- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Uhalisia wa Uhasama Kati ya Marekani na Iran Katika Eneo Hilo
(Imetafsiriwa)
Swali:
Amerika ghafla imetangaza hatari kwa vikosi vyake na maslahi yake katika eneo la Ghuba, inayotoka kwa Iran na vikundi vyenye mafungamano nayo; ilikuza kiwango cha utayari na kutuma meli ya kijeshi na yenye kubeba ndege, na hata kutuma hospitali ya wanamaji ikiashiria kukaribia kwa makabiliano katika Ghuba. Hii ili sadifiana na kumalizika kwa sera ya Amerika ya kuzitenga nchi zinazo agiza mafuta ya Iran ili kukomesha usafirishaji mafuta ya Iran. Iran imetishia kufunga Mwanya (strait) wa Hormuz kwa nchi zote za Ghuba zinazo safirisha mafuta kupitia hapo huku uhasama ukiendelea eneo hilo! Je huu ndio mwanzo wa vita vitakavyo anzishwa na Amerika katika eneo hili? Ama kuna lengo jengine? Mwenyezi Mungu akujaze kheri.
Jawabu:
Ili kufafanua taswira kamili, turegelea kadhia zifuatazo:
- Hakika, kuna ongezeko kubwa la uhasama katika eneo hilo, ikiwemo kile kilicho tajwa kupelekwa kwa vyombo vya kivita vya majini vya Marekani, ikiwemo Lincoln aircraft carrier, meli kubwa zaidi inayobeba ndege 90 za kivita na ikatuma kikundi cha B-52 kwenye ngome zake katika maeneo ya Ghuba hilo, ikiongeza tahadhari miongoni mwa vikosi vyake na kuondoa wafanyi kazi wasio na umuhimu sana katika ubalozi wao ulio Baghdad. Kile kilicho shuhudiwa ni kufuatishwa tishio la haraka kwa Iran: [Marekani imetuma shehena za kivita mashariki ya kati kwa Iran “ujumbe ulio wa wazi na bila kukoseka.’’ Mshauri wa masuala ya kiusalama John Bolton amesema nchi yake ilifanya hivyo “kujibu shida na ongezeko la mfano wake na onyo.’’ “kutumwa kwa meli za kivita katika Ghuba kufuatia habari za uezekano wa uvamizi kwa vikosi vya Marekani, kulingana na wanahabari wa Reuters wakimnukuu afisa wa Marekani ambaye hakutajwa jina …... Bolton amesema katika kauli kuwa, “Marekani inatuma vikosi vya kushambulia viitwavyo USS Abraham Lincoln strike group na jopo kazi la ulipuaji mabomu kwa eneo la taasisi kuu ya utoaji amri za kijeshi kutuma ujumbe ulio wazi na usio na makosa kwa serikali ya Iran kuwa shambulizi lolote kwa maslahi ya Marekani na washirika wake litakabiliwa na nguvu zisizo na huruma.’’ (BBC, 6/5/2019). Kiuhakika shehena za kubeba ndege ziliingia mkondo wa bahari wa Suez Canal tarehe 9/5/2019 na kisha kufika bahari Arabu mnamo 14/5/2019. Vyombo vya habari vimetangaza kuwa Marekani (yataka kutuma vikosi elfu 120 zaidi katika eneo hilo , habari ambazo zimekataliwa na Rais Trump wa Marekani, ingawa Kaimu Waziri wa Ulinzi Patrick Shanahan amefikisha pendekezo la mipango hiyo kwa Trump…( RT, 14/5/2019, ikinukuu gazeti la ‘New York Times’), yote yaongezeka kwa muongezeko wa matishio kutoka Iran (CNN, ilinukuu chanzo chake, mnamo Mei 7, kwamba utawala wa Marekani umepata habari za kiupelelezi zioneshazo Iran inapanga kuweka zana za kurusha makombora ya masafa mafupi katika vyombo vyake vidogo katika Ghuba. (RT, 14/5/2019)
- Kile kilichofanya mvutano wa Marekani kuwa zaidi ya maneno tu ni kilichofanyika kwa vyombo vinne vya kibiashara karibu na bandari ya Fujairah katika Imarati na shambulizi katika vituo muhimu vya mafuta katika nchi ya Ufalme wa Saudi na haya ndio yaliyofuatia:
- [Vyombo vya kibiashara vinne karibu na maji ya Imarati vilihujumiwa bila ya majeraha yeyote, kulinga na kile Waziri wa Kigeni wa Imarati alisema Jumapili. Haya yametendeka kama shinikizo la Marekani juu ya Iran, ambayo Rais Hassan Rouhani amekubali mapema kuwa nchi yake inakumbwa na hali ngumu. (Middle East Online 12/5/2019)]
- [Kikundi cha Yemen “Ansar Allah” kimetangaza, Jumanne kuwa, kimefanya mashambulizi kutumia ndege zisizo na rubani katika vifaa muhimu vya Saudi… Chombo cha habari Al Masira kikinukuu chanzo cha kijeshi, kilithibitisha kwamba “ndege 7 zisizo na rubani zimevamia vifaa muhimu vya Saudi,” chanzo kimeashiria kuwa “Uvamizi huu mkubwa umekuja kujibu ongezeko la fujo na hujuma kwa watu wetu,” kuongezea kuwa “Ansar Allah wako tayari kutekeleza shambulizi maalum na baya zaidi kama fujo na hujuma zisizo za haki zitaendelea.” (Sputnik Russian Agency, 14/5/2019)]. Kwa haya matokeo mawii, Kauli za Marekani zinakuja na hatari katika Ghuba hii na zimepata mazingira mazuri na mvutano wa Marekani na kukolea kwa hali hii ya Ghuba ni tofauti na matukio kama haya yaliyopita.
- Hata hivyo, na mvutano huu wote eneo la Ghuba, linaashiria vita viko mlangoni, kauli za pande zote mbili, Amerika na Iran, zinapeana taswira nyingine, kwamba vita havitarajiwi! Kauli hizi ikiwemo;
- [Trump amesema katika kauli kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi, katika Ikulu yake, akijibu swali ikiwa Marekani imedhamiria kupigana na Iran: “natarajia haitatokea.’” (RT, 16/5/2019)]
- [(Reuters 16/5/2019) Spika wa Bunge la Seneti wa Marekani Nancy Pelosi alisema siku ya Alhamis kwamba utawala wa Trump hauna idhini kutoka kwa bunge la Congress kuanzisha vita dhidi ya Iran, huku kukishuhudiwa muongezeko wa mvutano katika Mashariki ya Kati. Pelosi amewaambia wanahabari kuwa utawala wa Republican utatoa kauli baada ya mkutano wa ndani wa wakuu wa chama hicho wajulikanao kama ‘Gang of eight’, juu ya Iran siku ya Alhamisi.]
- [(Reuters 16/5/2019) New York Times ilisema mnamo Alhamis, wakinukuu maafisa ambao hawakutajwa jina, katika utawala wa Marekani - Raisi Trump amemwambia Kaimu Waziri wa Usalama Patrick Shanahan kwamba hataki mapambano ya kivita na Iran. Hilo gazeti lilisema kwamba Rais amemwambia Shanahan hivyo Jumatano asubuhi).
- [(Kiongozi mkuu wa Iran Ali Khamenei amesema hakutakuwa na vita na Marekani, katika maoni yaliyo chapishwa katika chombo cha habari cha serikali na katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Ayatollah Ali Khamenei alisema, “hatutafuti vita, wala hawavitafuti.” (BBC, 14/5/2019)]
- [(Mshikilizi wa wizara ya usalama wa Marekani, Patrick, aliliambia kongamano la wanahabari kuwa, lengo la utawala wa Marekani la kuthibitisha uwepo wake wa kivita katika Ghuba ya Arabu ni kuzuia wala si vita.” (France 24, 22/5/2019)] mwisho wa nukuu
Kauli hizi za Marekani na Iran zinaashiria kile kinacho tangazwa na vyombo vya habari, kuhusu vita kati ya Amerika na Iran si hakika. Kile alichokisema kiongozi wa Iran kwa watu wake ni, wala hawatafuti vita wala wao hawavitafuti, ndio kauli yenye uzito. Hii ni kulingana na kauli kuhusiana na vita, na kuharibiwa kwa meli za kivita za Marekani limetengwa. Na katika matarajio yaliyo kithiri, kama vita vitatokea, vitafungika katika kutetea muonekano wa pande hizo mbili. Kauli za viongozi wa Marekani mara kwa mara ni kwamba hawataki kubadilisha utawala. Mshauri wa masuala ya Usalama wa marekani, John Bolton, amesema: (sera zetu hazilengi kubadilisha utawala wa Iran, lakini tunataka kuweka shinikizo lisilo la kawaida kwa serikali ya Iran ibadili mwenendo’’... (Tovuti ya Ad-Dustoor 3/10/2018)
4- Kwa hivyo ni ipi sababu ya kuongezeka mvutano eneo hili? Jawabu liko katika sababu tatu zifuatazo:
Sababu ya kwanza ni soko la mafuta la kiulimwangu: Mtazamo wa Marekani kuhusu suala la mafuta umebadilika tofauti na Karne iliyopita, tangu kufanikiwa kwa utafiti wa kuchimba mafuta ya Shale, na Kuruhusu uuzaji wake katika masoko ya nje hata kama inaagiza mafuta kutoka nje na ili kuweka sawa mizani ya biashara na Uchina ni wazidishe uagizaji wa mafuta ya Marekani. Wakati huo huo Marekani inaagizia mafuta kwa bei rahisi kwa viongozi dhalili wa mataifa ya Ghuba, hasa utawala wa Saudi, ambao pesa zake zimerundikana Marekani bila ya kuwa na uwezo wa kuziondoa mpaka mahitaji yatokee, kwa hivyo wanakopa ilhali pesa zao wenyewe hawawezi kuzitumia. Kulingana na hali halisi, shinikizo la Marekani juu ya Iran na kukatazwa kuuza mafuta katika soko la nje itapandisha gharama za mafuta kiulimwengu na hili litafaidi Marekani, kama kuongezeka bei ya mafuta ni mazingira mazuri kwa gharama ya uzalishaji wa mafuta ya Shale. Shirika la Kimataifa la Nishati lazungumzia kuhusu kuchochewa na “kuchanganyikiwa na muonekano wa ugavi” wa mafuta na imeongea kuhusu uwezo wa Amerika kufidia kupungua kwa ugavi wa mafuta kutoka Iran na Venezuela. [(Shirika la Ulimwengu la Nishati lilisema mnamo Jumatano kwamba dunia inahitaji ugavi mdogo wa ziada wa mafuta kutoka OPEC mwaka huu, kwa kuwa Marekani itafidia pengo la uzalishaji litakalotokana na Iran na Venezuela kutosafirisha mafuta yao nje. (Reuters,15/5/2019)] sawia na [(Shirika la Ulimwengu la Nishati limesema, uchimbaji mafuta Marekani kutoka mawe makuu saba utazidi mpaka kufikia mapipa milioni 8.49 kwa siku kufikia mwezi wa Juni. (Reuters,17/5/2019) hivyo ni kuwa kampuni za mafuta za Marekani zinachimba mafuta zaidi wakati wa kuzidi mvutano wa Ghuba huku inazorotesha uchimbaji wa mafuta ya Iran kupitia vikwazo.
Muhimu zaidi, bei ya mafuta inapanda huku Amerika ikitishia kuhujumu vifaa na meli za kubeba mafuta (Tathmini ya Mafuta ilipanda baadaye, Jumatano huku kukiwa na kuzidi kwa mvutano Mashariki ya Kati, unaathiri ugavi wa mafuta ulimwenguni, ikikuza ongezeko la wawekezaji wa biashara ya mafuta iliyokuwa haikutarajiwa. Bei ya mafuta imepanda na senti 53 ama asilimia 0.7, kufikia dola 71.77 kwa kila pipa, ilhali bei ya mafuta ya Marekani kuuzwa dola 62.02 kwa kila pipa, kupanda kwa senti 24 ama asilimia 0.4. Bei za mafuta imepigwa jeki baada ya Saudi kusema Jumanne kwamba ndege zisizo na rubani zimelipua mabomba mawili ya mafuta siku mbili baada ya hujuma kwa meli za mafuta karibu na Imarati. (Reuters 05/15/2019).
Hivyo, iko wazi kuwa Amerika inafaidi katika mvutano huu kati yake na Iran kwa kuongezeka bei ya mafuta na imeweza kuongeza uchimbaji wa mafuta, kampuni za Amerika zimekimbilia kuchimba mafuta zaidi ya Shale kwa viwango ambavyo havikutarajiwa. Hakuna shaka kuwa Amerika inatizama mvutano huu kama faida kwa kampuni zake za mafuta haswa ni mtazamo wa fikra za kibiashara zinazo tawala mabongo ya uongozi wa Trump.
Sababu ya pili: Kuingia kwa makubaliano mapya ya kinyuklia na Iran, kutadhamini mgao mkubwa wa faida kwa kampuni za Amerika katika soko la Iran.
Inajulikana vizuri kwamba Amerika inacheza mchezo wa wazi na Iran ili kuingia kwa makubaliano mapya ya kinyuklia, ikiwemo mpango wake wa makombora na ushawishi wake katika eneo. Wakati Waziri wa Kigeni wa serikali ya Amerika alipozuru nchi ya Iraq, Kile Pompeo alicho mwambia Abdul Mahdi kiukweli, kulingana na vyanzo vinavyo jua kwa undani kuhusu mkutano wao, ilikuwa tofauti kabisa na hata Waziri Mkuu wa Iraq alishangazwa na vile Pompeo alivyo ongea naye. Pompeo alimwambia kuwa afikishe salamu Tehran kwamba Amerika haiko makini na vita na kile Trump anataka ni makubaliano mapya ya kinyuklia – makubaliano ambayo yana sifa zake mwenyewe… Noon Post 15/05/2019, nukuu British Middle East Eye). Na Rais wa Amerika hafichi lengo lake: (Rais wa Amerika aelezea hisia zake za kuwasiliana na Iran kumaliza mvutano, ambao unazidi kuwa tete, na uongozi ukaacha nambari za simu kwa Uswizi ili Iran iweze kuwasiliana nao ili wakubaliane. Rais wa Amerika amesema, “kile wanahitajika kufanya ni waniiite, tukae chini na tuweze kukubaliana, makubaliano bora.” Trump amesema, “Hatutaki tu, wawe na silaha za kinyuklia. Hatutaki mambo mengi, na tutawasaidia kuwaweka katika hali bora zaidi, hatutaki kuumiza Iran,” Trump amesema katika hotuba aliyoitoa Ikulu. “Nataka wawe na nguvu kubwa na wawe na uchumi mkubwa lakini lazima watuite na wakituita tuko tayari kuongea nawo.”
White House iliwacha nambari ya mawasiliano ya simu kwa Uswizi, ambayo inawakilisha Iran katika mahusiano ya kidiplomasia na Amerika, ili iwe daraja la mawasiliano ikiwa Tehran wanataka makubaliano na Washington (CNN, 11/05/2019). Vile vile kama RT walivyo ripoti 15/05/2019 kwamba Raisi wa Amerika Trump amesema yuko na uhakika kwamba Iran watataka makubaliano karibuni). Kwa mukhtadha huo huo, “Intikhab” Tovuti ya Iran iliyo karibu na wanamageuzi, umeweka wazi Jumanne malengo ya ziara ya Waziri wa Kigeni wa Oman Yusuf bin Alawe kwenda mji mkuu Tehran. Tovuti imesema 21/5/2019 kwamba (lengo la ziara ni kupatanisha kati ya Amerika na Iran na kujadili mada ya kulengwa ubalozi wa Amerika ulioko Baghdad na maendeleo ya eneo…) Tovuti ukaongezea kuwa (waziri wa Oman, Yusuf bin Alawe, amekuja pamoja nayo katika ziara hii ya ghafla salamu kutoka kwa Rais wa Amerika Donald Trump) bila kupeana maelezo ya ndani.
Tatu, na la muhimu zaidi, ni mchakato wa kuunda muungano wa Amerika na Waarabu ambao utajumuisha umbile la Kiyahudu dhidi ya Iran.
Ukiangalia malengo ya sera za Amerika katika eneo na msimamo wa eneo lenyewe, inaonyesha kwamba sababu muhimu ya Amerika kuongeza mvutano wake na Iran ni kujenga muungano na kuufanya rasmi. Hivyo ni kuhamisha mzozo wa eneo kutoka kwa uvamizi wa Israeli na kukaa kwake katika Ardhi tukufu ya Palestina ambayo lazima ipiganiwe na ikombolewe na irudishwe Palestina katika ardhi za Waislamu, mpaka kwa mzozo wa kimadhehebu dhidi ya Iran! Kwa maneno mengine, kujumuisha umbile la Kiyahudin katika eneo. Lengo hili, ambalo Amerika na Uingereza hazikufaulu kwa makarne, leo lina matumaini ya kufaulu kupitia viongozi wasaliti hasa wa eneo la Ghuba, ambao wanakimbilia kusawazisha na umbile la Kiyahudi chini ya kisingizio cha Amerika “hofu dhidi ya Iran”.
Hili liko wazi katika msimamo wa Umbile la Kiyahudi: “Katika kivuli cha mvutano katika Ghuba, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, katika uwepo wa balozi wa Amerika Friedman, amesema, “Kuna mwangaza mpya, mwamko mpya katika uhusiano wetu na nchi nyingi jirani zetu za Waarabu na nyingi za wasiokuwa Waarabu. Tumeunganishwa na hamu yetu ya kusimamisha uchokozi wa Iran. Israel na nchi zote katika eneo na nchi zote zenye kutafuta amani lazima zisimame pamoja na Amerika dhidi ya fujo za Iran. Lazima tuendelee kuimarisha taifa la Israel na kuendelea kuimarisha muungano wa lazima na Amerika.’’ (RT 14/05/2019). Kwa umbile la Kiyahudi kusimama na Waarabu au pengine nchi za Kiislamu na Amerika kusimamisha uchokozi wa Iran, inaashiria kuwa mazungumzo ya mpango wa mvutano wa Amerika ni kuunda muungano wa eneo dhidi ya Iran, ikiongozwa na Amerika, ikiwemo kujumuishwa umbile la Kiyahudi kupitia mvutano huu, kauli za uchochezi na baadhi ya matendo ya kijeshi kama ilivyo Fujairah na vyombo vya Aramco ni mchakato wa kuzindua muungano huu wa NATO ya eneo na mchakato wa kuzindua hilo bado waendelea. Utangulizi wake ni kupokewa Riadh siku ya Jumatatu, 6/04/2019 kwa mkutano wa Waarabu na Amerika ambao Qatar ilihudhuria katika kuzindua Muungano wa Mikakati ya Mashariki ya Kati inayojulikana kama “NATO ya Kiarabu” katika vyombo vya habari. Shirika la Habari la Saudi limetangaza [mkutano umefanyika “kwa ushirika mkubwa wa Saudi, Amerika, Imarati, Ufalme wa Bahrain, nchi ya Kuwait, Usultani wa Omani, nchi ya Qatar na Ufalme wa Jordan.” Mkutano umeeleza: “Ni hatua muhimu katika mchakato wa kuzindua huu muungano, ambao umedhamiria kuongeza usalama na utulivu katika eneo na duniani.” (RT 10/04/209)]. Kwa hivyo, mchakato wa kujenga muungano huu wa kivita uko na nguvu zote. Furaha ya Umbile la Kiyahudi ya kuratibu usalama na Waarabu na nchi za “Kiislamu” dhidi ya Iran inamaanisha umbile la Kiyahudi litahusika katika maamuzi ya Amerika na sheria lakini bila ya tamko. Kutangazwa kwake kutachelewa mpaka Amerika ipange kwa amani na la muhimu kusawazisha viongozi wasaliti wa Ghuba na Umbile la Kiyahudi.
Hitimisho
- Kuendelea kwa matukio na hali ya Mvutano sio mwanzo wa vita vya kina baina ya Amerika na Iran, lakini kuna uwezekano wa kufanikisha sababu tatu zilizo tajwa, lakini hili halitozuia mashambulizi madogo madogo kutokea ili kustiri muonekano wa pande hizi. Kuzuia kutoaibika kwa sababu ya mwenendo wao wa uchochezi na kauli zao za vitisho, kuzuia makosa yasitendeke na kubadilisha tabia!
- Inaumiza kwamba hata kama Amerika haikuficha malengo yake katika semi na vitisho vyake, viongozi wa nchi zetu, haswa za eneo la Ghuba, wanahalalisha kiburi cha Amerika na utawala wake kwenye eneo, kana kwamba wao ni viziwi, mabubu na vipofu na hawaelewi na kisha wanaukosa huu ulimwengu na wa mwisho.Mwenyezi Mungu (swt) asema kweli:
﴾وَمَنْ كَانَ فِي هَذِهِ أَعْمَى فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَى وَأَضَلُّ سَبِيلاً﴿
“Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi njia” [Al-Isra’: 72].
19 Ramadan 1440 H
Ijumaa, 24/5/2019 M