- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Mgogoro wa Mafuta na Athari Zake
(Imetafsiriwa)
Swali:
Habari zimeripotia kushuka kwa ghafla kwa bei ya mafuta, hususan mafuta ya Texas, hadi ikafikia takriban dolari 30 chini ya sifuri. Hata mafuta ghafi ya Brent, maarufu kwa biashara yake tegemewa, yalishuka kwa takriban asilimia 9 hadi dolari 25 kwa pipa, na sababu zake zinatofautiana, ima ni kwa sababu matangi ya mafuta yamejaa pomoni au yanakaribia kufurika na kumwaika, au kutokana na athari ya virusi vya Korona vilivyo pelekea kuporomoka kwa uchumi na kupungua kwa hitajio la mafuta… nk. Je, ni zipi sababu za mgogoro huu wa mafuta? Je, utakuwa ni wenye kuendelea? Na unaathiri vipi uchumi wa Amerika na ulimwengu?
Jibu:
Ili kutambua uhalisia wa mgogoro huu wa mafuta kiujumla na hususan mafuta ya Kiamerika (Texas Magharibi) na athari yake kwa uchumi wa Amerika na ulimwengu, ni muhimu kujua dhurufu tatu za kiuchumi na kisiasa na athari yake maalum juu ya mafuta ya Texas, kisha kuenea kwa athari yake hadi kwa mafuta ya Brent na kisha hadi kwa uchumi wa Amerika na ulimwengu:
Kwanza: Athari ya virusi vya Korona juu ya matumizi ya mafuta:
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakati virusi vya Korona vilipo anza kusambaa kutoka China na kisha hadi Ulaya na kisha hadi Amerika, na yale yaliyo andamana na hili ya ulazimisha wa hatua za karantini na kufungwa kwa sekta nyingi za uchumi katika kila nchi, vilevile hali ya kulemaa iliyo athiri safari za ndege kutokana na marufuku ya kusafiri baina ya nchi nyingi kuu, hususan Ulaya na Amerika, kwa hofu ya kusambaa kwa maambukizi, ikiongezewa na kuchanganyikiwa kukubwa katika biashara ya kimataifa ikisababisha uhaba mkubwa wa bidhaa zisizo za chakula na bidhaa za kimatibabu, kisha ikaathiri harakati za uchukuzi, huku inajulikana fika kuwa usafiri wa nchi kavu na angani hutumia mafuta kwa asilimia 68 (Independent Arabic, 24/4/2020), Na yote haya yamepelekea kikwazo kwa hitajio la mafuta kutokana na virusi vya Korona, na kikwazo hiki kinazidi kuongezeka zaidi na zaidi kwa ongezeko la janga la maambukizi kutoka nchi moja hadi nyengine. Janga hili lina andamana na ulemavu wa sekta za kiuchumi katika kila nchi ambayo janga hili limesambazwa, lakini uhusiano wa hili na mafuta hauko sawia, hivyo pindi janga hili lilipoingia katika nchi kuu za Ulaya lilisababisha mporomoko mbaya wa hitajio la kiulimwengu la mafuta, kwa sababu nchi hizi ndio watumizi wakubwa wa mafuta. Pindi virusi hivi vilipofika Amerika na kuishambulia vikali, inayo tumia asilimia 20 ya mafuta ya ulimwengu, mgogoro wa bei ya mafuta ukaporomoka vibaya.
Kwa upande wa kidijitali, hitajio la mafuta limeporomoka kwa takriban asilimia 30 katika ulimwengu ambao unatumia takriban mapipa milioni 100 kwa siku, na tutachukua taarifa mbili pekee miongoni mwa taarifa jumla zinazo thibitisha mporomoko huu katika hitajio:
1- Taarifa ya kwanza: [Shirika la Kimataifa la Kawi leo, Jumatano 15/4/2020, limetabiri kwamba hitajio la kiulimwengu la mafuta litapungua kwa mapipa milioni 29 kwa siku kwa msingi wa kila mwaka mnamo Aprili, na kurekodi viwango ambavyo havijapatapo kuonekana kwa miaka 25… (Tovuti ya Gazeti la Al-Wafd mnamo 15/4/2020)].
2- Taarifa ya pili: [Waziri wa Kawi wa Urusi Alexander Novak alitangaza kuwa hitajio la kiulimwengu la mafuta limepungua kwa mapipa kati ya milioni 20 na 30 kwa siku, akisema: "Sasa tumefika chini ya hitajio la kiulimwengu la mafuta." (Al-Arabiya Net, 22/4/2020)].
Hivyo, hitajio la mafuta lilianguka kwa kiwango cha kushangaza mno isipokuwa katika dhurufu za vita vya ulimwengu! Na yote haya yamejiri katika kipindi (kati ya miezi 3 na 4), yaani, wakati wa janga la virusi vya Korona, hadi mafuta ya Texas kufikia chini kabisa, yaani takriban -37, mnamo 20/4/2020, ambapo iliitwa "Jumatatu Nyeusi".
Pili: Dhurufu ya pili ni dhurufu ya kisiasa:
Kwa kuwa mafuta ni bidhaa ya kistratejia, ambayo nchi huyatumia kushambulia nchi nyenginezo, na hapa tunazungumzia kuhusu sera ya Kiamerika iliyo isukuma Saudi Arabia hadi katika vita vya bei ya mafuta pamoja na Urusi mwezi mmoja tu uliopita, na kufafanua hilo:
1- Amerika ilikuwa inailazimisha Urusi kupunguza uzalishaji wake wa mafuta ili kudumisha bei za juu ya mafuta ili kampuni za mafuta ya Kiamerika ya shale ziweze kushindana katika masoko, kwa sababu uchimbaji mafuta ya Kiamerika ya shale ni ghali mno, na kwa sera hii Saudi Arabia ilifaulu, kwa miaka mitatu, kuifanya Urusi ijiunge na OPEC katika kupunguza uzalishaji ndani ya kundi jipya la OPEC Plus kwa mapipa milioni 2.1 kwa siku. Makubaliano haya ya Saudi pamoja na Urusi yalimalizika muda wake mwishoni mwa Machi 2020. Yalikuwa ni makubaliano kabla ya kusambaa kwa virusi vya Korona, na mwisho wake ukasadifiana na kuenea kwa virusi vya Korona.
2- Kwa kuenea kwa virusi vya Korona nchini China na kuanza kusambaa kwake hadi nchini Italy, bei za mafuta zilianza kuanguka na kufikia dolari 45 kwa pipa (Brent), na kiwango hiki cha bei na kuendelea kuanguka ni hatari kwa wazalishaji wa mafuta wa Kiamerika, na inahatarisha kuwatoa katika masoko, na hivyo basi bei ni lazima ipandishwe. Kisha Amerika ikaisukuma Saudi Arabia kutia shinikizo juu ya Urusi ili kupunguza zaidi uzalishaji ili kukabiliana na kuendelea kuanguka kwa hitajio la kiulimwengu la mafuta kutokana na virusi hivi, hivyo mkutano wa OPEC Plus ulifanyika mnamo 6/3/2020 pindi Urusi ilipo kataa kukata zaidi uzalishaji, kwa hofu ya kuifidia Amerika kwa upunguzaji wa mafuta ya shale!
3- Kwa kufeli kwa mkutano wa OPEC Plus uliotangulia kutajwa, bei za mafuta zilianguka mara moja kwa asilimia 10 kutokana na kuenea kwa habari za tofauti za kundi la OPEC Plus.
4- Siku chache tu baada ya kufeli kwa mkutano huo, Saudi Arabia ilianzisha vita vya bei dhidi ya Urusi ili kuilazimisha kufanya ukataji huo mpya katika hatua tano:
a- Hatua ya kwanza: ilitupilia mbali makubaliano ya kwanza (kupunguza mapipa milioni 2.1) licha ya tangazo la Urusi la kujitolea kwake kwa makubaliano haya yaliyo tangulia,
b- Hatua ya pili: ni ongezeko kubwa la uzalishaji wake wa mafuta, kuanzia Aprili 1 (tarehe ya mwisho wa makubaliano ya kwanza pamoja na Urusi ya kupunguza uzalishaji) wa mapipa kati ya milioni 12 hadi 13 kwa siku licha ya matatizo ya hitajio la kiulimwengu la mafuta kutokana na virusi vya Korona,
c- Upunguzaji wa wateja wake wa Asia kwa dolari 6 kwa pipa, wa kwanza katika historia kwa kiwango hiki cha upunguzaji bei,
d – Kupitia hili, ilitaka upunguzaji uzalishaji na zaidi, ili wateja wanaofanya biashara ya mafuta ya Urusi kuchukua mgao wa soko,
e- Kukodi magari makubwa yenye matangi ya usafirishaji mafuta ili kuyatumia kama matangi yanayo elea baharini, ili kulizamisha soko kwa mafuta ya ziada.
5- Kwa hatua hizi za Saudi Arabia ambazo zilitangazwa siku chache tu baada ya tarehe 6/3/2020 (mkutano wa OPEC Plus uliofeli), bei za mafuta zilianguka kwa thuluthi moja (bei za mafuta zilipoteza hadi thuluthi moja ya thamani yake mnamo Jumatatu katika hasara yake kubwa zaidi ya kila siku tangu Vita vya Ghuba mnamo 1991, baada ya Saudi Arabia kuashiria kwamba ingeongeza uzalishaji ili kuongeza mgao wa soko, huku mkurupuko wa virusi vya Korona kihakika ukisababisha ongezeko la usambazaji katika soko! Kisha hifadhi ya mafuta ghafi ya Brent yanatarajiwa kushuka kwa asilimia 22 dolari 37.05 kwa pipa, baada ya mwanzoni kushuka kwa asilimia 31 hadi dolari 31.02 kwa pipa, ambacho ni kiwango cha chini zaidi tangu 12/2/2016… (chanzo: Reuters 9/3/2020). Tambua kwamba mafuta ghafi ya Brent yanachimbwa katika viwanja vya mafuta katika Bahari ya Kaskazini. Na mafuta ghafi ya Brent ni mchanganyiko wa mafuta ghafi ya Brent – Forties, Oseberg na Ekofisk, na hutumiwa kama kipimo cha uwekaji bei thuluthi mbili za uzalishaji wa mafuta wa kiulimwengu,hususan katika masoko ya Ulaya na Afrika, na wakati mwengine husafirishwa hadi Amerika na baadhi ya nchi za Afrika, endapo bei ni muwafaka, baada ya kuzingatia gharama za usafirishaji. Mafuta ghafi ya Brent yanauzwa katika soko la ubadilishanaji baina ya mabara (ICE) jijini London, ikimaanisha kuwa Saudi Arabia, kupitia hatua hizi, ilizishusha bei za mafuta, na baada ya tarehe 1/4/2020, ambapo hatua za Saudi zilichukuliwa kutabikishwa, baada ya makubaliano ya OPEC Plus pamoja na Urusi kumalizika mwishoni mwa Machi, ziada ya mafuta imedhihirika wazi sokoni, ambapo ilizisukuma chini bei za mafuta (ikilinganishwa na Brent) hadi chini ya dolari 30 wakati wa tarehe 4 mwezi Aprili na kabla ya tarehe 20/4/2020.
6- Sera hii ya Saudi ilikuwa ni sera ya Kiamerika ya kuishinikiza Urusi, lakini ilikuwa ni sera ambayo imechorwa jijini Washington takriban miezi miwili iliyopita, yaani, kabla ya vipimo vipya vya hitajio la mafuta kuanguka, kutokana na kuendelea kwa ukali wa mkurupuko wa virusi vya Korona, hususan ndani ya Amerika. Kutokana na natija ya mambo haya mawili (sera ya Saudi Arabia, inayo sukumwa na Amerika, na ongezeko kubwa la kuanguka kwa hitajio la mafuta) uharibifu mkubwa ambao idara ya Trump imefanya katika kuishambulia Urusi ilianza kushambulia kulia na kushoto na haikuzisaza kampuni zake za mafuta ya shale! Kwa maana nyengine ni kuwa, lile ambalo Amerika ililipanga, kukata bei za mafuta, halikutarajia kufikia chini kiasi hiki, na hili lilisababishwa na mambo mawili yanayo fanya kazi pamoja: sera ya Kiamerika (Saudi) dhidi ya Urusi, na kuendelea kuporomoka kwa hitajio la mafuta ulimwenguni, jambo ambalo halikugunduliwa wakati wa kuunda sera hiyo ya Kiamerika. Shinikizo kwa kampuni za mafuta ya shale liliongezeka nchini Amerika. Mnamo 2/4/2020, "Witting Petroleum" ilitangaza kufilisika kwake, na kampuni mia moja za mafuta ya shale zilisimama ukingoni mwa kufilisika, kwa sababu bei za mafuta sokoni zilikuwa chini kuliko bei za gharama ya uzalishaji: (gharama ya chini kwa kila pipa la mafuta ya shale ni takriban dolari 35 kwa pipa… (chanzo: tovuti ya Masoko ya Kiarabu, 11/3/2020. Kwa mujibu wa nakala ya Kiarabu ya gazeti la 'The Independent' 24/4/2020, hifadhi ya mafuta ya Texas Magharibi mnamo Alhamisi 23/4/2020 ilikuwa kati ya dolari 15 kwa usambazaji wa Juni na takriban dolari 27 kwa usambazaji wa Septemba, na mikataba ya hifadhi zote hadi kufikia mwishoni mwa 2020 zilikuwa chini ya bei ya dolari 30 na hili linatia shinikizo juu ya mafuta ya shale.
7- Kwa sababu ya hali hizi hatari ambazo sekta ya mafuta ya Amerika inazipitia, kutokana na mkurupuko wa janga la virusi vya Korona, idara ya Kiamerika ilitoa matangazo mengi ya nia yake ya kuingilia kati baina ya Urusi na Saudi Arabia ili ziregelea upunguzaji wa uzalishaji na Raisi wa Amerika alimwita Raisi wa Urusi ambaye ulafi wake uliamshwa, kwa kurudi kwa mawasiliano pamoja na Amerika kwa ushirikiano nayo (sio na Saudi Arabia) juu ya bei za mafuta. Trump pia aliwasiliana na Saudi Arabia; Trump alisema: "Tulikuwa na maongezi mwanana na Raisi Putin. Tulikuwa na maongezi mwanana na mfalme mtarajiwa." (Chanzo: Euronews, 1/4/2020)
Kijumla, yaweza kusemwa kwamba idara ya Trump imeyafadhili makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa mafuta kati ya Urusi na Saudia, makubwa zaidi katika historia, kwa takriban mapipa milioni 10 ya mafuta kwa siku: (wanachama wa OPEC na washirika wao walifikia makubaliano wastani ya kupunguza uzalishaji wa mafuta wa kiulimwengu kwa asilimia 10 baada ya kupungua kwa hitajio… Lililo thibitishwa mpaka sasa ni kuwa OPEC na washirika wake watapunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 9.7 kwa siku) (Chanzo: BBC, 12/4/2020). Makubaliano haya yanaanza utabikishwaji wake mnamo 1/5/2020 na kudumu kwa muda wa miezi miwili, baada ya hapo nchi zilizo tia saini makubaliano hayo wataukadiria tena uhalisia wa hitajio la kiulimwengu ili kuamua hatua nyengine. Ni makubaliano ya muda mfupi, kwa miezi miwili, yanayo subiri kuongezeka kwa hitajio la mafuta la kiulimwengu mwishoni mwa Juni. Lakini, imegunduliwa kwamba mgogoro wa bei ya mafuta umefikia kina kikubwa ambapo masoko hayakujibu makubaliano haya makubwa mno, hivyo bei hazikushuka kimsingi pekee, lakini bei ya mafuta ya Brent ilianguka chini ya dolari 30. Hili linafafanuliwa na hitajio la kiulimwengu ambalo limeshuka kwa mapipa milioni 30 kwa siku na kupunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 10 kwa siku hakusaidii!
Tatu: dhurufu ya tatu ni hifadhi ya mafuta ya Amerika.
Kuna aina mbili ya hifadhi ya mafuta nchini Amerika, ya kwanza ni hifadhi ya kistratejia ya dola, na ya pili hifadhi ya kampuni. Dhurufu hii, pamoja na dhurufu nyengine mbili, zimechangia kuongeza kwa kina cha mgogoro huu wa mafuta: upande mmoja inahusiana na hali ya hifadhi ya kistratejia, huku upande mwengine ni maalumu kwa Mafuta ya Magharibi mwa Texas, na ili kufafanua hilo:
1- Hifadhi ya mafuta ya kistratejia (ya nchi) kwa jumla aghlabu huwa iko katika matangi yaliyo chini ya ardhi ili kuhifadhi mafuta yanayo chimbwa kwa ajili ya matumizi wakati wa mgogoro, na nchi nyingi zimejengwa matangi haya baada ya mapendekezo ya Shirika la Kawi la Kimataifa kutokana na mgogoro wa mafuta katika vita vya 1973. Kila moja ya nchi hizo za mnunuzi mkuu ina matangi yake ya mafuta yenyewe, ambapo yaweza kutosheleza hitajio lake la kati ya siku 30 hadi 90 hii ni endapo itapunguzwa.
2- Mnamo 1975, Bunge la Congress la Amerika lilipitisha sheria inayoilazimisha serikali hiyo ya majimbo kubuni maeneo ya kuhifadhi viwango vya kutosha vya mafuta ghafi ili kulinda hitajio lake endapo upatikanaji wake utakumbwa na aina fulani ya hatari mbaya. Maeneo ya kuhifadhi yako katika pwani za majimbo ya Texas na Louisiana, dola ina jukumu la ulinzi wake mkali, na kiwango cha juu kabisa cha bidhaa hii ya kistratejia nchini Amerika ilifikia mapipa milioni 727 mnamo 2009. Kuongezea juu ya hifadhi za majimbo, kampuni za Kiamerika zinazo fanya kazi katika sekta ya kawi zinahifadhi viwango vyao wenyewe ambavyo kijumla ni sawia na Hifadhi ya Majimbo, matangi kama hayo ya ardhini ya kampuni ni mengi katika jimbo la Texas, kutokana na kuwa ndilo jimbo kubwa zaidi ambalo mafuta huzalishwa nchini Amerika kwa muda mrefu, ambayo huitwa "Mafuta Ghafi ya Texas Magharibi", pamoja na jimbo jirani la Oklahoma, ambalo mafuta ya Texas husafirishwa kutokea kwake hadi katikati mwa bara ya Amerika.
3- Kwa kuporomoka bei za mafuta siku za nyuma mnamo 6/3/2020 na kufuatia vita vya bei kati ya Saudi Arabia na Urusi, nchi nyingi, hususan Amerika na China, zilianza kujaza hifadhi za mafuta yao ya kistratejia, na wakati huo Trump alikuwa amefurahia bei za chini. Amerika ilifanya bidii kununua mafuta rahisi kutoka Saudi Arabia au kwengineko, na kabla ya kuja kwa "Jumatatu Nyeusi", matangi ya Texas yalikaribia kujaa, kama hayakuwa tayari yamejaa pomoni. Hivyo, tatizo la hifadhi za mafuta limefikia kiwango kibaya na kilicho pitiliza, kiasi ya kuwa uelekezaji wa uchimbaji zaidi wa mafuta (katika hali ya kukosekana mauzo) ili kuyahifadhi imekuwa kadhia ngumu, na wakati mwengine kutopatikana, ikimaanisha, ufungaji wa mkondo wa hifadhi kama suluhisho kwa wazalishaji mafuta, hususan katika jimbo la Texas.
4- Hivyo, hifadhi za mafuta za kistratejia za Amerika zimejaa kwa asilimia kubwa, na magari ya usafirishaji mafuta yanahudumu baharini kama huduma za hifadhi, hivyo kukoleza tatizo la hifadhi, kwani limepanuka hadi katika huduma za kuhifadhi mafuta ya Texas Magharibi katika nukta yake ya utoaji katika sehemu ya Cushing, Jimbo la Oklahoma, kaskazini mwa Texas (na viwango vya mafuta ghafi yaliyo hifadhiwa nchini Amerika, hususan katika sehemu ya Cushing, ambako ndio nukta ya utoaji kwa Texas Magharibi. Eneo la wastani kwa mafuta ghafi ya Amerika ni jimbo la Oklahoma, huku viwanda vya kusafisha mafuta vikipunguza shughuli zao kukabiliana na hitajio dhaifu (Chanzo: Al-Jazeera Net, 20/4/2020), uwezo wa juu zaidi wa kuhifadhi wa eneo la utoaji la Cushing ni mapipa milioni 76. Wamiliki wa mikataba ya mafuta wanaweza kupokea kiwango hicho kwa hicho haswa eneo la Cushing wakati wa mikataba hiyo, na wanaweza kuyahifadhi kwa viwango vya kawaida hadi yahamishwe katika bara ya Amerika hadi majimbo yaliyo ndani ndani, lakini yaliyo tokea ni:
[Eneo la Cushing, jimbo la Oklahoma, hususan ambako ndiko mafuta ghafi ya wastani ya Texas yanakohifadhiwa, viwango vya bidhaa hiyo vimeongezeka kwa mapipa milioni tano na inakaribia kufikia kiwango chake cha juu zaidi. Hifadhi za mafuta za Amerika na bidhaa zilizo safishwa pia zimeongezeka, huku matumizi ya kila wiki yakipungua kwa zaidi ya asilimia 25 kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na hatua za utengaji watu. (Chanzo: Rai Al-Youm, 25/4/2020)]. Hivyo inaweza kusemwa kwamba mporomoko huo usio wa kawaida katika hitajio la kiulimwengu la mafuta, linalo kadiriwa kuwa asilimia 30 (yaani takriban mapipa milioni 30 ya mafuta kila siku) ndio sababu kuu ya kwanza ya yale tunayo yatazama ya kushuka mtawalia kwa bei za mafuta, na kwa kuwa sera ya Kiamerika-Kisaudi ya kuishinikiza Urusi inawezekana tu kutekelezwa katika nyakati za kawaida pekee, sio nyakati za migororo katika hitajio, imesababisha kukoleza kikamilifu tatizo la bei za mafuta!
Nne: Yote haya yameathiri mafuta ya Texas. Huduma za hifadhi katika jimbo la Oklahoma zimefika kilele, na hakuna tena nafasi ya hifadhi isipokuwa kwa bei za juu mno, na mikataba hiyo imelazimika kufutiliwa mbali kwa gharama yoyote ile. Hivyo, ikapelekea mgogoro wa mafuta ya Texas Magharibi au "Jumatatu Nyeusi" mnamo 20/4/2020, ambapo mafuta yaliuzwa kwa dolari 37 chini ya sufuri kwa pipa, na wafanyi biashara katika soko la ubadilishanaji nchini Amerika wakapata hasara kubwa. Kilicho pelekea mambo kufika nukta hii na kuwa mabaya zaidi ni kile tulichokitaja juu: yaani, ni kujaa pomoni kwa matangi ya Cushing, pindi hifadhi ilipofikia kiwango cha juu kabisa, mpangilio ambao ni nadra sana, bei za hifadhi zikapanda, na kwa sababu utabiri wa matumizi ya mafuta, kwa sababu ya kuendelea kufungwa kwa uchumi, ulikuwa bado hauko wazi na ulikuwa na shaka, bei za hifadhi katika huduma za eneo la Cushing zimepanda pakubwa na zimekuwa ni jambo jengine linalo shinikiza washikilizi wa mikataba ya mafuta ya May. Na hivyo wamejaribu kuachana nayo kwa gharama yoyote, hivyo bei za mikataba hiyo zikashuka hadi dolari 10, kisha baada ya hapo hadi tano, kisha zikaendelea hadi sifuri katika mandhari ya kushangaza, na kisha ikaenda chini ya sifuri, mkataba wa mwisho kati ya hii ukauzwa kwa thamani ya dolari 37.6 chini ya sifuri, huku kukiweko na mshangao mkubwa kwa wafanyi biashara wake, walio athirika na hasara kubwa, pamoja na mshangao kwa wafanyi biashara wa soko la hisa. Hivi ndivyo namna mgogoro wa "Jumatatu Nyeusi" ulivyo tokea mnamo 20/4/2020 kwa mafuta ya Texas Magharibi, na hizi ndizo dhurufu zake zilizoungana pamoja na kupelekea mgogoro mbaya. Kisha mgogoro wa mafuta ya Texas Magharibi ukatokea, na furaha ya Trump haikuwa kwa ajili ya msaada, kupitia makubaliano ya OPEC Plus kati ya Saudi Arabia na Urusi, alipo sema mnamo 12/4/2020, "Hili litabuni maelfu ya nafasi za kazi za kawi nchini Amerika. Ningependa kumshukuru na kumpongeza Raisi wa Urusi Putin na Mfalme wa Saudia Salman bin Abdel Aziz" (Chanzo: CNN Arabic, 21/4/2020). Furaha ya Trump ilikuwa mbali na uhalisia, kwa sababu kuanguka kwa bei katika hali mbaya kama hii imesababisha hofu kubwa ulimwenguni na sio Amerika pekee. Kisha mgogoro wa kiuchumi ukashitadi, bila ya kutaja sekta ya kawi, hivyo vibofu vyake vimekuwa tayari kupasuka!
Tambua kwamba mafuta ya wastani ya Texas Magharibi yanachimbwa kutoka katika viwanja vya mafuta nchini Amerika, na kimsingi yanachimbwa kutoka Texas, Louisiana, na Dakota Kaskazini, na kisha kusafirishwa kupitia mabomba hadi Cushing, jimboni Oklahoma, kwa ajili ya usambazaji, na hifadhi ya mafuta ghafi ya wastani ya Texas Magharibi yanauzwa kupitia soko la ubadilishanaji la New York Mercantile Exchange (NYMEX), linalo milikiwa na Chicago Mercantile Exchange (CME).
Tano: Kwa upande mwengine, tangu mwanzoni mwa janga la virusi vya Korona, Amerika imetabanni mipango kwa ajili ya kusaidia, kuokoa, au kuchangamsha, na mipango hii imeanzishwa, wa kwanza ni mpango mdogo unaogharimu dolari bilioni 8.3 wa matumizi ya dharura ili kusaidia miradi ya afya na kuiwezesha kudhibiti mkurupuko wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona nchini Amerika. Baada ya janga la maambukizi ya Korona kushambulia uchumi nje ya sekta ya afya, [Amerika ilipunguza viwango vya riba hadi kukaribia sufuri, na kuzindua mradi wa kuchangamsha wa gharama ya dolari bilioni 700, katika juhudi ya kuulinda uchumi kutokana na athari ya virusi vya Korona. (Chanzo: BBC, 16/3/2020)], na ikayajaza masoko kwa dolari taslimu ili kukabiliana na upungufu wa pesa taslimu. Kisha ikatabanni mpango wa kuchangamsha wenye gharama ya dolari trilioni 2.2 mnamo 27/3/2020, mpango mkubwa zaidi katika historia ya Amerika, na sehemu kubwa ya mpango huu imeelekezwa katika ununuzi wa madeni ya kampuni zilizo ukingoni mwa kufilisika ili kuzuia kuporomoka kwake wakati huo huo. [Hifadhi ya Majimbo ilitangaza mapema kwamba ingenunua angaa dolari trilioni 500 za bondi za hazina na si chini ya dolari bilioni 200 za rehani za mikopo ya nyumba. Mfumo wa Hifadhi ya Majimbo ya Amerika pia ulitangaza kuunda mradi mpya ambao utatoa ufadhili wa hadi dolari bilioni 300, katika jaribio la kusaidia mtiririko wa pesa kwa waajiri, watumizi na kampuni. (Chanzo: Traders (App), 24/3/2020)]. Kiwango cha gharama za afya juu ya wagonjwa wa virusi vya Korona inatarajiwa kuwa kubwa mno nchini Amerika, na huenda ikazisukuma kampuni za bima kuporomoka, ambazo ni kampuni kubwa sana. Amerika pia inateseka kutokana na janga baya la ukosefu wa ajira, takriban milioni 30 ya Waamerika wamepoteza kazi kutokana na janga la virusi vya Korona, na kwa sababu kampuni zilizokuwa zimewaajiri ziko katika hali mbaya ya kifedha, kurudi katika kazi zao haitakuwa haraka mwaka huu. Idadi hii kubwa inaakisiwa na bajeti ya umma kwa idadi kubwa ya wanaopeleka maombi ya misaada ya serikali ambao wamejisajili kwayo, zaidi ya milioni 22 ya Waamerika wasio na ajira, na janga hili lingali linaendelea. Endapo nchi hiyo itaendelea kutabanni, vifurushi vikubwa vya misaada, pesa ya Amerika huenda ikashuhudia mporomoko mbaya ambao utaidhuru Amerika na nchi zote na watu wote wanaotumia dolari.
Sita: Mgogoro huu haukuathiri tu Amerika pekee, japo ndiyo iliyo shambuliwa vibaya zaidi, lakini pia umeathiri nchi nyenginezo ulimwenguni:
1- Ama Ulaya, hali yake sio nzuri zaidi kuliko ile ya mwenzake Amerika; athari ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona zimetishia muundo wake wa kisiasa pamoja na athari za kiuchumi. Migogoro tunayoishuhudia katika janga hili la maambukizi nchini Italy, Ufaransa, Uhispania, Ujerumani na Uingereza ni ishara wazi. Raisi wa Ufaransa Macron alionya katika mkutano wa waandishi habari kupitia simu mnamo 26/3/2020 kuwa, "mkurupuko wa virusi vya Korona unatishia kuvunja nguzo kuu za muungano…" Aliongeza, "Kilicho hatarini ni kupona kwa mradi wa Ulaya… Hatari tunayo kabiliwa nayo ni kufariki kwa Schengen (Chanzo: Russia Today 26/4/2020; Reuters 27/3/2020). Chansela wa Ujerumani Merkel alisema: "(Kwa uoni wangu, Muungano wa Ulaya unakabiliwa na mtihani mkubwa tangu kuasisiwa kwake… Kitu muhimu ni kuwa Muungano huu uibuke imara kutokana na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na virusi hivi"… (Chanzo: Reuters 7/4/2020). Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alisema mnamo 5/4/2020: "Dhurufu zilizoko kwa sasa ni za kipekee na zinatoa wito wa misimamo imara. Ima tuibuke kutokana na changamoto hii au tutafeli kama muungano…" (Chanzo: German Frankfurter Allgemeine 5/4/2020). Viongozi wa Muungano wa Ulaya katika mkutano wao wa video mnamo 23/4/2020 walikubaliana mara moja juu ya kifurushi cha uokozi cha takriban euro bilioni 500, lakini wakayaacha maelezo yaliyo zozanwa ya ufadhili zaidi hadi msimu wa kiangazi. Walijadiliana kuunda hazina ya misaada, na kutoa bondi za pamoja za virusi vya Korona. Lakini Ujerumani, Uholanzi, Austria na Finland zilitangaza kupinga kwao bondi hizi na hazikulikubali wazo la hazina. Huku Ufaransa, Italy na Uhispania zikiunga mkono mradi huo na ndizo nchi zilizo athirika zaidi. Na kukataa kwa Ujerumani ni kutokana na ukweli kwamba inataraji kutoa mikopo kwa jina lake ili nchi hizi ziwe na madeni kwake ili kuzidhibiti nchi nyenginezo za Ulaya!
2- Ama China, Benki ya Dunia imeonya kwamba "athari za uchumi wa kiulimwengu huenda zikasababisha kukua kwa uchumi wa China kushuka kwa asilimia 2.3 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 6.1 katika mwaka wa 2019" (Chanzo: Alhurra.com/usa 10/4/2020). Ukurasa huo ulimnukuu afisa wa benki kuu ya China akisema: "Anapendekeza kuwa Beijing isiweke kiwango cha ukuaji mwaka huu, kutokana na kuzuka kwa mambo mengi yasiyo tarajiwa inayo kabiliwa nayo." Gazeti rasmi la Kiuchumi la Kila Siku lilimnukuu Ma Jun, mwanachama wa Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki ya Watu ya China, akisema kuwa, "Itakuwa vigumu kufikia asilimia 6 ya ukuaji." Akiongeza kwamba "kuweka lengo huenda ikazipunguza hatua rasmi za kukabiliana na athari za virusi hivi."
3- Ama Urusi, inategemea asilimia 60 ya mafuta na gesi kutoka ng'ambo. Mafuta yanakadiriwa kuwa ndio uhai wa uchumi wa Urusi, hivyo inateseka kutokana na hasara inazozipata, na pesa ya Urusi, ruble, iko katika hali mbaya zaidi, kwani imeanguka hadi thamani ya dolari ni takriban ruble 79 baada ya vita vya bei ya mafuta. Katika ripoti kutoka kwa shirika la habari la Reuters kuhusu hali nchini Urusi, zikiinukuu benki ya Urusi ikisema kuwa: "Uzalishaji jumla wa nchi (GDP) huenda ukapungua kwa asilimia 15 endapo bei za mafuta zitashuka chini ya dolari kumi kwa pipa.
Saba: Kufeli kwa Urasilimali kunafichuka wazi zaidi, kushindwa kwake na kuchanganyikiwa kwake katika kukabiliana na janga la virusi vya Korona kumeibuka, na ulafi wake umeibuka miongoni mwa nchi zake, ambazo zimepigwa na Makonde makali hadi kuziangusha chini sakafuni, hivyo kilicho bakia ni kuasisiwa kwa mfumo tajiri na sahihi wa Kiislamu. Kuna fursa kwa Ummah wa Kiislamu kuinuka tena. Lakini, serikali katika nchi za Kiislamu na wale wanaozisaidia wameweka kizingiti njiani mwa harakati ya Ummah, kwani watawala hawa wanasisitiza juu ya uadui wao kwa kushirikiana kwao na nchi kuu za kikoloni.
Ummah unahitaji uongozi wa kweli wenye ikhlasi utakao waongoza kwa mujibu wa Uislamu wa kweli, na bila shaka unatambua kwamba Hizb ut Tahrir ndio kiongozi asiye wadanganya watu wake, basi unapaswa kuungana nayo na kufanya kazi kwa ikhlasi,
(وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ)
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj: 40].
Kaka zangu na dada zangu wapendwa, matukio haya yanaashiria kwamba msimamo wa kimataifa baada ya virusi vya Korona hautarudi kuwa kama ulivyo kuwa kabla. Kwa nchi zilizo kuwa zikidhani kuwa ni waungu duniani, na kutunga kanuni na sheria kinyume na aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt) kwa Mtume Wake (saw), na kuifanya batili kuwa haki na haki kuwa batili.
Kufeli kwao kumethibitika mbele ya kiumbe kidogo mno ambacho cha karibia kutoonekana, ambacho kimewaporomosha chini, huku waking'ang'ana jinsi ya kukabiliana, na kupambana nacho, na wangali wanatapatapa katika giza la dhulma zao hadi wanashambuliwa na maneno ya Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz:
(وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً)
“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [Al-Isra’: 81].
Khilafah itapambazuka tena, ikimulika ulimwengu na kueneza kheri kote ulimwenguni,
(وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً)
“...Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra’: 51].
6 Ramadhan Al-Mubarak 1441 H
29/4/2020 M
#Covid19 #Korona كورونا#