- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza Inataka Kuipiga Marufuku Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Habari:
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly alitangaza kupiga marufuku Hizb ut-Tahrir, akilitaja kama shirika la kigaidi. Alisema kuwa Hizb ina chuki dhidi ya Mayahudi kwa vile ilisherehekea mashambulizi ya Hamas huko Gaza dhidi ya ‘Israel’ mnamo Oktoba 7. Alisema kwamba Hizb iliwasifu Hamas kama mashujaa na kwamba hatua hiyo inashajiisha ugaidi. (BBC 01/15/2024).
Maoni:
Tulisema katika maoni yetu yenye kichwa “Vyombo vya habari vya Uingereza vinataka kuhujumu Dawah ya Hizb ut Tahrir” kwamba “ulinganizi wa Hizb ut Tahrir uliwakasirisha na kuwakera. Kutoa wito kwa majeshi kutaharaki kuinusuru Palestina na kuwaunganisha Waislamu chini ya bendera ya dini kunaashiria mwisho wa utawala wao juu ya nchi za Kiislamu na kurudi nyuma kutoka kwa uongozi wa dunia. Walipiga honi zao ili kupotosha ulinganizi wa Hizb na kuwashambulia wanachama wake, wakidhani kwamba hilo lingewavunja moyo wanachama wa Hizb kutokana na Dawah yao, ambayo ilikuwa imeota mizizi na kuenea miongoni mwa Waislamu. Mashambulizi yao yalizidisha tu kuenea kwa Dawah ya Hizb na mkusanyiko wa umma wa Waislamu walioizunguka, kwani ulinganizi wa haki umedhahiri na ulinganizi wa batili pasi na budi utatoweka.” Na sisi hawa hapa leo tunaona kufeli kwa vyombo vyao vya habari kuhujumu Dawah ya Hizb ut Tahrir. Hawana chaguo ila kuipiga marufuku, ingawa hilo linakiuka uhuru wao wa kirongo na sheria za kirongo.
Ndio, Hizb ut Tahrir imewakera kwa kuyataka majeshi kuondosha viti vya utawala vya madhalimu katika nchi zetu, kutabikisha Uislamu na kutangaza jihad ili kuikomboa nchi na watu wake. Matokeo ya mashambulizi yao ya vyombo vya habari dhidi ya Hizb ni kwamba waliwaunganisha Waislamu kwenye Dawah sahihi, na ilikuwa ni propaganda kwa Hizb ambayo hawakuikusudia. Hawakupata njia yoyote isipokuwa ile sera ya kuwanyamazisha watu, ambayo waliifanya na wanaifanya katika makoloni yao ya kale na ya kisasa katika ulimwengu wetu wa Kiislamu.
Hoja zinazodaiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza za kuipiga marufuku Hizb ni za uongo na ni kinyume na fikra ya Hizb ut Tahrir. Hoja ambazo hazikumdanganya yeyote, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ziliamsha rai ya jamii ya Kiislamu na hata watu wengi wasiokuwa Waislamu, ambao walilaani marufuku hii na sera ya kunyamazisha midomo kwa visingizio duni na kukiuka sheria za uhuru wanazodai. Dawah ya Hizb ut Tahrir ni kusimamisha dola ya Kiislamu katika nchi za Kiislamu ambazo Uingereza na nchi nyingine za Magharibi zilizikoloni na kuzigeuza kuwa magofu baada ya kuwa dola inayoongoza katika nyanja zote, ambapo Waislamu na wasiokuwa Waislamu wataishi chini ya kivuli cha mfumo wa kiwahyi tu ambao Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanautafuta leo.
Mnamo 2005, kiongozi wa chama cha Labour alijaribu kupiga marufuku Hizb ut Tahrir lakini alishindwa, na kisha kiongozi wa Chama cha Conservative David Cameron alijaribu jambo lile lile na akashindwa. Wote wawili walijaribu kuambatanisha mashtaka ya uwongo ya ugaidi na unyanyasaji kwa Hizb, lakini kila mtu anajua njia ya mabadiliko ya Hizb ut Tahrir. Mivutano ya kifikra na mapambano ya kisiasa, njia iliyoelezewa kwa kina katika fasihi yake, ni njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina. Leo, chama tawala cha Conservative kinataka kwa mara nyingine kuipiga marufuku Hizb ili kulifurahisha umbile la Kizayuni, ambalo lilitikiswa hadi mizizi yake baada ya kushindwa kwa kishindo mnamo Oktoba 7, 2023. Marufuku hiyo itajadiliwa katika Bunge la Uingereza na kupigiwa kura mnamo siku ya Alhamisi, 18/01/2024.
Kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Uingereza hakutaizuia Hizb na mashababu wake kutokana na Dawah yao, kwani ni ulinganizi wa haki wa Uislamu, ulinganizi utakaobakia mpaka Mwenyezi Mungu atubariki kwa dola ya Kiislamu, ambayo itaikomboa nchi na watu na kutetea heshima.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 30:4-5].
Imeandikwa kwa Ajili ya Upeperushaji wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Abdul Rahman Al-Ayoubi