Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Vya Habari 13/06/2020

Vichwa vya Habari:

Amerika Yaongeza Uwepo wa Kijeshi katika Bahari ya Pasifiki ili kuidhibiti China

Kuporomoka kwa uchumi wa Syria na Lebanon Kunaonyesha kwa nini Mapinduzi ni Muhimu

Serikali Mpya Kibaraka Yaweka Hifadhi Mpya ya Kisheria kwa Uwepo wa Mabeberu wa Amerika Nchini Iraq

Maelezo:

Amerika Yaongeza Uwepo wa Kijeshi katika Bahari ya Pasifiki ili kuidhibiti China

Ni takriban muongo mmoja sasa baada ya Raisi Obama kuanza kuligombania bara la Asia. Uhasama kati ya Amerika na China umefikia kileleni. Haya ni kwa mujibu wa ripoti moja ya shirika la habari la Associated Press katika gazeti la The Los Angeles Times:

Kwa Mara ya kwanza katika mda unaokaribia miaka mitatu, manuari tatu za kubeba ndege za kijeshi zimekuwa zishikilia doria katika bahari ya Pasifiki, maonyesho hayo makubwa ya nguvu za kivita za baharini katika eneo lililotanda taharuki kati ya Amerika na China na ishara kwamba jeshi wanamaji la Amerika limerudi tena baada ya vikwazo vinavyo tokana na kukabiliana na mkurupuko wa virusi vya korona.

Kuonekana kwa pamoja kusiko kwa kawaida kwa manuari hizo tatu za Amerika, huku zikiandamana na meli aina ya Navy cruisers, destroyers, pamoja na ndege za kivita na nyenginezo, kunajiri huku Washington ikiendelea kuitupia lawama Beijing, kutokana na kushughulikia kwake mkurupuko wa virusi vya korona, malengo yake ya kuweka udhibiti wake kwa Hong Kong na kampeni yake ya kijeshi katika visiwa bandia vilivyoko katika bahari ya kusini mwa China.

“Uwezo wa kuwepo kwa njia imara ni sehemu ya ushindani. Na kama ambavyo daima nimekuwa nikawaambia watu wangu hapa, ni lazima uwepo ili uweze kushinda wakati unapambana” alisema  Rear adm Stephen Koehler, mkurugenzi wa operesheni katika Mamlaka ya Indo-Pasifiki. Ndege na meli hizi kubwa za kivita ni alama ya nguvu kubwa ya majini ya Amerika isio na kifani. Hakika ninafuraha sana kwamba kwa sasa tuko nazo tatu”…

Hii ndio “hali mpya ya kawaida” alisema  Koehler, aliyasema hayo huku kukiwa haitarajiwi kuwepo wa meli hizo kubwa tatu katika bahari ya Pasifiki kwa kipindi kirefu, “ni jambo ambalo tunaweza kulifanya muda wowote tukitaka.”

Mzozo mkubwa wa kistratejia baina ya Amerika na China unaupa Ummah wa Kiislamu nafasi adhimu ya kusimamia na kuendesha mambo yake wenyewe na kuwang'oa vibaraka ambao wanatawala kwa niaba ya Wamagharibi. Njia zote za mafanikio zipo wazi, kinacho hitajika ni kuwa tayari na kujitoa mhanga kwazo.

Kuporomoka kwa uchumi wa Syria na Lebanon Kunaonyesha kwa nini Mapinduzi ni Muhimu

Kwa mujibu wa gazeti la Guardian:

Maandamano yamepangwa kufanyika katika mji unaodhibitiwa na serikali ya Syria mwishoni mwa wiki hii huku mgogoro unaoibuka wa kiuchumi ukiwazunguka hata wafuasi watiifu zaidi wa Basha al Assad na sasa kuleta changamoto kubwa kabisa kwa mshiko wake wa nchi wa miaka mingi.

Chakula kimepanda bei kuliko wakati mwingine wowote ule ndani ya miaka 9 ya mzozo, ikichochea matukio yenye kukumbusha maandamano ya Mapinduzi ya Kiarabu ya 2011 katika barabara za mji unaoitwa kuwa mtiifu kwa serikali wa Sweida wiki hii.

“Hatutaki kuendelea kuishi, tunataka kufa kwa heshima”, na yule anayewanyima watu wake chakula ni muasi.” haya yalisikika kwa waandamanaji kwa siku kadhaa mfululizo katika mji wa kusini mwa syria, wakitaka raisi kuachia madaraka. Maandamano mengine yamepangwa kufanyika Jumamosi.

Assad, amejikuta akisibiwa na mambo mengi tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na  tishio la janga la virusi vya korona, mzozo baina yake na binamu yake Rami Makhlouf na kugawanya maslahi sawa kwa sawa kwa wanaomuunga mkono, Moscow na Tehran.

Tatizo mkubwa zaidi la Raisi huyu, hata hivyo, ni hali mbaya ya kifedha kwa jirani yake Lebanon ambayo imepelekea uchumi wa Syria kudorora. Vikwazo vipya vya Amerika dhidi ya serikali yake ambavyo vitaanza utekelezwaji wake wiki ijayo huenda vikaleta athari mbaya zaidi.

Nidhamu dhaifu ya kiuchumi iliyorithishwa na Urasilimali wa Kimagharibi, haiwezi kuleta maendeleo ya uhakika na ya kudumu. Badala ya kutuliza na kutatua matatizo ya uchumi, mfumo huu unazidisha matatizo. Hii ni kwa sababu mfumo huu umejengwa juu ya uhuru wa kumiliki ambao unaliwezesha kundi dogo la wasomi kuteka utajiri na rasilimali nyingi za jamii. Wakati huo huo mfumo huu unashindwa kuzalisha ajira za kutosha kwa jamii ili nayo ipate mafanikio. Waislamu hawataweza kutatua matatizo yao ya kiuchumi mpaka pale watakapo ukataa mfumo huu na kuubadilisha kwa kutabikisha sheria za Kiislamu chini ya utawala wa Khalifah mwongofu.

Serikali Mpya Kibaraka Yaweka Hifadhi Mpya ya Kisheria kwa Uwepo wa Mabeberu wa Amerika Nchini Iraq

Kulingana na Guardian:

Baada ya mazungumzo ya kwanza ya kimkakati baina ya Iraq na Amerika mjini Baghdad yaliofanyika mnamo Juni 11, wawakilishi wa pande zote mbili walitoa tamko la pamoja kuhusu maamuzi walioafikiana katika mzunguko wa kwanza wa mazungumzo. Tamko hilo la pamoja lilipitisha upya makubalino ya kimkakati yaliyotiwa saini mwaka 2008, pamoja na nyaraka zingine baina ya nchi hizo mbili, haswa barua mbili kutoka Iraq kwenda Baraza la la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Juni na Septemba, 2014 Barua hizo ziliomba jamii ya kimataifa kuifadhili katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

 

Kisiasa, Washington ilisisitiza tena heshima kwa “ubwana wa Iraq, heshima ya eneo, na maamuzi sahihi ya mamlaka za Utunzi na Utekelezaji wa sheria za Iraq. Amerika imeelezea uungaji mkono wake wa serikali mpya ya Iraq na mpango wake wa kufanyika uchaguzi wa mapema. Masuala ya ubinaadamu ikiwemo Haki za kibinaadamu na kuwaregesha nyumbani waliohamishwa pia hili lilidokezwa.

Huku mgogoro wa kisiasa ukiwa umeikumba Iraq katika miezi ya hivi karibuni, nguvu za kisiasa za Iraq – na pia makundi yanayounga mkono Iran – zimekuwa zikituma ishara nzuri kwa Amerika, zikiomba usaidizi ili kutatua tatizo hili. Akizungumza baada ya Bunge kumpitisha Waziri Mkuu mpya Mustafah al Kadhimi mnamo Mei, Muhammad al Ghabban kiongozi wa chama cha PMU alisema “ Washington yafaa kuonyesha kupendezwa kwake na Iraq kwa kutilia umuhimu katika kuifadhili Iraq  wakati wa hali Ngumu. Pamoja na kuwahakikishia watu wa Iraq itatoa msaada kwao na sio kuungana na chama chochote cha kisiasa cha Iraq dhidi ya chama chengine”

Katika masuala ya usalama, Iraq imejitolea kutoa ulinzi kwa majeshi ya muungano yanayo ongozwa na wa Amerika ambayo yapo nchini mwake. Amerika nayo ikasema haikusudii kuwa kamba ya kudumu nchini humo, badala yake Amerika ina mpango endelevu wa kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Iraq ndani ya kipindi cha miezi michache ijayo. Pia itajadili kuhusu idadi ya baadhi ya wanajeshi wake watakaobakia Baghdad.

Nchini Iraq Amerika inatekeleza njama yake ya kikoloni kwa kupandikiza serikali ya kibaraka ambayo ni tiifu kwake ili kuhalalisha shughuli za dola ya kigeni. Hawafanyi hivi ili kujihalalisha mbele ya ulimwengu lakini suala la muhimu zaidi ni kuzinyima dola za kibeberu za Kimagharibi nafasi ya kudai chochote, kwani nchi za Kimagharibi ziko katika uhasimu na ushindani mkali wa utajiri na rasilimali za ulimwengu. Kwa yakini Amerika inataka kupunguza kambi zake nchini Iraq, kama ilivyofanya Afghanistan, kwa sababu inataka serikali vibaraka wake zishughulikie ulinzi wao wenyewe wa ndani, na kuyawacha huru majeshi ya Amerika kupanua nguvu  zao katika eneo pana zaidi. Amerika inamiliki karibia kambi elfu moja za kijeshi kote duniani kama sehemu ya himaya ya kijeshi ya kiulimwengu ili kuhifadhi hadhi yake kama dola inayo ongoza duniani. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hivi karibuni Waislamu watasimamisha tena Dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itakuwa chanzo cha kuinuka nguvu mpya katika mambo ya kiulimwengu, ikieneza nuru ya Uislamu kote duniani. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu:

]وَمِنَ الَّذِينَ قَالُواْ إِنَّا نَصَارَى أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُواْ حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاء إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللّهُ بِمَا كَانُواْ يَصْنَعُونَ * يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ * يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنِ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ[

"Na kutoka kwa wale walio sema: Sisi ni Manasara, tulichukua ahadi yao, lakini wakasahau sehemu ya waliyo kumbushwa. Kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya. Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka." [al-Maida: 14-16]

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 15:19

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu