- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuwang'oa Makamanda Walio Nyuma ya Mzozo nchini Sudan ndio Njia Pekee ya Kukomesha Vita vya Kipuuzi, vya Uharibifu Huko!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Takriban watu 150, wakiwemo watoto 35, wanahofiwa kufariki katika mauaji katika kijiji kimoja katikati mwa Sudan yanayolaumiwa juu ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), kundi la wanamgambo linalopigana na jeshi. (BBC)
Maoni:
Zaidi ya mwaka mmoja umepita sasa tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, kati ya vikosi vya jeshi, vikiongozwa na Burhan aliye maarufu, na Vikosi vya Msaada wa Haraka, vinavyoongozwa na Dagalo anayelaaniwa. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha uharibifu mkubwa. Vimesababisha hasara ya maisha ya maelfu ya raia na wanajeshi Waislamu. Vimesababisha mamilioni ya watu kuhama kutoka ardhi zao. Vimesababisha uchochezi wa fitna za kikabila za Ujahiliya wa kabla ya Uislamu ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliziweka chini ya miguu ya watukufu wawili, Umar bin Al-Khattab (ra) na Hamza ibn Abdul-Muttalib (ra) walipoongoza msafara mmoja wa Maswahaba (ra) kutoka katika makabila mbalimbali.
Maafa haya ya kutisha na uhalifu wa kutisha ulioikumba Sudan ni matokeo ya kupigania madaraka, kama wanavyodai. Ni kati ya pande mbili za viongozi wa vikosi vya kijeshi nchini. Walakini, kama hii ingekuwa kweli, aina ya mzozo nchini ingekuwa tofauti. Ingekuwa msingi wa unyongaji na mauaji kati ya pande hizo mbili. Yaani Al-Burhan, kwa mfano, angemuua Dagalo mwaka jana alipomkamata, au Dagalo angemtuma mmoja wa mamluki wake kumuua Al-Burhan. Hata hivyo, matokeo halisi ni kwamba watu hawa wawili waoga wanatumia uwezo wa kijeshi wa nchi, kutoka pande zote mbili, kuharibu nchi. Wanatumia uwezo wa Sudan dhidi yake, kwa kuigawanya kwake, na mauaji na uhamisho wa watu wake. Wamefanya hivyo hadi hali ya nchi ikawa haina tofauti na ile ya Ukanda wa Gaza, uliolengwa na nguvu za uovu wa kimataifa, zikiongozwa na Mayahudi ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia.
Kwa kisingizio cha kumaliza upinzani, dola ya Mayahudi iliharibu kabisa Ukanda wa Gaza. Kadhalika, kwa upande wa Sudan, kwa kisingizio cha kupigania madaraka, na kuegemea upande mmoja wa kisiasa dhidi ya mwingine, Sudan iliharibiwa. Mapigano, majeshi yanayoshindana nchini Sudan yalisababisha uharibifu mkubwa kwa Sudan, kama vile Mayahudi walivyoharibu Gaza. Watu hawa wawili waaoga na Netanyahu, ambaye walikuwa wamehalalisha mahusiano naye, wote ni sawa. Wote walitoa madai yale yale ya uwongo, huku lengo la uovu wao likiwa ni jambo jengine kabisa, ambalo ni kuharibu nchi na kuua watu. Hii ni kwa sababu tu wao ni vibaraka mikononi mwa viongozi wahalifu wa ulimwengu, wanaopanga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu mchana na usiku.
Maafisa wanyoofu katika jeshi la Sudan, na vikosi vyote vya kijeshi vilivyomo ndani yake, lazima wawalenge Al-Burhan na Dagalo, wawang'oa wote wawili na wasaidizi wao. Ni lazima wawabadilishe kwa uongozi wa dhati wa kisiasa nchini. Hii ni kwa kupitia maafisa hao wanyoofu katika jeshi la Sudan kutoa Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah pekee ndiyo itakayowaunganisha Waislamu wa Sudan. Zaidi ya hayo, chini ya bendera ya Khilafah, nchi za Mto Nile, ambazo ni zaidi ya nchi kumi, zitaungana. Hivyo basi, Khilafah Rashida itakayoibuka hapo itakuwa ni kiini chenye nguvu cha dola kubwa ya Kiislamu duniani. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]
“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [Surah As-Saffat 37:61].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan