Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mirziyoyev Afufua “orodha nyeusi” za Waislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mwanablogu mashuhuri wa Uzbekistan, Mirrahmat Muminov, alitangaza kwamba ana habari kuhusu kuanzishwa kwa udhibiti kamili na ufuatiliaji wa waumini sugu wa misikiti nchini. Aliripoti haya kwenye ukurasa wake wa Facebook:

“Kamati ya Masuala ya Kidini na Bodi ya Waislamu ya Uzbekistan, pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani, waliagizwa kuandaa orodha za waumini sugu wa kudumu wa misikiti. Uamuzi huu unahusiana na kukua kwa itikadi kali za kidini na umaarufu wa fikra za kidini miongoni mwa vijana. Lengo ni kuzuia uingizaji itikadi kali kwao. Maimamu pia wanaagizwa kuwaelekeza vijana, kuwaepusha na misimamo mikali, na kuweka orodha za waumini sugu. Misikiti inahitajika kutoa data kutoka kwa kamera za uchunguzi kwa vyombo vya utekelezaji sheria.

Maimamu wa misikiti pia wana jukumu la kuwashauri vijana wenye ndevu, kukuza fikra ya uvumilivu kidini wa madhehebu yao, na kuonya kuhusu hali ya mizozo ya kidini duniani. Maimamu lazima watengeneze orodha tofauti za vijana wakorofi wanaowadharau viongozi wa misikiti au kuwasema vibaya.

Aidha, misikiti yote imeagizwa kusajili kamera zao za CCTV na kukabidhi rekodi hizo kwa vyombo vya sheria. Maimamu wamekumbushwa kwamba ingawa wanapenda kazi zao, kutotii mamlaka kutasababisha adhabu, karipio na matokeo mengine makubwa.”

Maoni:

Kumbuka kwamba “orodha nyeusi” ya wanaharakati wa kidini ilianzishwa na Rais wa zamani wa Uzbekistan Islam Karimov kama sehemu ya vita vya kipekee alivyopigana ili kuzuia mwamko wa kidini na kisiasa nchini. Baada ya kuingia madarakani mnamo 2017, Mirziyoyev alifuta rasmi “orodha nyeusi” za watu wanaoshukiwa na shughuli za Kiislamu au waliohukumiwa kwazo, kisha akatangaza kwa dhati kuondolewa kwa watu elfu 16 kwenye orodha hiyo. Na mnamo 2019, mwakilishi wa Sekretarieti ya Kamishna wa Haki za Kibinadamu, Saidbek Azimov, alisema kwamba Uzbekistan haihifadhi tena rekodi kama hizo za wanaharakati wa kidini na hakuna “orodha nyeusi”.

Ikiwa orodha kama hizo za wahudhuriaji wa msikiti zitakusanywa na kufuatiliwa, kitendo hiki hakitamaanisha tu kurudi kwa siku za nyuma, bali ongezeko kubwa la shinikizo kwa watu, hata ikilinganishwa na zama za Karimov. Ni dhahiri kuwa lengo la hatua hizo ni kuunda mazingira ya hofu miongoni mwa watu ili kupunguza uhudhuriaji misikitini kwa jumla na hivyo kupunguza kasi ya watu kuregea katika kujitambua kwa Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu