Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 22/12/2021

Vichwa vya Habari:

• Pakistan Yakumbwa na Uhaba wa Gesi

• Matatizo katika Eneo la Balkan

• Je, Uchaguzi wa Libya Umeahirishwa?

Maelezo:

Pakistan Yakumbwa na Uhaba wa Gesi

Pakistan inakabiliwa na uhaba mkubwa wa gesi msimu huu wa baridi unaokuja na serikali tayari inatoa visingizio vyake. Chaudary Fawad Hussain, waziri wa zamani wa habari wa Pakistan anadai kuwa Pakistan inamaliza kwa kasi akiba yake ya gesi ambayo inapungua kwa zaidi ya asilimia 9 kwa mwaka, lakini utabiri wa siku zijazo na visingizio havisaidii wakati wafanyikazi wanaachishwa kazi kwa sababu ya kufungwa kwa viwanda. Bei za kimataifa za LNG zimepanda kwa kiwango kisichoweza kufikiwa na familia nyingi za Pakistan na watumizi wakubwa na kugeukia matumizi ya umeme kutazidisha tu hali iwe mbaya zaidi katika utoaji wake. Mgao mkali wa gesi na umeme unatarajiwa na huu hakika utakuwa msimu wa baridi wa kutoridhiwa kwa utawala wa PTI. Fursa zilizokosekana na maslahi yaliyowekwa yana njama ya kudumisha hali halisi ilivyo sasa na kama ilivyo kwa masuala mengi yanayoikabili Pakistan hakuna suluhisho rahisi kwani miongo kadhaa ya usimamizi mbovu haiwezi kurudishwa nyuma kwa wiki kadhaa.

Matatizo katika Eneo la Balkan

Kiongozi wa Waserbia wa Bosnia, Milorad Dodik, ametishia kujiondoa katika taasisi nyingi za serikali ya Bosnia, ikiwa ni pamoja na jeshi la taifa, Mahakama na mamlaka ya kodi jambo linalohatarisha amani ambayo tayari ni tete. Iwapo hii ni njama ya ubabaishaji ya Kirusi kutoka kwa hali ya wasiwasi nchini Ukraine au ni jaribio kubwa la kuvuruga makubaliano ya amani ya Dayton bado ingali haijaonekana. Hatua hiyo inatishia kufufua tena mzozo mbaya zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia na kulirudisha eneo hilo katika mizozo ya kikabila na kidini. Msimamo wa Urusi na Serbia pamoja na mwitikio unaotarajiwa wa Marekani na washirika wake una ushawishi mkubwa juu ya kile kitakachotokea kwani bila idhini ya Urusi na Serbia Republika Srpska ina nafasi ndogo ya kufaulu.

Je, Uchaguzi wa Libya Umeahirishwa?

Mkuu wa Tume ya Juu ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini Libya (HNEC) ameamuru kuvunjwa kwa kamati za uchaguzi nchi nzima, katika hatua inayoahirisha ipasavyo uchaguzi wa rais wa wiki hii. Taarifa ya ndani iliyovuja ya Imad al-Sayeh ya tarehe 20 Disemba ilieleza mambo sita, haswa "kuvunjwa kwa afisi na kamati za uchaguzi za mikoa na mitaa". Mwanachama mmoja wa bodi ya wakurugenzi ya HNEC mnamo Jumanne alithibitisha uhalisi wa waraka huo. Malik Traina wa Al Jazeera, akiripoti kutoka Tripoli, alisema mvutano unaokua katika wiki za hivi karibuni ndani ya vyombo vya kisiasa na kiusalama vya nchi hiyo umetilia shaka iwapo uchaguzi wa Disemba 24 utaendelea kama ilivyopangwa. Baadhi ya waangalizi wamesema walitarajia uchaguzi huo kuahirishwa. Migogoro kuhusu kanuni za msingi zinazosimamia uchaguzi imeendelea katika mchakato mzima, ikiwa ni pamoja na kuhusu ratiba ya upigaji kura, sheria tata ya uchaguzi iliyotolewa Septemba na spika wa bunge, kustahiki kwa wagombea wakuu na mamlaka ya baadaye ya rais na bunge.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu