- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Wanasiasa wa Denmark Wanawaweka Waislamu chini ya Tuhuma za Kimfumo na Kuwataka Wawe Wamagharibi
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 5 Aprili, msemaji wa Social Democrat wa uhamiaji, Frederik Vad, alitangaza mambo muhimu kwa sera za sasa za uhamiaji na uwiano. Hasa zaidi kwamba ajira, elimu, lugha na rekodi safi za uhalifu, hazitoshi kwa wahamiaji na raia wenye asili ya wahamiaji, ikiwa hawafuati maadili ya kisekul, na hivyo eti watafanya kazi ya kuhujumu jamii ya Denmark kutoka kwa ndani. Hotuba yake katika Bunge la Denmark imezua mijadala, na kukashifiwa na wanachama na mameya wa Chama chenyewe cha Social Democrat, huku mawaziri kadhaa wakiunga mkono hotuba hiyo kwa usaidizi wa ziada.
Maoni:
Serikali ya Denmark inawatilia shaka raia wa Kiislamu watiifu kwa sheria, wanapofuata maadili ya Kiislamu. Serikali ya Denmark inadai kwamba hata kama vigezo muhimu vya uraia mwema, kwa ufafanuzi wao wenyewe wa uwiano, vitazingatiwa, Muislamu aliyebeba maadili ya Kiislamu ni tishio linalowezekana kwa jamii ya Denmark.
Isitoshe, wanasiasa wa Denmark wanawataka Waislamu kwamba kile wanachokiita “uoanishaji maadili” ambayo ina maana kwamba Waislamu wanapaswa kuwa wamagharibi katika maadili waliyonayo ili kuepusha kushukiwa na kuonekana kuwa wahalifu.
Tuhuma hii ya kimfumo na uoga wa serikali ya Denmark inafuatia miongo kadhaa ya kutisha wananchi wa Denmark dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wanalenga kuzusha hofu na wasiwasi dhidi ya Waislamu hadharani, ambapo Muislamu yeyote anatazamwa kama muovu na mlaji njama.
Hata kama Waislamu watachangia kwa jamii kwa kazi zao tukufu au viwango vya juu vya elimu, wanawekwa chini ya shaka ikiwa hawafuati maadili huria ya kisekula. Iwapo Waislamu wataunga mkono na kutoa sauti ya kutaka kukombolewa Palestina na kusambaratishwa uvamizi wa Kizayuni, basi wanatazamwa kama ni wahalifu, na matamshi hayo yanakuja katika mazingira ambayo watu wengi wa Denmark, sambamba na Wamagharibi wengine, wanaziwajibisha serikali za Magharibi kwa kushiriki kwao katika mauaji ya halaiki nchini Palestina na uungaji mkono wao wa mara kwa mara kwa umbile la Kizayuni.
Vitisho vya kweli kwa jamii na mahusiano kati ya wananchi ni wanasiasa hawa wenye kauli na sera zao za chuki dhidi ya Uislamu.
Yale yanayoitwa maadili yao angavu yanazorota na kufichuka mchana kweupe kama udanganyifu.
Wakati wanasiasa hawa kwa kejeli na kinafiki wanataka kulazimisha kulisha kwa nguvu maadili ya kisekula kwa Waislamu, Wamagharibi wanautazama Uislamu na kusilimu kama matokeo ya mijadala ya kifikra na hoja zenye lengo, wanapokutana na hoja zenye kusadikisha za Uislamu. Hoja, fikra na ufafanuzi, ni mambo ambayo serikali ya Denmark haina uwezo kabisa wa kuyawasilisha kwa Waislamu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorzcyk