Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 27/03/2021

Tume ya Kifaransa Yayataja Mauwaji ya Rwanda kama ‘Kufeli’

Baada ya miaka mingi ya tuhma dhidi ya serikali ya Ufaransa kwa dori yake katika mauwaji ya Rwanda ya 1994, ambayo inakadiriwa kuwa watu 800,000 waliuawa, tume rasmi ya kihistoria ya Kifaransa imekataa kwamba Ufaransa ilikuwa na ushiriki wowote wa moja kwa moja lakini ikajifunga kwa kuilaumu Ufaransa kwa kuunga mkono kwake uongozi wa Wahutu wa wakati huo dhidi ya waasi wa Kitutsi, ikiwatuhumu Wafaransa kwa "… kufungia macho maandalizi ya mauwaji ya halaiki na watu wenye msimamo mkali wa utawala huu". Kwa kweli, Francois Mitterrand, rais wa Ufaransa wakati huo, ameshakufa zamani.

Mauwaji hayo ya kutisha ya Rwanda ni dalili ya kuumiza ya ubeberu wa Magharibi na ushindani na uhasama kati ya dola za Magharibi. Nchi za zamani za kikoloni ambazo sasa zinaonekana huru ni kweli bado ziko chini ya udhibiti wa Magharibi, na bado ni chombo cha ushindani kati ya dola za Magharibi. Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Dola ya Ubelgiji ilichukua udhibiti wa Rwanda kutoka kwa Wajerumani, na kuitumia kama mzalishaji wa mazao ya biashara, ikianzisha na kulima kahawa kupitia mfumo wa kazi ya kulazimishwa; ili kudumisha nguvu, Wabelgiji walicheza ushindani kwa kati ya Watutsi na Wahutu, ilizidi kukoleza kupitia kasumba na sera za ubaguzi wa rangi kwa kuwapendelea Watutsi. Ufaransa iliitawala Rwanda kupitia uungaji mkono wake wa mapinduzi ya 1973 yaliyofanywa na Juvenal Habyarimana, ambaye hatimaye alikuwa rais, na kuendeleza mwelekeo huo huo wa kibaguzi lakini badala yake aliwaunga mkono Wahutu. Kulingana na ripoti hiyo, Mitterrand "alidumisha uhusiano thabiti, wa kibinafsi na wa moja kwa moja na rais wa nchi ya Rwanda". Lakini, ilikuwa Amerika, mnamo 1994, ambayo ilitafuta kuipindua serikali ya Rwanda, kupitia vikosi vya Watutsi wa Rwandan Patriotic Front (RPF) vilivyoungwa mkono na Uganda, na hii ndio iliyopelekea mauwaji ya halaiki na serikali ya Wahutu, ikiungwa mkono na Ufaransa. Ripoti hiyo inaashiria tishio la Amerika: "Kuelea juu ya Rwanda lilikuwa tishio la ulimwengu wa Anglo-Saxon, uliowakilishwa na RPF na Uganda, pamoja na washirika wao wa kimataifa".

Himaya zimekuwepo kwa muda mrefu katika historia ya ubinadamu lakini kupitiliza kwa ubeberu wa Magharibi hakuna ulinganisho katika zama za awali. Mgawanyiko wa Magharibi baada ya Westphalia kuwa mataifa yenye msimamo mgumu umezidisha ushindani na uhasama kati yao, huku fahamu ya dola ya kitaifa pia imezidisha tofauti kati ya taifa la kibeberu na mali zake za kikoloni. Ingawa dola za Magharibi huepuka kutekeleza mashambulizi ya moja kwa moja wenyewe kwa wenyewe, wanaona kuwa mchezo mzuri ni kushambulia maslahi ya kila mmoja, ambayo ni pamoja na mali zao za kikoloni. Unyonyaji wa ulimwengu wa Magharibi hautaisha hadi Umma wa Kiislamu utakaposimamisha tena Khilafah Rashida ya Kiislamu kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itaunganisha ardhi zote za Waislamu, kukomboa maeneo yaliyokaliwa, kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu wote. Dola ya Khilafah, kama ilivyokuwa kwa miaka elfu moja hapo awali, itaregesha amani, maelewano na ustawi kwa ulimwengu wote kupitia kwanza kuzikabili, halafu kuzidhibiti na kuzituliza dola kuu, ambazo safu zake itaziingia karibu kuanzia kusimamishwa kwake kwa sababu ya ukubwa wake usio kifani, idadi ya watu, rasilimali, eneo na mfumo. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kurudi kwa Dola ya Khilafah kumekaribia.

Misri, Libya

Kufungwa kwa bahati mbaya kwa Mkondo wa Suez wiki hii na meli kubwa ya makontena ambayo imesaki karibu na kingo za mkondo huo kwa mara nyengine tena imeangazia umuhimu wa kistratejia wa Mkondo wa Suez kwa usafirishaji wa ulimwengu. Karibu asilimia 12 ya biashara ya ulimwengu inakadiriwa kupitia katika mkondo huo. Bei ya mafuta iliruka kwa asilimia 4 mara tu baada ya habari za kufungwa huko. Misri ilichukua udhibiti kamili wa Mkondo wa Suez mnamo 1956 lakini ukweli ni kwamba rais wa wakati huo, Gamal Abdel Nasser, alikuwa kibaraka wa Amerika ambaye vitendo vyake vilikusudiwa kudhoofisha ushawishi wa dola  za Ulaya, na hivyo huo ni mfano mwingine tu wa uhasama wa kibeberu wa Magharibi. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Khilafah wa Kiislamu itakayoregeshwa itachukua usimamizi wa Mkondo wa Suez kwa maslahi ya Waislamu pekee.

Amerika inaendelea katika mpango wake wa kuchukua udhibiti kamili wa Libya, mwishowe ikiondoa uwepo wa Ulaya ambao umetawala Libya tangu nyakati za ukoloni. Amerika kwanza ilianzisha uasi nchini Libya, kupitia kibaraka wake Khalifa Haftar; wakati Haftar iliposhindwa kuichukua Tripoli, Amerika iliwaingiza vibaraka wake, Uturuki na Misri, katika pande tofauti za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya. Kwa kufanya kazi pande zote mbili, Amerika iliweza kuanzisha makubaliano juu ya "Serikali ya Umoja wa Kitaifa", iliyoundwa mnamo 10 Machi 2021. Serikali hiyo mpya iko karibu na Uturuki lakini pia inaanzisha mafungamano na Misri. Waziri Mkuu wa GNU Abdul Hamid Dbeibah alizuru Cairo mwezi uliopita na Misri imetangaza kufungua tena ubalozi wake jijini Tripoli na ubalozi mdogo jijini Benghazi. Sasa, wiki hii, Mohammad Menfi, mkuu wa Baraza la Urais la Libya, alizuru Misri, alikutana na Rais Sisi, na kisha akaruka kutoka hapo kukutana na Rais Erdogan nchini Uturuki. Watawala wa sasa wa Waislamu sio kitu zaidi ya vibaraka mikononi mwa nguvu za Magharibi. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utapindua upandikizaji huu wa kigeni na kuchukua udhibiti wa mambo yake wenyewe, na kumpa bay'ah Khalifa muongofu, mwenye uwezo, mwadilifu, ambaye ataongoza utawala jumla na uongozi kwa Umma mzima wa Waislamu.

Amerika Yaisukuma Ulaya dhidi ya China ili Kusawazisha dhidi ya Urusi

Katika siku za hivi karibuni, Amerika imechukua mkakati ufuatao wa Uingereza wa karne nyingi, ambao umekuwa ni kutodumisha marafiki au maadui wa kudumu lakini kufanya kazi endelevu ya kuzisawazisha dola nyengine dhidi yao kwa yao.

Katika hotuba katika makao makuu ya NATO jijini Brussels wiki hii, Anthony Blinken, katika ziara yake ya kwanza barani Ulaya kama Waziri wa Kigeni wa Amerika, ilishajiisha muamala wa Ulaya pamoja na China, akisema kuwa Amerika, “haitawalazimisha washirika katika chaguo la ‘sisi-au-wao’ pamoja na China”. Hii ni licha la msuguano mkali katika wakati huu kati ya Amerika na China.

China ni tatizo linaloongezeka kwa Amerika kwa sababu ya kuingilia kwake Bahari ya China Kusini, ambayo inaathiri Bahari ya Pasifiki, ikizingatiwa na Amerika kukaribia kuwa eneo lake la kipekee ka kistratejia. Lakini Amerika inajua kuwa kuinuka kwa China hakuwezi kusimamishwa mara moja, kwa hivyo Amerika imetaka kuiondoa China kutoka Pacifiki kupitia, kwa mfano, kuishajiisha China katika kujihusisha kwake katika Bahari Hindi, au uwekezaji wake mkubwa na matumizi katika mpango wake wa Ukanda Mmoja Barabara Moja Muamala wa Ulaya na China utasaidia zaidi kwa lengo hili, na pia lingine, ambalo ni kuisawazisha China dhidi ya Urusi. Amerika imetaka kuunda mzozo kati ya Ulaya na Urusi na, kwa mfano, imepinga vikali Bomba la Nord Stream2 ambalo sasa linakaribia kukamilika kuipatia Ujerumani gesi asilia ya Urusi

Ni mzozo huu kati ya dola kuu ambazo hutoa nafasi ya siasa za eneo kwa ajili ya kuibuka kwa dola mpya, ambayo Dola ya Khilafah itakayo simamishwa tena itakuwa nayo tangu kuanzishwa kwake. Kinachohitajika ni Waislamu kutambua nguvu na fursa yao na kutambua wajibu ambao Mwenyezi Mungu amewaamuru juu yao kuutekeleza Uislamu kwa ukamilifu, ambao hauwezi kutekelezwa bila ya utawala wa Kiislamu, kwani sharia nyingi za Kiislamu zinahusishwa na utawala, na dola ima ni sharti la kisheria au hitaji la vitendo kwa utatuzi wa karibu changamoto zote zinazoukabili Umma wa Kiislamu leo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu