Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  8 Rajab 1440 Na: 1440/023
M.  Jumamosi, 16 Machi 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Viongozi wa Kimagharibi Ndio Wachochezi wa Mauwaji ya New Zealand!
(Imetafsiriwa)

Mauwaji mabaya yalitekelezwa na mhalifu Brenton Tarant (kutoka Australia) mnamo Ijumaa, 15/3/2019, aliyeingia ndani ya Msikiti wa Al-Nour eneo la Christchurch, New Zealand, na kuua mashahidi 41 na kujeruhi idadi kubwa waliokuwa wakifanya ibada humo. Kisha akaenda Msikiti wa Lenwood, umbali wa maili tatu kutoka Msikiti wa Al-Nour. Matokeo ya uhalifu huu maradufu ni mashahidi 50 na majeruhi 47. Licha ya uhalifu huu wa mara mbili kuchukua dakika 45 baina yake, maafisa wa usalama hawakumzuia kutokana na utekelezaji uhalifu wake wa pili!


Gaidi huyo akachapisha manifesto yenye kurasa 74 akitoa wito kwa wengine kuiga mfano wake kuwafanyia ugaidi Waislamu walioko Magharibi kupitia kuwauwa ili kuwafanya watoke Magharibi, pasi na huruma yoyote au ubaguzi kwa watoto, wanawake na wazee … Ni wazi katika taarifa yake kuwa uhalifu wake ulikuwa ni mandhari nyengine tena endelevu ya vita vinavyo endelea vya kimsalaba. Alikuwa amekiri kuwa alipata idhini ya shambulizi hilo kutoka kwa Templar Knights, kikundi cha kimasoni kilicho asisiwa baada ya vita vya kwanza vya kimsalaba.


Lakini swali hapa ni: Je, uhalifu huu utakoma kwa kitendo cha katili huyu, kama ilivyo fanyika nyuma pindi “daktari” Baruch Goldstein, aliye wauwa watu 29 waliokuwa wakiswali swala ya alfajiri katika Msikiti wa Ibrahimi katikati mwa mwezi wa Ramadhan 1994, na kuwajeruhi 125 wengine? Kama ambavyo Waserbia walivyotekeleza mauwaji maarufu ya Srebrenica, yaliyopoteza maisha ya Waislamu 8000, ambayo yalitekelezwa machoni mwa majeshi ya Umoja wa Mataifa yaliyo “dhamini” ulinzi wa Waislamu? Na hayo hayo ndiyo yanayojitokeza kwa mauwaji ya Waislamu nchini Kashmir, Afrika ya Kati na nchini Myanmar? Au je, uovu huu utakoma kwa viongozi wa miungano ya kimataifa, walioanzisha mashambulizi 32,000 ya anga nchini Syria na Iraq chini ya kisingizio cha kupambana na ISIS, wakiwa na habari kamili ya vifo vya maelfu ya raia? Pasi na kuwataja waathiriwa wa uhalifu wa Urusi, yakiwemo mashambulizi manne ya hivi karibuni kwa raia mjini Idlib, huku Mayahudi jana wakianzisha mashambulizi 100 katika Ukanda wa Gaza!


Ndio, hakuna siri ya ukubwa wa khiyana ya kimataifa dhidi ya Waislamu popote walipo, licha ya aina zote za uhalalishaji na miito. Viongozi wa Kimagharibi kwa muda mrefu walianzisha kampeni mtawalia zinazolenga kuwamaliza Waislamu, kama ilivyotokea kwa Waamerika wanati barani Amerika. Endapo watafeli, basi lengo litakuwa ni kuwatisha na kuwabagua Waislamu na kuwalazimisha kuachana na Dini yao, kama zifanyavyo tawala za China na Turkistan Mashariki, na utawala wa Urusi inchini Urusi.


Mhalifu halisi sio mtu huyu wala yule, bali ni sera iliyo tabanniwa na viongozi wa Kimagharibi katika kuuchafua Uislamu na Waislamu ili kutia chuki katika nyoyo za watu wao. Chuki hii inajitokeza katika vitendo vya kihalifu, rasmi kupitia serikali au visio rasmi kupitia watu binafsi hapa na pale.


Mwenyezi Mungu (swt) ametuambia ukweli wa chuki za wahalifu hawa, katika maneno yake:


(وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا)


“Na hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqara: 217]


Na maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):


(قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ)


“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.”  [Al-Imran: 118]


Mwenyezi Mungu (swt) ametuonyesha njia ya kuhifadhi hadhi na fahari ya Waislamu na jinsi ya kukomesha umwagaji damu yao na kuhifadhi heshima yao, ambayo yote haya ni kwa kupitia kuwepo kwa Khalifah pekee, ambaye hutia hofu ndani ya nyoyo za maadui na kumzuia yeyote anayetaka kuudhuru Uislamu na Waislamu.


(وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ)


“Na waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua.” [Al-Anfal: 60]


Maadui hawa hufahamu lugha ya nguvu pekee. Mtume wa Mwenyezi Mungu mkweli amesema:


«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika, imam (Khalifah) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwayo.”


Enyi Waislamu, njia ya fahari yenu, mafanikio yenu na radhi za Mola wenu, imewekwa wazi kwenu. Damu yenu, hadhi yenu zitalindwa pekee na dola ya Khilafah, inayowaleta pamoja na kuunganisha nguvu yenu na kumzuia adui yenu, na kuwatoa katika hali mbaya hadi katika hali ya kuwa Ummah bora muliotolewa kwa watu.


Ewe Mwenyezi Mungu, warehemu mashahidi wetu nchini New Zealand na kila mahali na wakubalie Pepo ya juu kabisa, na tusaidie kusimamisha Khilafah karibuni kuliko baadaye, Wewe ni Mlinzi wa hilo na muweza wake.

 

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu