Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mvunjifu na Mdhamini Pamoja: Serikali Yalenga Nini?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Recep Tayyip Erdogan, simu ya Mwenyekiti wa MHP Bahceli kuhusu Rais, “Ndugu zangu wapendwa Wakurdi, tunatarajia mshike mkono huu kwa dhati, ushikeni kwa nguvu. Tunataka muondoke kwenye njia ya wale ambao ni wafuasi wa Mazayuni wa Israel, vibaraka wa ubeberu, wachonganishi wa maadui wa Uturuki.” Erdogan pia alimshukuru Mwenyekiti wa CHP Özgür Özel kwa kuunga mkono mradi wa udugu, na kisha akasema, “Kwa nini unasumbuliwa na hili wakati jiografia yetu imegeuka kuwa duara la moto, wakati wanachama wa shirika la kigaidi wanaharibu Esenyurt? Hutasumbuliwa na hili. Kinyume chake, utaunga mkono utawala uliopo sasa hapa” alisema. (30.10.2024 TRT News)


Maoni:

Erdogan alizungumza kwa mara ya kwanza baada ya mshirika wake wa muungano Devlet Bahceli kumwalika kiongozi wa shirika la kigaidi la PKK Abdullah Ocalan kwenye Bunge ili kulitaka shirika hilo kuweka silaha zake chini. Katika hotuba yake, alitumia hotuba nzuri dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa huku akijaribu kuwazuia wapiga kura wa Kikurdi wasishiriki katika mapambano. Devlet Bahceli, ambaye alichukua nafasi ya msemaji wa mchakato huo mpya, alialikwa makhsusi na Erdogan, kwa sababu ikiwa mchakato huo hautapata jibu kwa misingi ya kijamii na kuathiriwa, Bahçeli atatangazwa kuwa na hatia. Erdogan ametoa ujumbe wa umiliki kwa kuchukua uongozi wa mapema dhidi ya hili. Siku moja baada ya hotuba ya Erdogan, meya wa CHP wa Esenyurt, wilaya kubwa zaidi ya Istanbul na yenye wakaazi wengi wa Kikurdi, alifutwa kazi na mdhamini akateuliwa badala yake. Tunaweza kutathmini ufunguzi mpya wa serikali ya Wakurdi, au Mpango wa Uturuki Usio na Ugaidi katika maneno ya Devlet Bahceli, kama ifuatavyo ndani ya mfumo wa taarifa za Erdogan na maendeleo yanayofuata: Hebu tukumbuke!

1. Mrengo tawala ulitoa wito wa kuwepo kwa maelewano mapya ya kijamii kupitia Ocalan ili kuhakikisha amani ya ndani na kuimarisha mrengo wa ndani, kwa kutumia kisingizio kwamba vitisho vya nje dhidi ya Uturuki vimeongezeka.

2. Ili makubaliano haya yatimie, yanalenga kubadilisha katiba na Rais Erdogan kuchaguliwa tena kuwa rais. Kwa sababu hii, imepangwa kutenganisha Chama cha DEM, ambacho ni chama kikuu, kutoka kwa CHP, na kufuta ushawishi wa Kandil kwenye Chama cha DEM kupitia Ocalan na kuifanya sehemu ya makubaliano ya kijamii.

3. Kutokana na matukio haya yanayolenga kujifilisi, Kandil au PKK walianzisha mashambulizi ya kigaidi dhidi ya TAI, ambayo ni ujumbe kwa serikali na Chama cha DEM, ili kuwafanya wahisi kuwa mchakato ambao hawaukubali, hauwezi kufanyika bila wao kwenye meza, kwamba Abdullah Ocalan hana tena ushawishi wowote kwenye shirika, kwamba mazungumzo na mchakato ufanyike pamoja nao.

4. Baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya TAI, Rais Erdogan alisema kwamba shambulizi hili liliimarisha zaidi dhamira yao ya kufikia maridhiano ya kijamii, na kwamba hawakuwaita wapiganaji wa kigaidi huko Qandil, msemaji wa wito huo walikuwa watu wa Kikurdi.

5. Meya wa Jiji la Istanbul Ekrem Imamoglu, kwa hotuba yake mnamo Oktoba 29, alimlenga Rais Erdogan na Mfumo wa Serikali wa Urais na akatoa hotuba kana kwamba yeye ndiye mwenyekiti wa CHP na mgombea urais, na sio meya.

6. Baada ya matukio haya, Meya wa Esenyurt wa CHP alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa ugaidi na mdhamini akateuliwa badala yake. Inaonekana kuwa serikali inalenga yafuatayo kwa kutumia zana za kikatiba na wadhamini pamoja katika muktadha wa mchakato mpya wa Ujenzi:

- Wale ambao hawakubaliani na itifaki ya kijamii na kufanya siasa chini ya ushawishi wa Qandil hawatapewa fursa; ushawishi wa Qandil kwenye siasa utajaribiwa kuondolewa.

- Chama cha DEM kitafanywa kuwa sehemu ya itifaki ya kijamii na jaribio litafanywa la kujitenga na CHP na kutenga CHP katika siasa.

- Ekrem Imamoglu ataondolewa kwenye siasa ili kuzuia kugombea kwake urais na kujaribu kuleta mgogoro ndani ya CHP.

- Kwa kuhakikisha uungwaji mkono wa Chama cha DEM, jaribio litafanywa kuweka njia kwa ajili ya marekebisho ya katiba na kuchaguliwa tena kwa Rais Erdogan.

Bila shaka, haya yote sio kuanzisha udugu wa Waislamu wa Kituruki na wa Kikurdi. Hii ni kufinika tu mambo kwa sababu wale ambao hawana chochote isipokuwa usekula, utaifa na maslahi binafsi katika ajenda zao, ambao hawaangalii siasa kwa mtazamo wa “La ilaha illallah Muhammadun Rasulullah”, hawawezi kuunganisha Ummah wala kutatua matatizo ya Uturuki. Iwe ni serikali au upinzani, miundo kama hii ya kisiasa haiwezi kukwepa kuwa wafungwa wa ukoloni, kama vile mtazamo wao wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu na Kimbunga cha Al-Aqsa kinachoendelea, wanatumikia maslahi ya makafiri wakoloni ili tu kudumisha viti vyao. Madhumuni yao pekee ni kuzuia ummah wa Kiislamu kuelekea katika Khilafah na kujaribu kuzalisha miungano bandia, dhidi ya umoja halisi wa Khilafah. Matukio ya hivi majuzi katika siasa za ndani za Uturuki katika mkorogo wa mgogoro wa kiuchumi na mporomoko wa kijamii sio chochote isipokuwa hili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yildirim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu