Jumapili, 05 Rajab 1446 | 2025/01/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa Vya Habari 11/07/2020

Vichwa vya habari:

Iran Yanyamaza Kimya Huku Amerika Ikishambulia Vituo vya Kinyuklia vya Iran

Iran Yaruhusu Uwepo wa Majeshi ya China katika Ardhi Yake

Uturuki Yafikia Kikomo Chake Ilichowekewa Nchini Libya

Maelezo:

Iran Yanyamaza Kimya Huku Amerika Ikishambulia Vituo vya Kinyuklia vya Iran

Kulingana na gazeti la New York Times:

Wakati ambapo kituo cha kuendeleza uzalishaji wa nyuklia, kimesambaratishwa baada ya mlipuko ambao unasadikika kutekelezwa na Israel, mzozo wa muda mrefu baina ya Amerika na Tehran unaonekana kupamba moto na kuelekea katika awamu hatari ambayo inaweza kuathiri wakati wa kampeni ya uchaguzi wa uraisi wa Amerika.

Picha mpya za satilaiti za kituo hicho lilicho shambuliwa cha Natanz zinaonyesha uharibifu mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa imeripotiwa awali wiki iliopita.  Maafisa wawili wa kijasusi waliopata habari mpya ya tathmini ya uharibifu ya kiwanda hicho cha Natanz ilio kusanywa hivi karibuni na Amerika na Israel, inasema huenda ikawachukua Wairan muda wa hadi miaka miwili kuuregea mradi wao wa kinyuklia mahali ulipokuwa awali kabla ya mlipuko huo.  Uchunguzi wakuaminika unakadiria kuwa itachukua mwaka au zaidi kwa Iran kuregesha uwezo wake wa uzalishaji wa centrifuge.

Mlipuko mwengine mkubwa ulipiga Iran mapema Ijumaa asubuhi na kusababisha mwangaza mkubwa katika eneo la kitajiri la Tehran.  Bado tukio hilo halijatolewa ufafanuzi lakini lilionekana kutokea upande wa kambi ya mabomu ya masafa marefu (missile base). Ikiwa itasadikika kuwa ni shambulio jingine, litawatikisa Wairan zaidi kwa kuwaonyesha kwa mara nyingine kuwa hata vituo vya Nyuklia na vituo vya mabomu ya masafa marefu vyenye ulinzi imara vimesha ingiliwa.

Iran inatawaliwa na makundi mawili,'kundi lenye msimamo wa kati na kati' na 'lenye msimamo mkali' lakini makundi yote mawili yanashiriki katika mipango miovu ya Amerika. Pindi Amerika ikihitaji huduma ya Iran katika eneo hilo inaruhusu kupanuka kwa kundi lenye msimamo mkali. Lakini wakati America haihitaji tena utumishi wake, inawakandamiza wenye msimamo mkali na kuwaruhusu wenye msimamo wa kati na kati kuwa na ushawishi mkubwa.

Iran Yaruhusu Uwepo wa Majeshi ya China katika Ardhi Yake

Wakati huo huo Wairan wenye msimamo mkali wamefichua mpango wa serikali inayo dhibitiwa na Wairan wenye msimamo wa kati na kati, mpango ambao unaruhusu uwepo wa jeshi la China kwenye ardhi ya Iran. Kwa mujibu waal-Monitor :

"Hamna la kuficha kuhusu mpango huo. Kila hatua imekuwa ipo wazi na tutakapo maliza mkubaliano kila jambo tutaliweka hadharani". Waziri wa Mambo ya Nje, Mohammad Javad Zarif aliwaambia watunga sheria wiki iliyopita alipobanwa kutoa ufafanizi juu ya makubaliano yenye utata ya ushirikiano wa miaka 25 na China. "Nukta muhimu ambayo yafaa kutiwa maanani katika sera yetu ya mambo ya nje ni kuhama na kuwa Taifa lenye nguvu duniani" Zarif alitoa hoja hiyo akijitetea kuhusiana na makubaliano hayo.

Kwa mujibu wa maafisa  wa Iran, waraka unaofahamika kama Ushirikiano wa Kamili wa Kimkakati baina ya China na Iran,  ulitiwa saini na serikali ya Hassan Rouhani mwezi wa Juni. Yaliyomo kwenye waraka huo yamesababisha mjadala mkubwa na unatiliwa shaka. Wakiti waraka huo ulipokuwa unafanyiwa kazi kwa zaidi ya miaka mitano, wengi hawakuutia maanani mpaka pale baadhi ya vyombo vya habari vilianza kuripoti kuhusu baadhi ya vipengele muhimu ndani ya waraka huo.

Mnamo Septemba, 2019 mwanauchumi wa Petroli, akitegemea chanzo cha habari ambacho hakikutajwa ndani ya wizara ya mafuta ya Iran, alitoa ufafanuzi wa kina wa uwekezaji wa China wa dola billioni 400 chini ya mpango wa sekta ya mafuta, gesi na uchukuzi za Iran, huku Beijing ikinufaika na punguzo la asilimia 32% wakinunua mafuta ambayo bado hayajasafishwa pamoja na pumziko la miaka miwili kwenye malipo.  Taarifa nyingine zina sema kwamba waraka huo unaipa serikali ya China nafasi muhimu kwenye miradi mingine kama vile usalama, miundumbinu ya mawasiliano, afya na utalii.

Kile haswa kilicho wakasirisha wapinzani nchini humo ni madai kwamba mpango huo utaipa China ruhusa ya kuleta vikosi vyake takriban 5000 ili kulinda maslahi yake na pia muhimu zaidi kulinda visiwa vya kusini mwa Iran ambavyo pia in muhimu kwa biashara.

Aliyekuwa Raisi wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kufichua mpango huo kwa ummah. Mahmoud Ahmadinejad aliikosoa vikali serikali ya Rouhani  kwa  "kutia saini mkataba huo kwa siri" na dola ya kigeni.  makubaliano au mpango wowote kama huu ambao upo dhidi ya matakwa ya watu na maslahi ya taifa unakosa uhalali na hautotambuliwa na taifa la Iran" alionya huku akisema kwamba pia mikataba hiyo imekwenda kinyume na misingi imara ya mapinduzi ya Kiislamu ambayo yalitarajiwa "kutoficha chochote kwa taifa.”

Raisi wa zamaniAhmadinej ad katika kuishambulia serikali, akumbuke kwamba naye pia alishirikiana waziwazi na dola ya kigeni, Amerika, katika uvamizi wake katili wa Afghanistan na Iraq. Serikali ya Iran inafanya kosa ambalo serikali zote za Waislamu zimekuwa zikilifanya, kosa lenyewe likiwa ni kutaka msaada kwa wabeberu makafiri wa kigeni.  Mwenyezi Mungu anasema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّـهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا)

"Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?" [an-Nisaa: 144]

Uturuki Yafikia Kikomo Chake Ilichowekewa Nchini Libya

Amerika inarudia tena mpango ule ule nchini Libya walioutumia nchini Syria, ambao ni kuwaweka watumishi wake pande zote mbili za mzozo kwa malengo ya kutengeneza makaazi baina yao jambo ambalo linaendana na maslahi ya Amerika, wakati huo hairuhusu mtumishi yeyote kuidhibiti hali kikamilifu. Uchambuzi mdogo wa Uturuki kurudi nyuma wiki iliopita unatoa ishara ni kwa kiasi gani Amerika inairuhusu Uturuki kuendelea ndani ya Libya. Kwa mujibu wa tovuti ya moderndiplomacy.eu:

Msururu wa mafanikio ya serikali inayoungwa mkono na Uturuki nchini Libya (GNA) ghafla ulilisita mnamo Julai tarehe 4 wakati ambao uwanja wa ndege Al Watiya ambao hivi karibuni ulidhibitiwa na GNA, ulishambuliwa na ndege za kivita zisizo fahamika.  Jeshi ambalo ni tiifu kwa GNA liliingia uwanja wa ndege wa Al-Watiya wiki chache zilizo pita baada ya mashambulizi makali kwa ushirikiano na ndege zisizo na rubani za Uturuki.  Huko nyuma wapiganaji wa GNA walijipiga picha na chombo cha kivita kwa jina Pantsir S-1 kilicho achwa na Jeshi la Kitaifa la Libya (LNA) Libya. Badala ya Pantsirs vilivyotengezwa Urusi mifumo ya Kituruki ya MIM-23 HAWK iliwekwa katika kambi.

Picha mpya za Al Watia kutoka katika satilaiti zinaonyesha wazi kuwa vyombo hivyo vya kivita vilikuwa na hitilafu au vimeharibika kabisa kutokana na shambulizi hilo. Matokeo haya bila shaka ni pigo kubwa kwa fahari ya uongozi wa Uturuki kwa sababu linajiri muda mchache tu baada ya waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar kutamatisha ziara yake jijini Tripoli.  …

Uturuki na GNA hazikuweka wazi kiwango cha majeruhi waliopatikana kwenye shambulizi, lakini kiuhalisia umuhimu wake ni mdogo. Jambo la maana zaidi ni kinaya kilicho nyuma ya shambulizi lililoisukuma Uturuki kuwa na Mipango ya kuyateka maeneo muhimu ya kimkakati ya bandari ya Sirte na uwanja wa ndege wa Jufra. Mzozo wa Libya unategemea uwezo wa uongozi wa Uturuki  kuelewa ujumbe huu.

Ummah wa Kiislamu hakika utaijua amani, haki na maendeleo pale tu Waislamu watakapoling'oa tabaka la watawala vibaraka wanaotumikia maslahi ya wabeberu makafiri wa kigeni na kutabikisha nidhamu zao za sheria na utawala katika ardhi za Waislamu. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ulimwengu karibuni utashuhudia kuregea kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw), itakayoziunganisha ardhi za Waislamu, ikitabikisha Uislamu na kuubeba ujumbe wake ulimwengu mzima.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 01 Septemba 2020 11:12

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu