya halali (yaliyoruhusiwa) na haramu (yaliyoharamishwa) na vinavyozingatia ugavi wa mali na kukataza kuhodhi. Mzunguko wa mali huleta ustawi na kutengeneza fursa kwa watu.
Ardhi za Waislamu ni lazima ziunde sera ya kiuchumi inayotokana na Aqidah ya Kiislamu. Sera nyengine yoyote ya kiuchumi ni mbovu, sio tu kwa ajili ya utulivu wa kiuchumi bali hata kama mtu anapata manufaa kutokana na mfumo mwingine wa kiuchumi unaogongana na Uislamu basi anakuwa ni muasi kwa Mwenyezi Mungu (swt), wala kuunda na kujaribu kuitekeleza hakutasababisha matokeo yoyote zaidi ya kuongeza matatizo ya kiuchumi, kuwafukarisha watu, kuendeleza mporomoko na matatizo. Kwa hivyo, sera ya uchumi ya ardhi za Kiislamu lazima iwe sera ya kiuchumi ya Kiislamu kama ilivyokuwa siku zote. Kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume kutawasaidia Waislamu kuregesha heshima na utukufu wao uliopotea. Sisi kama Waislamu lazima tukumbuke kwamba mafanikio yetu yanategemea utiifu wa Mwenyezi Mungu, sio kwa hatua ambayo itatusaidia kuishi wakati huu, lakini inatusukuma kwenye hasira ya Mwenyezi Mungu (swt). Sisi Waislamu wa Pakistan tunakataa kudanganywa zaidi na kukataa kuwa wahanga wa mikataba yoyote ya IMF.
Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [Sura An-Nur 24:55].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan