Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 27/10/2021

Vichwa vya Habari:

  • Mapinduzi Nchini Sudan
  • Bangladesh Kuondoa Uislamu kutoka kwa Katiba Yake
  • India Yasaini Mkataba wa Kwanza wa Uwekezaji huko Kashmir Pamoja na Imarati (UAE)

Maelezo:

Mapinduzi Nchini Sudan

Mtawala wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, ameripotiwa kumwambia afisa mmoja wa Amerika aliye ziarani kuwa jeshi huenda likachukua hatua siku moja kabla ya kufanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok. Burhan alikuwa akizungumza na Jeffrey Feltman, mwakilishi wa Washington katika Pembe ya Afrika, mjini Khartoum, Axios iliripoti. Mapinduzi ya kijeshi yalifanyika mnamo Jumatatu Oktoba 25 ndani ya saa chache baada ya Feltman kuondoka mji mkuu wa Sudan. Feltman amekuwa akishiriki katika mazungumzo ya kupunguza mvutano kati ya jeshi la Sudan na uongozi wa kiraia. Afisa mmoja wa Kizayuni ambaye jina lake halikutajwa aliiambia Israel Hayom kwamba mapinduzi ya hivi karibuni nchini Sudan ni habari njema kwa juhudi za usawazishaji mahusiano. Afisa huyo alisema al-Burhan ana uwezekano mkubwa wa kuimarisha mafungamano na 'Israel' kuliko Hamdock.

Bangladesh Kuondoa Uislamu kutoka kwa Katiba Yake

Waziri wa Habari wa Serikali ya Bangladesh, Murad Hassan, amesema Uislamu sio dini ya serikali na nchi hiyo hivi karibuni itaregea kwenye katiba yake ya asili ya kisekula ya 1972 iliyopendekezwa na mwanzilishi Sheikh Mujibur Rahman. Ikiwa hatua hiyo itaanza kutekelezwa, Uislamu hautakuwa tena dini ya serikali ya nchi hiyo yenye Waislamu wengi. Katiba ya asili ya kisekula ya Bangladesh ilifanyiwa marekebisho wakati wa utawala wa Jenerali HM Ershad mwishoni mwa miaka ya 1980 na Uislamu ukawekwa kama dini ya serikali. Mshirika wa karibu wa India na Amerika, chama tawala cha Awami League kinafurahia wingi wabunge katika Bunge kwa hivyo kupitishwa kwa marekebisho mapya kunaweza kusiwe vigumu. Hatua hiyo huenda ikaibua upinzani kutoka kwa vyama vya Kiislamu ambavyo vimekuwa vikiendesha kampeni ya kuifanya Nchi hiyo kuwa ya Kiislamu zaidi. Nchi hii inapitia awamu mbaya zaidi ya ghasia za kijamii katika miaka mingi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na mamia kujeruhiwa.

India Yasaini Mkataba wa Kwanza wa Uwekezaji huko Kashmir Pamoja na Imarati (UAE)

UAE imetia saini makubaliano ya kujenga miundombinu huko Jammu na Kashmir, wakati ambapo eneo la Himalaya linashuhudia kuzuka upya kwa ghasia. Mkataba wa Makubaliano unashughulikia ukuzaji wa mali isiyohamishika, mbuga za viwanda, minara ya IT, minara ya kazi anuwai, usafirishaji, vyuo vya matibabu, hospitali maalum na mengineo. Makubaliano hayo yalisifiwa "kama mafanikio makubwa kwa India" na kamishna mkuu wa zamani wa Pakistan Dkt Abdul Basit, huku makubaliano hayo yakizua hasira nchini Pakistan. Kulingana na Dkt Basit kipengee kimoja cha mkakati wa Kashmir wa India kimekuwa jinsi ya kuyashawishi baadhi ya mataifa ya Kiislamu kufungua misheni au balozi zao huko Kashmir na kuwekeza katika eneo hilo ili kupinga ushawishi wa OIC (Shirika la Nchi za Kiislamu). Wachambuzi pia walibainisha kuwa huu ni ujumbe wa Dubai kwa ulimwengu kwamba Pakistan haina eneo la kusimama Kashmir. Mpango huo uliikasirisha Pakistan tangu madai yake juu ya Kashmir na majaribio ya kutangaza suala la Kashmir kuwa la kimataifa yanategemea pakubwa uungwaji mkono wa OIC.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu