Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kazakhstan na Afghanistan zote Zinafuata Mfumo wa Kibepari!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirika la habari la Kazinform liliripoti mnamo tarehe 29 Disemba: “Mamlaka za Kazakh zimeamua kuwaondoa Taliban kutoka kwenye orodha ya mashirika yaliyopigwa marufuku. Mwakilishi rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kazakhstan Aibek Smadiyarov alimwambia mwandishi wa Kazinform.

- Kwa nini uamuzi huu ulifanywa?

- Kazakhstan hukagua mara kwa mara orodha ya kitaifa ya mashirika ya kigaidi yaliyopigwa marufuku nchini Kazakhstan ili kuisasisha. Kama sehemu ya mchakato huu, uamuzi ulifanywa kuwaondoa Taliban kutoka kwenye orodha kwa mujibu wa utendakazi wa Umoja wa Mataifa. Kwa hivyo, kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambayo ni ya lazima, Harakati ya Taliban haimo katika orodha ya mashirika yanayotambuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mashirika ya kigaidi.

- Je, mawasiliano ya kidiplomasia kati ya Kazakhstan na Taliban yatakuaje?

- Kuhusiana na mawasiliano ya kisiasa, ningependa kusisitiza kwamba Kazakhstan itaendelea kuzingatia kwa dhati maamuzi na maazimio yaliyopitishwa na Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa”.

Maoni:

Hapo awali, wakati Taliban ilipoingia madarakani nchini Afghanistan, Kazakhstan haikuitambua Taliban kuwa halali na ilisema kwamba “wanaunga mkono taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuzuia uwepo wa makundi ambayo yanatishia mataifa mengine na kuheshimu sheria za kimataifa”. Ni nini kimebadilika katika mahusiano kati ya jamhuri hizo mbili leo?

Kwanza: Ubalozi wa Kazakhstan jijini Kabul umeendelea kufanya kazi na kuanzisha uhusiano wa kibiashara tangu serikali mpya ilipochukua madaraka mnamo 2021, kwa tahadhari tu kwamba ushirikiano sio na Taliban, bali na Afghanistan. Mnamo Aprili 2023, Kazakhstan iliruhusu Taliban kukalia ubalozi wa Afghanistan huko Astana na kuanza kazi. Na leo, mamlaka za Kazakh, tena zikirejelea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zilitoa taarifa mpya kwamba zimeamua kuwaondoa Taliban kutoka kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi. Yaani, waliamua "kuhalalisha" rasmi mahusiano imara ya biashara ambayo tayari yashaanzishwa, kwa sababu itaonekana kuwa Kazakhstan inafanya biashara na shirika ambalo liko kwenye orodha ya marufuku na zaidi ya hayo linachukuliwa kuwa shirika la kigaidi.

Pili: Kazakhstan, ambayo inategemea Urusi, haiwezi tu kuamua mambo yanayohusu usalama wa serikali bila idhini ya bwana wake. Mamlaka za Urusi ziliiongeza Taliban kwenye orodha ya mashirika yaliyopigwa marufuku na ya kigaidi tangu mnamo 2003. Baada ya hapo, jamhuri zote za jirani ndani ya CSTO ziliidhinisha orodha hii ya mashirika yaliyopigwa marufuku, na Taliban ikawa ya kigaidi na kupigwa marufuku katika Asia yote ya Kati. Kwa hivyo, inashangaza kwamba Kazakhstan iliamua kukiuka vifungu vya CSTO na kipeke yake kuwatenga Taliban kutoka kwa orodha hii.

Leo, Urusi, ambayo iko chini ya vikwazo vya kiuchumi na kisiasa, hutumia njia za mkato kuuza rasilimali zake. Kazakhstan, kwa taarifa yenu, ni fursa nzuri kwa Urusi. Kwa kusudi hili, Zh. Tokayev anaonyesha uhuru wake wa madai kutoka kwa Urusi na uhuru wa maamuzi katika kutatua maswala kadhaa. Kwa mfano, kilicho muhimu kwa suala la Urusi ni maeneo yaliyotekwa nchini Ukraine. Tokayev, akionyesha waziwazi uhuru wake kutoka kwa msimamo wa Kremlin, alisema kwamba hatambui uhuru wa Jamhuri za Watu wa Donetsk na Lugansk kutoka Ukraine. Kuondolewa kwa vuguvugu la Taliban la Kazakhstan katika orodha ya mashirika ya kigaidi iliyokusanywa na Urusi mnamo 2003 pia ni moja ya hila kama hizo.

Taliban, kwa upande wake, inataka kutambuliwa na Jamii ya Kimataifa na inajaribu kujenga uhusiano wa kibiashara na nchi nyingi. Walakini, Taliban inajenga uhusiano juu ya masharti ya jamii ya ulimwengu, ambapo mfumo muovu wa ubepari, uliovumbuliwa na mwanadamu, unatawala. Uhalisia unaonyesha kuwa mfumo wa kibepari haujaleta manufaa yoyote kwa watu wowote duniani, kwani unalenga kuwakoloni watu na kupora maliasili zao.

Je, hadi lini nchi za Asia ya Kati na Afghanistan zitaendelea kubaki kwenye rehema ya Urusi kwa upande mmoja na mfumo wa kibepari wa Marekani kwa upande mwingine? Je, sio wakati sasa kwa Waislamu wa Asia ya Kati kutambua kwamba sababu ya udhaifu na umasikini wetu ni ukosefu wa umoja na dola? Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume inajumuisha usalama, utajiri na uhuru wa kweli wa nchi, watumishi wake na utajiri wake. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu