Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mashirika ya Kimataifa Hayapaswi Kulaumiwa kwa Afya ya Ulimwengu

Habari:

Trump alisema katika mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari mnamo 10 Aprili 2020 kuwa, “Kwa kipindi cha miaka yote, miaka mingi, tumekuwa tukiwalipa kwa kiasi cha dolari milioni 300 hata 500, na hata zaidi, kwa mwaka. China imekuwa akiwalipa chini ya 40 kwa miaka yote hiyo. Hivyo tunawalipa mara 10 zaidi ya China. Na wao, wangali wamepagawishwa mno na China.”

Maoni:

Shambulizi la Trump kwa juhudi za Shirika la Afya Duniani (WHO) za kukabiliana na janga hili limechipuza kutokana na hamu ya kutaka kujipurukusha kutokana na kushinda kwake yeye mwenyewe katika kukabiliana na janga hili, na inaonyesha dosari halisi katika muundo na utendakazi wa mashirika ya kimataifa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa  na inaungwa mkono kwa kiasi fulani kwa makosa halisi yanayo fanywa na Shirika hilo la Afya Duniani.

Mnamo 14 Januari Shirika la Afya duniani WHO liliandika kwenye mtandao wake wa tweeter kwamba “Uchunguzi wa awali uliofanywa na mamlaka za China umekuta kwamba hakuna ushahidi wa wazi wa maambukizi kati ya mtu na mtu ya virusi vya korona vilivyo gunduliwa jijini Wuhan, China”, lakini madaktari wa China walikuwa wanajaribu kuionya dunia mapema kabisa tangu Disemba kwamba maambukizi kati mtu na mtu yalikuwa yakitokea. Kuongezea mkanganyiko huu kutoka Shirika la Afya, WHO ilichelewa sana kutangaza kuwepo kwa janga la virusi na hili likazipa serikali za kitaifa uhalali wa kirongo wa kuchelewa kwao kuchukua hatua.

WHO inazingatiwa kwa kiasi kikubwa kuwa ni taasisi huru, lakini, bila shaka, Trump yupo sahihi kwamba shirika hilo limeundwa na watu kutoka nchi mbalimbali kote ulimwenguni na ajenda tofauti tofauti lazima ziangaziwe katika utendakazi wa shirika hilo. Njia kubwa inayo angazia hili, lakini, sio maamuzi yanayo unga mkono ajenda maalumu, bali ni kupitia maamuzi na matangazo yanayo penyezwa kupitia ngazi nyingi za msururu mrefu wa hatua katika jaribio la kutaka kuepukana na lawama za kidiplomasia mbele ya dola zote wanachama. Matokeo ni kwamba madai ya China lazima yayapiku madai ya Taiwan, kwani Taiwan anatambuliwa na wanachama kumi na nne pekee kati ya wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa, na kauli rasmi za serikali ya China hutangulia (kipaumbele) juu ya madai kinzani yanayo tolewa na raia binafsi wa China. Fauka ya hayo, msururu mrefu wa hatua huhakikisha utangazaji wa polepole na wa uangalifu baada ya kujenga itifaki ya kindani ili kuepusha makosa. Kwa kuzingatia yote haya, WHO ni shirika la kibinaadamu kiasi ambacho ushawishi wa baadhi ya dola unaweza kuwa mkubwa kuliko dola nyengine kulingana na ukubwa wa dola hizi na kiwango cha uwekezaji wao. Ile fahamu ya shirika la kimataifa au sheria ya kimataifa ina dosari kwani dola pekee ndizo zinazo weza kuwa chimbuko la sheria. Dola hukubali tu kufanya kazi ndani ya hiyo inao itwa mipangilio ya kimataifa kwa mujibu wa nguvu zao na maamuzi yao juu ya iwapo mipangilio hii itatumikia maslahi yao ya muda mrefu kwa kiasi ambacho zitayatoa kafara baadhi ya maslahi ya muda mfupi.

Kwa kujua mapungufu ya kidhana na kivitendo ya WHO kama chombo cha kimataifa, uongozi wowote ulio na ikhlasi unapaswa uunde vitendo vyake juu ya msingi kuwa ni serikali za kitaifa ndio zenye kuwajibika dhidi ya afya za watu wake, na wala sio WHO. Trump, hivyo basi, anakosea kulilaumu shirika la WHO kutokana na ukweli uliopo kwamba Amerika sasa iko katikati ya janga, ambalo ukubwa wake halisi ndani ya mipaka yake unazidi uwezo wao wa kulipima.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Abdullah Robin

#Covid19    #Korona     كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 28 Aprili 2020 10:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu