Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mabinti wa Ummah Wanauawa mbele ya Macho Huku Ulimwengu Unasikiliza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakati makumi ya maelfu ya raia wa Gaza wakikimbilia kusini, kutafuta usalama kwenye mpaka wa Rafah na Misri, hadithi moja ya jaribio la kutoroka inadhihirika: ile ya Hind Rajab mwenye umri wa miaka 6. Alikuwa njiani na wanafamilia wengine kukutana na mama yake wakati gari la Kia walilokuwa wakisafiria liliposhambuliwa na Majeshi ya umbile la Kiyahudi, na familia zote zilizokuwa kwenye gari hilo ziliuawa. Alikuwa ndiye pekee aliyeokoka. Alikuwa na akili ya kutumia simu ya rununu kuomba msaada, na gari la Hilali Nyekundu lililojaribu kumuokoa liliharibiwa kabisa, na kuua wahudumu wote wa afya. Ulimwengu ulijua kwa siku mbili mahali alipokuwa ameketi pamoja na maiti, lakini hakuna mtu aliyemwokoa. Alipatikana akiwa amekufa baada ya siku kadhaa, na simu yake ya mwisho iliisha kwa milio ya risasi.

Maoni:

Mamake Hind, Wissam, alihojiwa. Alikuwa akisubiri katika hospitali moja kupata habari za bintiye. Alikuwa ameshika kibegi kidogo cha waridi huku Hind akifanya mazoezi ya mwandiko wake. Anaripotiwa kusema,

"Kwa kila mtu ambaye alisikia sauti yangu na sauti ya kuomba msaada ya binti yangu, lakini hakumwokoa, nitawahoji mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama," aliiambia BBC. "Netanyahu, Biden, na wale wote walioshirikiana dhidi yetu, dhidi ya Gaza na watu wake, ninawaombea dhidi yao kutoka ndani ya moyo wangu. Je! ni kina mama wangapi zaidi ambao munangojea wahisi uchungu huu? Je, munataka watoto wangapi zaidi wauawe?" alisema.

Uhalisia wa kuhuzunisha ni kwamba binti wa Ummah huu alishambuliwa, alinusurika na alikuwa na akili ya kutumia simu kuomba msaada na bado alipuuzwa ni jambo lisilofikirika!

Wakati mwanamke mmoja wa Kiislamu aliposhambuliwa na Mayahudi katika zama za Khalifa Mutasem, alituma jeshi zima kwenda kunusuru heshima yake, ilhali tunalo kundi zima la viongozi wa Kiislamu wanaoyazuia majeshi kutokana na wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu (swt). Hakika hao ni wahalifu sako kwa bako na wauaji. Hatuwezi kamwe kulikubali hili kama jambo la kawaida kwani miezi 4 imepita huku Ramadhan inakaribia lazima tutafakari juu ya hili katika mwezi wa ushindi. Tuna wasaliti na watumwa wa nchi za Magharibi kama viongozi, na mauaji ya Waislamu walionaswa kwenye kona ya Rafah yanaongezeka tu kwa njaa kwani njia ya kifo cha polepole inafanyika moja kwa moja kwenye milisho yetu ya habari za rununu. Ni lazima tuendeleze wito si wa mihemko na machozi, bali wa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyokidhia ili kuwakomboa watoto wetu kutokana na mateso ambayo si yao kuyabeba.

[أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ أَإِلَٰهٌ مَعَ اللَّهِ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ]

“Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia!” [An-Naml: 62]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu