Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Miaka 60 ya ‘Mapinduzi’ ya Zanzibar: Kuna Chochote cha Kusherehekea?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Januari 12, 2024 kile kinachoitwa “mapinduzi” ya Zanzibar yalifikisha miaka sitini tangu yalipotokea Januari 12, 1964. Baada ya miaka mingi kupita, swali muhimu linabaki: Je, cha kusherehekea, ukiachilia mbali wanasiasa na wachache katika “familia za wanamapinduzi” je watu wa kawaida wana kitu cha kusherehekea?!

Maoni:

Kwa mujibu wa Serikali (ya Zanzibar) mwaka 2022, biashara ya Zanzibar ilikuwa na thamani ya Sh1.4 trilioni, ikilinganishwa na Sh 913.1 bilioni mwaka 2020, ikiwa ni ongezeko la asilimia 57.6.  Zanzibar imeuza nje bidhaa zenye thamani ya Sh180.4 bilioni mwaka 2022, ikilinganishwa na Sh65.7 bilioni mwaka 2020, sawa na ongezeko la asilimia 174.7. Pia katika upande wa zao kuu la biashara, Zanzibar imeuza nje tani 6,452.8 za karafuu zenye thamani ya Sh118.3 bilioni mwaka 2022 ikilinganishwa na tani 3,506.8 zilizouzwa nje mwaka 2020, zenye thamani ya Sh38.37 bilioni, sawa na ongezeko la asilimia 208.1.

Ingawaje serikali inajaribu kuwafanya watu waamini kwamba kuna mabadiliko chanya na mafanikio katika miaka hii sitini, kwa kweli hii ni kinyume, na kiuhalisia hali ni mbaya zaidi. Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu Tathmini ya Umaskini wa Zanzibar ya mwaka 2022, Zanzibar ilishuhudia ukuaji mkubwa wa Pato la Taifa (GDP) kwa kila mtu kati ya mwaka 2009 na 2019, lakini ukuaji huo haukuongeza matumizi ya kaya, ambayo ina maana ukuaji wa uchumi huu hauakisi chochote katika maisha ya walio wengi, huku wananchi walio wengi bado wako katika umaskini uliokithiri, licha ya takwimu za ukuaji wa uchumi zisizo na maana yoyote.

Umwagaji damu wa Waislamu kwa jina la “mapinduzi” ulisababisha vifo vya Waislamu zaidi ya 17,000 visiwani Zanzibar, kuporwa mali na serikali zikiwemo ardhi, na maelfu kukimbilia Oman na mataifa mengine zikiwemo nchi za Ulaya hususan Uingereza. Mauaji hayo yaliyosukumwa na Uingereza kama ala ya kusahilisha muungano uliofuata kati ya visiwa hivyo na Tanganyika mnamo tarehe 26 Aprili 1964, miezi mitatu tu baada ya mauaji hayo. Jambo hilo lilikuwa ni njia ya Uingereza kubakisha ushawishi wake katika Afrika Mashariki baada ya uhuru wa bendera. Majeraha ya mauaji haya na mbegu ya ubaguzi wa rangi miongoni mwa Waislamu wa Zanzibar ni miongoni mwa athari mbaya zisizosahaulika za baada ya mapinduzi haya. Baada ya haya yote je, tuna la kusherehekea!?

Amma kuhusiana na mapinduzi ya kweli, ni lazima yawe ya kimfumo kwa lengo la kuondoa mfumo muovu na badala yake kuweka mfumo bora zaidi. Mfumo wa kibepari ndio unaopaswa kuondolewa duniani kote, na nafasi yake kuchukuliwa na mfumo wa Uislamu kama mfumo kamili na mpana wenye ufumbuzi wa kila tatizo la mwanadamu, ambao unahitaji kutekelezwa chini ya kivuli cha Dola ya Kiislamu ya kiulimwengu ya Khilafah.

Umma wa Kiislamu una dhima na wajibu wa kumuiga kiongozi wetu Mtume (saw) jinsi alivyoleta mabadiliko ya kimsingi ya kimfumo kwa kubeba fikra madhubuti ya Kiislamu kutoka kwa Muumba iliyozalisha dola huru yenye ufumbuzi wa matatizo yote ya mwanadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu