Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 20/02/2021

Katika Moja ya Hotuba Zake Kubwa za Kimataifa, Biden Aonya Kuhusu Urusi

Wiki hii, Rais wa Amerika Joe Biden, ameshiriki vikubwa, akitumia hutuba yake katika mkutano wa mwaka wa ulinzi uliofanyika Munich kuonya dhidi ya Urusi na China, huku akiapa Amerika kuendelea kujizatiti na kushirikiana na washirika wake wa Ulaya. Wakati akiishutuma China “kwa matumizi mabaya ya uchumi na matumizi mabaya ya nguvu”, Biden alilazimika kuijumuisha na Urusi,  akimshutumu Rais Putin kwa kujaribu  “kudharau na kutishia hali za watu”  badala ya kufanya makubaliano “pamoja na kuungana kwa karibu na jumuia ya transatlantic”. Wakati huo huo Biden ametambua taharuki chini ya mtangulizi wake, Rais Trump, na kujikita kuboresha uhusiano na Ulaya, akisema, “Najua miaka michache iliyopita imetetelesha uhusiano wetu. Lakini Amerika imejizatiti kuamiliana upya na Ulaya. Kushauriana na nanyi. Kurudisha upya nafasi yetu ya uaminifu na uongozi.

Kama tulivyojadili mara nyingi hapo mwanzo katika mtazamo huu, sio mpango jumla utakaobadili utawala kutoka utawala lakini kujaribu kufanyia kazi mipango hiyo. Trump aliweka wazi hasira zake dhidi ya Ujerumani kwa uhusiano wake na Urusi, haswa kuhusu ujenzi wa bomba la Nord Stream 2 katika ya nchi hizo mbili, ikifungua njia kwa Urusi kusambaza gesi kwa nchi masikini za Ulaya. Mbali na mazungumzo kuhusu kusaidiana na kushirikina, utawala wa Biden kama utawala uliopita wote wanapinga ujenzi wa bomba hilo; ingawa imeamuliwa kujiuzia katika kuichukulia hatua Ujerumani, mnamo siku ya Ijumaa ilitangaza vikwazo dhidi ya meli ya Urusi iliyoshiriki katika ujenzi huo.

Nafasi ya Amerika kuhusu urusi ni sura mbili lakini zikiwa na uhusiano mkubwa. Amerika yenyewe imefikiria kuomba usaidizi kutoka Urusi, kwa mfano Syria katika kuvunja mapinduzi ya kumuondoa Assad, na Libya, kwa ajili ya kumsaidia kibaraka wa Amerika Khalifa Haftar. Lakini Amerika haihitaji nchi yoyote kunufaika na Urusi. Zaidi ya hayo, Amerika inafanya kazi kuhakikisha uhasama baina ya dola kubwa, ili kutengeneza usawa wa kinguvu miongoni mwao. Hivyo Amerika inaihamasisha Urusi kuchukua hatua dhidi ya nchi za ulaya, wakati huo huo nchi za ulaya dhidi ya Urusi. Ulaya inafahamu hilo, na ndo maana zinafanya juhudi kuwa na uhusiano na Urusi, bila kujali uchokozi wa Urusi. Lakini utawala wa Urusi ni rahisi kutoeleweka na Amerika kwa sababu ya kupotea kisiasa kwa siasa za Urusi baada ya kuangaka kwa Umoja wa Kisoviet. Hivi leo, Urusi haiongozwi na wanasiasa bali wanachama wa zamani na shirika la kijasusi linalojulikana kama  siloviki, likimjumuisha Putin mwenyewe, ambaye ni alikuwa afisa wa ngazi ya kati wa KGB.

Ni muhimu juu Umma wa Kiislamu kuunda ufahamu mpana wa kisiasa, ambao hauwezekani bila ya kuwa na ufahamu mpana wa mambo ya kimataifa. Kisha itakuwa ni sahali kwa Umma kufahamu na kuwa na uwezo wa kuwaelewa wanasiasa wa ndani na viongozi ambao wanafahamu mgeuko wa kilimwengu na kuacha nafasi hiyo kuchukuliwa na urejeshaji wa dola ya Kiislamu ya  Khilafah kwa njia ya mtume (saw), hilo litaunganisha ardhi yote ya Waislamu, kukomboa ardhi zilizokwapuliwa, kurudisha mfumo wa maisha ya Kiislamu na kubeba ulinganizi wake katika dunia nzima. Dola ya Khilafah itaingia, katika mipaka yote hadi katika nchi kubwa, kwa kuzingatia, nguvu yake, nafasi yake, rasilimali na mfumo wake. Hivi sasa nchi kubwa zinapinga urejeshwaji wa dola ya Khilafah. Lakini kwa udharura wake, haraka watatizama nafasi zao na namna watakavyonufaika kwa kuijumuisha kwao Khilafah katika kufanya usawa mgeuko wa dola kubwa, upingaji umekuwa ni silaha katika mikono yao, na kwa kujiamini wameweka malengo yao, wakifaya uharibifu kwa kutumia nguvu yao ya kikafiri. Utawala wa Khilafah kwa muda huo lazima uwe macho kwa aina ya dola na kurudisha uimara wa hali na utulivu na upendo katika hali ya kimataifa.

Saudi Arabia, Iraq na Afghanistan

Mifano zaidi ya utofauti wa njia za Biden lakini kufanana kwa karibu kisera kunaweza kuonekana kupitia mahusiano yake na Saudi Arabia. Wiki hii, msemaji wa ikulu ya White house Jen Psaki alisema kwamba muelekeo wa mahusiano kati ya Rais Biden na utawala wa Saudi utakuwa katika mipaka ya mfalme Salman, tofauti na Trump aliyeshirikiana na mtoto wa mfalme Mohammad bin Salman, anayejulikana kama MBS. Yote kwa yote, waziri wa ulinzi wa Amerika Lloyd Austin alisuhubiana na MBS siku kadhaa baadaye ili  kufikisha taarifa ya uungaji mkono wa Amerika kwa ulinzi wa Saudi Arabia dhidi ya kushambuliwa na Mahouthi nchini Yemen na  “ukizingatia jukumu msingi la Saudi Arabia katika usalama wa kanda katika mashariki ya kati na umuhimu wa kushirikiana katika jukumu la ulinzi wa kanda na uimara” kulingana na taarifa kutoka idara ya ulinzi. Na hata hivyo kuna mabadiliko ya sera kwa kuzingatia miaka kadhaa ya vita vya Yemen, hii inawakilisha uimarishaji wa sera uliwekwa wakati wa Obama na chini Trump. Amerika imekuwa ikihamasisha vita vya Yemen katika pande zote ili kutengeneza mazingira ya kujiimarisha Yemen ili kuzalisha serikali itakayokubali kuwa chini ya Amerika, tofauti na miongo iliyopita serikali chini ya Ali Abdullah Saleh, ambaye alitoa kiapo chake kwa Uingereza na sio Amerika. Ilikuwa ni Uingereza, dola kuu iliyopita, ambayo iliongoza uangushwaji wa dola ya Khilafah ya kiuthmani miaka mia iliyopita, na ilikuwa ni Uingereza ambayo kwa muda ule ilinufaika sana, kwa kujiingiza kwake katika ulimwengu wa Kiislamu. Dola yenye nguvu kwa sasa Amerika, imezishikilia nchi zote katika ulimwengu wa Kiislamu lakini Uingereza imebaki na ushawishi katika baadhi ya nchi hizo kama inavyo fanya Ufaransa. Kwa hali yoyote, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hivi punde Umma wa Kiislamu utasimama na kuondoa vibaraka ambao wameapa kulinda maslahi ya makafiri katika ardhi za Waislamu.

Ingawa Trump, aliegemea katika kujijenga kindani zaidi, alikuwa na ghera ya kumaliza vita Afghanistan na Iraq,  alizuiliwa kufanya hivyo kwa kuiunda Amerika na kufanikiwa tu kupunguza wanajeshi 2,500 kutoka katika kila nchi hizo mbili, hakuwa amejizatiti kuondoa vikosi vyote vilivyopo Afghanistan kufikia mwezi wa tano mwaka 2021, kitu ambacho ni mbali na muda wake wa utawala. Hivi sasa Biden amejikita katika kuimarisha uwepo wa majeshi ya Amerika katika nchi zote mbili. Ameonekana kuanza hilo wiki hii ikiwa ni katika tangazo la Amerika yenye ushawishi mkubwa zaidi NATO uamuzi wa kuonyesha umuhimu wa kuongeza zaidi vikosi nchini  Iraq kutoka 500 hadi 4,000, wakati huo huo akiendelea kupeleke wanajeshi 9,600 Afghanistan. Amerika imeshaanza kuvunja ahadi ya Trump ya kuondoa wanajeshi Afghanistan, na Waziri wa Ulinzi wiki hii, alisema, kuwa Amerika “haiwezi kuchukua uamuzi wa kukurupuka au kupinga kujiondoa kutoka Afghanistan; hilo litaviweka vikosi vya NATO katika hatari, aliongezea “bado hakuna kilicho amuliwa kuhusiana na mustakbali wa vikosi vyetu”. Ingawa ni wazi kwamba Amerika haihitajii kujiingiza katika vita vya ‘milele’, ni kweli pia kwamba, Amerika haitaki kuacha nchi iliyoivamia ikijikusanya upya kuunda kambi za kijeshi. Vita vya Amerika Afghanistan na Iraq havikuwa rahisi kwa malengo ya sasa lakini ilikuwa ni kufanya kituo katika ulimwengu wa Kiislamu na kuunda eneo maalum dhidi ya Urusi na China. Kambi hizi zinafanikiwa sio tu kwa juhudi zake bali kwa usaidizi na ulinzi wa serikali vibaraka walizoziunda katika nchi hizi, zinazo ongozwa na  Kadhimi nchini Baghdad na  Ghani wa Kabul. Lakini baada ya kurejeshwa dola ya Kiisalmu ya Khilafah na kuwaondoa vibaraka hawa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itakuwa ni kazi nyepesi kwa vikosi vya makafiri kuondolewa katika ardhi ya Waislamu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu